Iundwe Wizara ya Uchumi, Viwanda na Biashara. TRA irudishwe Hazina kama Idara ndipo tutatoboa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,607
141,429
Ni ushauri kwa bunge, wabunge na Spika mpya Dr Tulia Ackson.

Jaribuni kuishauri serikali ili mipango ya kiuchumi ihamishiwe wizara ya Viwanda na Biashara kisha ateuliwe mbunge nguli wa Uchumi, Biashara na Masoko kuendesha wizara.

TRA irudishwe Hazina kwani lengo la Sanare na Kezilahabi wakati wanaiasisi ilikuwa isimamie Mapato yote ya serikali na siyo ya kodi tu kama ilivyo sasa. Lengo hili limeshindikana na badala yake vitengo vya Forodha na kile cha Kodi za Ndani ziko kama idara za Hazina kama awali.

Ikumbukwe kutoza ushuru ni suala la kikarani hivyo lirejeshwe Hazina kama idara na mambo ya sera yatasimamiwa na Kurugenzi ya Hazina.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
 
Warudishe Tume ya Fedha na Mipango waitoe Kuwa kitengo/Idara ndani ya Wizara ya Fedha Magu hapa alibugi sana. Philip Mpango amsauri mama juu ya hili maana amehudumu Kama Katibu wa Tume ya Fedha na Mipango kwa miaka mingi, sijui kwanini anakaa kimya?
 
Hiyo wizara ya viwanda tu pekee yake ni ngumu.

Hatuoni viwanda, hata vile walivyojimilikisha enzi za ben wameshindwa kuvirejesha.

Matunda yanaoza tumeshindwa kuyasindika yote hiyo ni viwanda.

Tunashindwa hata kufanya packaging maana vifungashio hamna, yote hiyo ni viwanda na watu wapo maofisini wananawiri tu.

Kila kitu ni mchina even toothpicks

Ukiiongezea mzigo hiyo wizara haiwezi.
 
Kwa CCM hii na kwa Katiba hii inayompa mamlaka yote mtu mmoja - aisee tutasubiri sana watanzania.
 
Wazo zuri maana TRA wanalazimisha kodi bila kutengeneza mikakati na kushauri wafanyabiashara ni jinsi gani ya kuongeza mapato na kutoa Elimu juu ya biashara.

Unakuta Afisa TRA anakuja dukani kwako kuomba kodi bila ya kukuelimisha jinsi ya kuongeza kipato katika biashara yako na hapo Afisa huyo amekaa Chuo cha kodi pale Posta miaka 3
 
Uchumi,Viwanda na Biashara?John the Baptist vipi bwana mbona umejichanganya.Viwanda havi-contribute kwenye uchumi?Na bila biashara uchumi utatoka wapi na Viwanda si biashara?To me Uchumi unaletwa na biashara iwe ya bidhaa za viwandani au kilimo na hata services.

Na TRA?Ibaki kuwa an autonomous institution chini ya Wizara ya fedha,Ila kuwe na usimamizi mzuri kutoka Wizara ya Fedha,na vetting by ya watendaji iwe more rigorous.

TRA inahitaji watendaji wenye weledi na uaminifu wa hali ya juu usiotiliwa shaka,Ilivyo sasa mm.
 
....

... toka enzi hiyo sio kazi ya watoza ushuru; kukufundisha namna ya kufanya biashara? Watoza ushuru wa wapi hao wanafanya hivyo?
 
Naona tatizo ni rushwa, wizi na ulafi kwenye hayo maofisi, kila mtu anazidi kulegeza kamba aongeze urefu wa malisho.
 
Akili yako umeifunga katika mambo ya Kisiasa
sasa kwa nini mtoa hoja pamoja na wachangiaji wanahangaika hangaika mara hamisha TRA peleka Hazina - unafikiri mzizi wa tatizo upo wapi?

Tukiuliza Tanzania ya viwanda imefikia wapi hivi unaweza kujibu ?
 
Kwahiyo na CDM akiwa anaongoza nchi tukiwashauri hivyo utasema kosa ni chama na katiba?
 
Warudishe Tume ya Fedha na Mipango waitoe Kuwa kitengo/Idara ndani ya Wizara ya Fedha Magu hapa alibugi sana. Philip Mpango amsauri mama juu ya hili maana amehudumu Kama Katibu wa Tume ya Fedha na Mipango kwa miaka mingi, sijui kwanini anakaa kimya?
Hii Time hii, ilikuwa kiungo muhimu Sana!
Sijui ilitokomezwa wapi huko kusikojulikana!?
 
Ni ushauri kwa bunge, wabunge na Spika mpya Dr Tulia Ackson.

Jaribuni kuishauri serikali ili mipango ya kiuchumi ihamishiwe wizara ya Viwanda na Biashara kisha ateuliwe mbunge nguli wa Uchumi, Biashara na Masoko kuendesha wizara.

TRA irudishwe Hazina kwani lengo la Sanare na Kezilahabi wakati wanaiasisi ilikuwa isimamie Mapato yote ya serikali na siyo ya kodi tu kama ilivyo sasa. Lengo hili limeshindikana na badala yake vitengo vya Forodha na kile cha Kodi za Ndani ziko kama idara za Hazina kama awali.

Ikumbukwe kutoza ushuru ni suala la kikarani hivyo lirejeshwe Hazina kama idara na mambo ya sera yatasimamiwa na Kurugenzi ya Hazina.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Mheshimiwa, ni haki yako ya kikatiba kupendekeza jambo lo lote unaloona lina manufaa kwa taifa. Lakini haya unayopendekeza ama yanaturudisha nyuma au huelewi unachopendekeza. Kwa kifupi ni kwamba; kwanza, mapungufu ya watendaji ya kutokuwa na uwezo wa kazi husika, kuwa wabadhirifu au wavunja sheria hayarekebishiki kwa kubadili mfumo peke yake. Pili, kwenye muundo wa wizara, unapendekeza kukusanya shughuli zinazofanana chini ya wizara moja; lakini TRA unapendekeza kutawanya shughuli za ukusanyaji fedha ambazo zinafanana ziwe kwenye sehemu za utawala tofauti. Mapendekezo yako yanapingana Tatu, Uchumi ni suala la sekta nyingi kuliko viwanda na biashara. Kwa mtazamo wako huo wa wizara ya uchumi, wizara zaidi ya sita zinatakiwa zikusanywe chini ya wizara moja! Mwisho, kuna wizara mtambuka na wizara ambazo majukumu yake hayazifungi wizara nyingine. Mfano wa wizara mtambuka ni wizara ya fedha na mipango, wizara ya sheria, wizara ya mambo ya ndani na wizara ya mambo ya nje. Sasa hiyo wizara unayopendekeza ungependa iwe upande upi. Watu wengi,hata viongozi wa siku hizi, hawaelewi mantiki inayounda idara za Serikali na baadhi ya makosa ya kiutendaji yanatokana na kuchokonoa miundo hiyo bila kupima faida na hasara ya kuibadilisha. Kwa hiyo kama unapeleka mapendekezo, basi peleka hoja yenye mchanganuo na pia hasara na faida za mfumo unaoukataa na faida ya mfumo unaopendekeza.
 
Hiyo wizara ya viwanda tu pekee yake ni ngumu.

Hatuoni viwanda, hata vile walivyojimilikisha enzi za ben wameshindwa kuvirejesha.

Matunda yanaoza tumeshindwa kuyasindika yote hiyo ni viwanda.

Tunashindwa hata kufanya packaging maana vifungashio hamna, yote hiyo ni viwanda na watu wapo maofisini wananawiri tu.

Kila kitu ni mchina even toothpicks

Ukiiongezea mzigo hiyo wizara haiwezi.
Toothpick zinatengenezwa Tanzania kwa sasa naona urekebishe lawama yako happ dear
 
Uchumi,Viwanda na Biashara?John the Baptist vipi bwana mbona umejichanganya.Viwanda havi-contribute kwenye uchumi?Na bila biashara uchumi utatoka wapi na Viwanda si biashara?To me Uchumi unaletwa na biashara iwe ya bidhaa za viwandani au kilimo na hata services.

Na TRA?Ibaki kuwa an autonomous institution chini ya Wizara ya fedha,Ila kuwe na usimamizi mzuri kutoka Wizara ya Fedha,na vetting by ya watendaji iwe more rigorous.

TRA inahitaji watendaji wenye weledi na uaminifu wa hali ya juu usiotiliwa shaka,Ilivyo sasa mm.
Huku veta nako kuna mtu anaitwa nacte kavamia mtaa
 
Back
Top Bottom