Iundwe team kutoka kitengo itakayohakiki upya waajiriwa hewa

Observe

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
294
140
Kwanza kabisa nitoe pongezi za dhati kwa Raisi ambaye kwa nia njema na dhamira safi amejipambamua kuwa ni mtumishi wa watanzania wote bila ujanja na ulaghai kama wenzake waliomtangulia.

Kashifa za wafakazi hewa zimesikika kwa miaka mingi sana lakini mamlaka zilipoita hazikuonyesha kuguswa na hujuma mbaya hii, na kwamanahiyo kwa mda mwingi serikali imekuwa ikipoteza mabilioni kila mwaka kulipa mishahara hewa hivyo kupelekea wakurugenzi kunufaika binafsi. Na inapotokea mtumishi amefukuzwa kazi ama emafariki dunia, kwa makusudi kabisa taarifa zimekuwa hazitolewi na kisha wakurugenzi kuhodhi hiyo mishahara na kuiweka kwenye akaunti zao.

Baada ya agizo la Raisi kwamba kila mkuu wa mkoa apitie upya majina na idadi kamili ya watumishi wa umma kwa kila mkoa na wilaya, kazi hiyo imefanyika na taarifa tayari zimekabidhiwa kwa mamlaka husika zikiwa na idadi ya watumishi hewa.

Lakini kumetokea sitofahamu na kigugumizi juu ya ukweli halisi wa jinsi hali ilivyo, inawezekana kabisa kwa baadhi ya wakuu waikoa ama kwakuwalinda wakurugenzi na hii dhahama au kwa makusudi ya kukwamisha juhudi za Raisi wameamua kutoweka idadi kamili ya watumishi hewa. Tatizo la mishahara hewa ni sugu na linamasilahi makubwa kwa baadhi ya wakurugenzi na wakuu wa wilaya na mikoa na hivyo hawajalifanyia kazi kama agizo lilivyowataka. Nimejaribu kujiuliza labda pengine Raisi aliwapa mda mchache sana kiasi kwamba wamelifanya zoezi hili kwa kukimbia mno wakiogopa endapo hawatakailisha kwa mda uliopangwa wangekumbana na panga kama majipu.

Kwahiyo napendekeza iundwe tume nyingine toka usalama wa taifa itakayo fanyia kazi swala hili huku ikiwachunguza baadhi ya wakuu wa mikoa/wilaya na wakurugenzi uadilifu wao juu ya jambo hili kwakuwa waliapishwa ma wakakubali kulitekeleza kwa kiwango Raisi anataka. Naamini tutakujasikia zaidi ya wafanyakazi hewa wengine zaidi ya 2000 nchi nzima.

Pendekezo jingine langu ni kwamba: Sasa ni wakati mwafaka kwa serikali kuwasajili watumishi wa umma kwa njia ya ki-electronic na wapewe vitambilishp kama zilivyolazi za ATM vikiwa na neno la siri, pia wawe wanavi update kila mwezi kiasi kwamba makao makuu itawatambua kupitia password zao na endapo mrumisho atashindwa kua update kadi yake kwa kila mwezi basi atakuwa amejifuta mwenyewe kwakuwa mishahara ya kila mwezi itatolewa kwa walio ipdate tu nahivyo kuiwezesha makao makuu kuwatambua watumishi wote kwa urahisi.

Ili kufanikisha zoezi hili ni lazima serokali itaweka mashine kwa kila halimashauri, manispaa, na majijini mahali ambapo mtumishi atatakiwa kuingiza kadi yake na password yake kwa ajili ya kuia update kadi yake kila mwezi, hii inamaanisha kwamba amabaye hata update kadi yake kwa mda uliopangwa tayari ataifuta kwa utumishi. Na ikitokea mtu akaugua basi itambidi mke wake mtu mwingine wa karibu atafanya hoyi kazi kwakuwa kua update siyo kuchukua mshahara kwahiyo haitaleta utata au wasiwasi kwa wahusika, ikibidi mtumishi aweza kua update kadi yake kwa kurumia simu yake ya mkononi kuingiza namba za kadi yake na neno la siri kwakuwa kadi hii itabeba taarifa zote za muhusoka, mke au mme wake na watoto wake ili ikitokea kwa bahati akafa ghafla kwa ajali basi mme/mke au watu wakaribu ambao majina yao yamerekodiwa kwenye hiyo kadi wataweza kufutalia haki ya ndugu yao na wakaipata bila usumbufu wowote.

Ni kama tu vile mtu anapojiunga na mifuko ya jamii kwa ajili ya mafao anavyoandilisha majina ya watu watakao weza kuhusika na mafao yake endapo atafariki ghafla.Nasema hivyo kwasababu jambo hili la wakazi hewa limewaghalimu watanzania mabilioni ya shilingi kwa miaka mingi, nahii ijumulishe na mashirika yote ya umma. Mfano mdogo kwenye hizi hela za TASAF, yaani watu wameandishwa hata wale ambao hawana sifa za kuchukua huo mgao; kuna jirani yangu ni mfanyakazi tena mwajiliwa kwenye shule moja ya binafisi na umri wake ni miaka 40 eti naye anachukua TASAF kila baada mwezi moja kisa ni balozi wa nyumba kumi. Sasa hapo sijaelewa kama mabalozi wa nyumba kumi wana free entrance kwenye mfuko huu.
Hebu fikiria ni watu wangapi wanavuta hii hela, kule vijijini si ajabu ukakuta wenyeviti wa vijiji wameandikisha mpaka majina ya ndugu zao au majina hewa na hivyo kupelekea mfuko huu kutowanufaisha walengwa

Naamini hii itapunguza au kumaliza kabisa ukilitimba unapfanywa na baadhi ya wakurugenzi wasio waaminifu katika utumishi wao.

NAOMBA KUWASILISHA KWENU WAKUU (NOT ONLY GREAT THINKERS BUT ALSO GREATEST THINKERS).

NB.
Sehemu ya kurekibisha na irekebishwe tu, kama kunanyongeza ama sikufikia takwa la maada pia wakuu mwaweza kuongezea njinsi ya kufanya lengo ni kuondoa watumishi hewa hali inayoleta hasara kwa serikali na Taifa kwa ujumla.
 
Wazo zuri ila sina hakika kama litatekelezeka hasa kwa wenzangu wa kule Nanyumbu kwa Mmawia
 
wazo zuri ila 85% ya wafanyakazi hawajui neno "update" sasa ikiwa ni kila mwezi kutakuwa na msururu wa kesi za mishahara then jamaa wa IT watapiga hela aje!!!!
 
Wazo zuri ila sina hakika kama litatekelezeka hasa kwa wenzangu wa kule Nanyumbu kwa Mmawia
Kwenye maada zinazohusu masilah makubwa ya Taifa kwa ujumla huwa unaweka kejeli ili kuvuruga mjadala...sasa hapa kumwita mtu nyumbu inahusika vipi na hoja ya mtoa maada punguzeni ushabiki wa kivyama katika maslahi mapana ya Taifa...kwani Mmawia anazuia vipi kuunda tume huru ya kuchunguza Mishahara hewa..
 
Nakubaliana na wazo la mleta maada..japo muda mwingine yawezekana aliyekuwa anakagua(mkuu wa mkoa) ndio mnufaika ya hyo mishara au alipgiwa pande mpaka akaupata huo ukuu wa mkoa kupitia kwa yule anayemkagua...kwahiyo naungana na mtoa maada kuwa hii kazi ingefanywa na USALAMA WA TAIFA
 
Dawa ni kuweka makamanda wa JWTZ kuwa wakuu wa mikoa na wilaya kama akina Brig. Maganga na Maj. Gen Kijuu, tunao wengi sana rais Magufuri awachukue na kuwakabidhi kazi uone kama kuna ushenzi utaendelea. Makamanda wa jeshi nidhamu na uzalendo ndio sifa yao namba moja.
 
Bravo! Hili zoezi limefanikiwa kwa 25% tu...Zoezi limefanyika bila ya kuwahusisha wakuu wa idara mfano wakuu wa mashule wanapaswa kupekela taarifa sahihi za watumishi waliopo kazini vivyo hivyo na idara zingine....wakifanya hivi kuna watumishi hewa wengi mno watagundulika.....Pili uongozi husika yani AFISA UTUMISHI,AFISA ELIMU NA MKURUGENZI,M/WILAYA wapite kwa awamu ya pili kituo kwa kituo apo watagundua hili zoezi la mara ya kwanza kumbe halikufanukiwa kwa kiwango kizuri....wanufaika na hii mishahara hewa ni wakuu wa idara wakishirikiana na ma wakurugenzi.....
 
PIA MIE NINGEOMBA WAZEE WA KITENGO PIA WAMSAIDIE RAIS KWA KWENDA BODI YA MIKOPO KUHAKIKI USAHIHI WA WANAFUNZI WANAOPEWA MIKOPO.NAAMINI WATAKUTA WANAFUNZI HEWA WENGI WANAMIKOPO 100% NA HAWAPO VYUONI.
 
Dawa ni kuweka makamanda wa JWTZ kuwa wakuu wa mikoa na wilaya kama akina Brig. Maganga na Maj. Gen Kijuu, tunao wengi sana rais Magufuri awachukue na kuwakabidhi kazi uone kama kuna ushenzi utaendelea. Makamanda wa jeshi nidhamu na uzalendo ndio sifa yao namba moja.
Ni kweli kabisa aisee lkn kabla ya hapo mh. JPM aunde tume ya kuchunguza vyeti vya wanajeshi +polisi ili tujue nidhamu yao ni ya kweli mpk Kwny vyeti vyao.
 
Dawa ni kuweka makamanda wa JWTZ kuwa wakuu wa mikoa na wilaya kama akina Brig. Maganga na Maj. Gen Kijuu, tunao wengi sana rais Magufuri awachukue na kuwakabidhi kazi uone kama kuna ushenzi utaendelea. Makamanda wa jeshi nidhamu na uzalendo ndio sifa yao namba moja.
Mbona hata hao wakubwa wa Jeshi ni wapigaji tu wanavuta vitambi tu......hebu kawaulize askari wa vyeo vya chini usikie wanavyolia juu ya wakubwa zao wanavyotafuna pesa zao.......unamkumba Balozi wa China Shimbo?? ha ha ha ha!!!
 
Hata hao watu wa TISS nao hawaaminiki kwa 100% inabidi tume hiyo iundwe kwa kushirikisha watu tofauti kutoka wafanyakazi wa kawaida kutoka vyombo vingine vya ulinzi na usalama kama Polisi,JWTZ,Magereza etc......kwa sababu hao TISS wangekuwa wako vizuri wizi kama wa EPA,ESCROW na meengine meengi tu visingetokea kwa hiyo nao wana matatizo yao si wa kuamini kwa asilimia zote!!!
 
PIA MIE NINGEOMBA WAZEE WA KITENGO PIA WAMSAIDIE RAIS KWA KWENDA BODI YA MIKOPO KUHAKIKI USAHIHI WA WANAFUNZI WANAOPEWA MIKOPO.NAAMINI WATAKUTA WANAFUNZI HEWA WENGI WANAMIKOPO 100% NA HAWAPO VYUONI.
Hapa kuna points
 
Mimi wazo langu liko hivi, kuna vijana wengi tu wamemaliza vyuo vikuu hawana ajira. Wangepewa kazi ya kufuatilia hilo suala kwani wao bado hawajaingia kwenye hiyo michezo ya wizi serekalini. Upatikanaji wao uwe ni wa kuomba, kisha ule mkoa uliotumia kuomba unahamishwa kwenda mkoa mwingine ili kuepuka kurubuniwa. Wakapitie kwa uhakika kisha hatua stahiki zichukuliwe kwa wale wote waliokuwa wakishiriki mchezo huu wa mishahara hewa.
 
Kwanza kabisa nitoe pongezi za dhati kwa Raisi ambaye kwa nia njema na dhamira safi amejipambamua kuwa ni mtumishi wa watanzania wote bila ujanja na ulaghai kama wenzake waliomtangulia.

Kashifa za wafakazi hewa zimesikika kwa miaka mingi sana lakini mamlaka zilipoita hazikuonyesha kuguswa na hujuma mbaya hii, na kwamanahiyo kwa mda mwingi serikali imekuwa ikipoteza mabilioni kila mwaka kulipa mishahara hewa hivyo kupelekea wakurugenzi kunufaika binafsi. Na inapotokea mtumishi amefukuzwa kazi ama emafariki dunia, kwa makusudi kabisa taarifa zimekuwa hazitolewi na kisha wakurugenzi kuhodhi hiyo mishahara na kuiweka kwenye akaunti zao.

Baada ya agizo la Raisi kwamba kila mkuu wa mkoa apitie upya majina na idadi kamili ya watumishi wa umma kwa kila mkoa na wilaya, kazi hiyo imefanyika na taarifa tayari zimekabidhiwa kwa mamlaka husika zikiwa na idadi ya watumishi hewa.

Lakini kumetokea sitofahamu na kigugumizi juu ya ukweli halisi wa jinsi hali ilivyo, inawezekana kabisa kwa baadhi ya wakuu waikoa ama kwakuwalinda wakurugenzi na hii dhahama au kwa makusudi ya kukwamisha juhudi za Raisi wameamua kutoweka idadi kamili ya watumishi hewa. Tatizo la mishahara hewa ni sugu na linamasilahi makubwa kwa baadhi ya wakurugenzi na wakuu wa wilaya na mikoa na hivyo hawajalifanyia kazi kama agizo lilivyowataka. Nimejaribu kujiuliza labda pengine Raisi aliwapa mda mchache sana kiasi kwamba wamelifanya zoezi hili kwa kukimbia mno wakiogopa endapo hawatakailisha kwa mda uliopangwa wangekumbana na panga kama majipu.

Kwahiyo napendekeza iundwe tume nyingine toka usalama wa taifa itakayo fanyia kazi swala hili huku ikiwachunguza baadhi ya wakuu wa mikoa/wilaya na wakurugenzi uadilifu wao juu ya jambo hili kwakuwa waliapishwa ma wakakubali kulitekeleza kwa kiwango Raisi anataka. Naamini tutakujasikia zaidi ya wafanyakazi hewa wengine zaidi ya 2000 nchi nzima.

Pendekezo jingine langu ni kwamba: Sasa ni wakati mwafaka kwa serikali kuwasajili watumishi wa umma kwa njia ya ki-electronic na wapewe vitambilishp kama zilivyolazi za ATM vikiwa na neno la siri, pia wawe wanavi update kila mwezi kiasi kwamba makao makuu itawatambua kupitia password zao na endapo mrumisho atashindwa kua update kadi yake kwa kila mwezi basi atakuwa amejifuta mwenyewe kwakuwa mishahara ya kila mwezi itatolewa kwa walio ipdate tu nahivyo kuiwezesha makao makuu kuwatambua watumishi wote kwa urahisi.

Ili kufanikisha zoezi hili ni lazima serokali itaweka mashine kwa kila halimashauri, manispaa, na majijini mahali ambapo mtumishi atatakiwa kuingiza kadi yake na password yake kwa ajili ya kuia update kadi yake kila mwezi, hii inamaanisha kwamba amabaye hata update kadi yake kwa mda uliopangwa tayari ataifuta kwa utumishi. Na ikitokea mtu akaugua basi itambidi mke wake mtu mwingine wa karibu atafanya hoyi kazi kwakuwa kua update siyo kuchukua mshahara kwahiyo haitaleta utata au wasiwasi kwa wahusika, ikibidi mtumishi aweza kua update kadi yake kwa kurumia simu yake ya mkononi kuingiza namba za kadi yake na neno la siri kwakuwa kadi hii itabeba taarifa zote za muhusoka, mke au mme wake na watoto wake ili ikitokea kwa bahati akafa ghafla kwa ajali basi mme/mke au watu wakaribu ambao majina yao yamerekodiwa kwenye hiyo kadi wataweza kufutalia haki ya ndugu yao na wakaipata bila usumbufu wowote.

Ni kama tu vile mtu anapojiunga na mifuko ya jamii kwa ajili ya mafao anavyoandilisha majina ya watu watakao weza kuhusika na mafao yake endapo atafariki ghafla.Nasema hivyo kwasababu jambo hili la wakazi hewa limewaghalimu watanzania mabilioni ya shilingi kwa miaka mingi, nahii ijumulishe na mashirika yote ya umma. Mfano mdogo kwenye hizi hela za TASAF, yaani watu wameandishwa hata wale ambao hawana sifa za kuchukua huo mgao; kuna jirani yangu ni mfanyakazi tena mwajiliwa kwenye shule moja ya binafisi na umri wake ni miaka 40 eti naye anachukua TASAF kila baada mwezi moja kisa ni balozi wa nyumba kumi. Sasa hapo sijaelewa kama mabalozi wa nyumba kumi wana free entrance kwenye mfuko huu.
Hebu fikiria ni watu wangapi wanavuta hii hela, kule vijijini si ajabu ukakuta wenyeviti wa vijiji wameandikisha mpaka majina ya ndugu zao au majina hewa na hivyo kupelekea mfuko huu kutowanufaisha walengwa

Naamini hii itapunguza au kumaliza kabisa ukilitimba unapfanywa na baadhi ya wakurugenzi wasio waaminifu katika utumishi wao.

NAOMBA KUWASILISHA KWENU WAKUU (NOT ONLY GREAT THINKERS BUT ALSO GREATEST THINKERS).

NB.
Sehemu ya kurekibisha na irekebishwe tu, kama kunanyongeza ama sikufikia takwa la maada pia wakuu mwaweza kuongezea njinsi ya kufanya lengo ni kuondoa watumishi hewa hali inayoleta hasara kwa serikali na Taifa kwa ujumla.

Hongera ndugu kwa fikra ambazo umeziandaa kwa uzalendo na kupenda kusaidia kwaajili ya kutatua tatizo, binafsi, si mfuasi sana wa kuunda tume au timu zingine kwa ajili ya kubaini yaliyomo humo.

Naamini kwamba Mh. JPM anozo taarifa zote tayari mezani na yeyote atakayejaribu kupotosha atakuwa sehemu ya mfano mbaya.

Nije kwenye "control" uliyoigusia, automated control. Ukiazingatia kwamba hawa watu ni walewale, na mawazo yao ni kutatua kila mpango kama ni tatizo kwao. Nikumbushe kwamba mpaka ss, utakuta waalimu wanampa mmoja wao ATM card zao ili akawachukulie fedha. Kwa hiyo, watatengeneza tu mazingira, kwa kuwa hawatakuwa wanaonekana, wawape watu vitambulisho na password wafanye kama wale ambao hawatakiwi kuwapo.

Kuna aina mbalimbali za "controls" ambapo mamlaka inaweza kuzitumia, nyingine ni (preventive, detective au corrective)
nyingine ni manual au automated n.k.
Control muhimu, ambayo inaendelea kusaidia mpaka sasa ni ukaguzi wa ndani na nje usio na maslahi (objective and independent audits), ambazo report zake zipo siku zote, zikieleza kwa mapana matatizo yote, pamoja na haya ya wafanyakazi hewa, lakini taarifa zimekuwa zikiangaliwa, na kugeuzwa na kutengenezewa makabati makubwa bila kusomwa na kufanyiwa kazi.
#Wangwana tunashukuru kwamba hawa watuhumiwa hawakupata akili za kuzichoma moto au kuzipoteza.

Na usalama wa taifa wapo kila mahala, ndo maana taarifa hata za wale wakaguzi wanaoweza kuhongwa na kupotoshwa ukweli zinafikishwa kama zilivyo kwa mh.

Nafikiri kwamba tusubiri tuone, hii kitu si ndogo mkuu, zingatia kwamba wote wanaohusika watawajibika... na ni wote, so tutegemee anguko kubwa la wale waliohusika kwa kipindi chote, na kuokoa pesa kwa mabilioni zinazohusika na mishahara hewa.
 
Back
Top Bottom