ITV Washindwa Kuliandika kwa Usahihi Jina la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi

Kichankuli

JF-Expert Member
Dec 18, 2008
887
189
Inashangaza chombo cha habari kikubwa kama ITV kinalikosea kuliandika jina la Mwenyeketi wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu Damiani Lubuva na kumwita Damian Luduva. Hili nimeliona katika kipindi cha matukio ya wiki ambacho kinaendelea hivi sasa. Kwa vile haya ni matukio ya wiki inamaana kipindi hiki kilirushwa siku za nyuma kati ya jumatatu haji jumamosi ya wiki hii, sina uhakika kama hawakugundua kosa hilo na hivyo kulifanyia masahihisho ama ni udhaifu wa utamkaji wa maneno alionao aliyeandika habari hiyo. Lakini Mhariri wa kipindi naye yuko wapi.
 
Wacha kulaumu bila sababu,kukosea kila mtu anakosea.
mbona wewe umeandika YUME badala ya Tume,kama wao wamekosea kwenye kuzungumza,wewe umekosea kwenye kuandika,nyie wote ni kitu kimoja
 
kile kipind kilirekodiwa hvyo kinarushwa kama kilivyorushwa mwanzo. Pia hzo ni typing error tu kama wewe ulivyoandika YUME badala ya TUME.
 
Inashangaza chombo cha habari kikubwa kama ITV kinalikosea kuliandika jina la Mwenyeketi wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu Damiani Lubuva na kumwita Damian Luduva. Hili nimeliona katika kipindi cha matukio ya wiki ambacho kinaendelea hivi sasa. Kwa vile haya ni matukio ya wiki inamaana kipindi hiki kilirushwa siku za nyuma kati ya jumatatu haji jumamosi ya wiki hii, sina uhakika kama hawakugundua kosa hilo na hivyo kulifanyia masahihisho ama ni udhaifu wa utamkaji wa maneno alionao aliyeandika habari hiyo. Lakini Mhariri wa kipindi naye yuko wapi.

Wewe mwenyewe umeshindwa kuliandika neno TUME!UMEANDIKA YUME!!
 
kukosea kitu cha kawaida. Mbona wewe mwenyewe umekosea heading?.
 
Liondoe kwanza boriti lililo katika jicho lako kabla ya kuona boriti lililo ktk jicho la mwenzio,
anyway hana umuhimu wowote huyo kitaifa,
 
nahisi umetumwa akikosewa jina lake ana umuhimu gani kwako na kwa watanzania r u normal?? sorry whr r u first may be we ar talking with our colleague frm mirembe by the way we luv u all
 
Tuache kupenda sifa na kufuata mikumbo. Kweli huyu ndugu yetu kakosea kuandika na hilo ni dhahiri, lkn sidhani kama ni justification ya ITV kuandika majina hovyo. ITV ni chombo cha habari ambacho nategemea kiwe serious kwenye kazi. Huyu bwana wakati anaandika nadhani alikuwa peke yake na simtetei lkn tutambue kuwa si muandishi huyu.

ITV (tuseme vyombo vyetu vingi vya habari hapa TZ) wamekuwa na mistakes za namna hii nyingi. Si kwenye kuandika tu, hata matamshi. Kuna watangazaji kadhaa wa kike (siwajui majina) wa Radio One hawawezi kusoma kwa ufasaha neno 'KUTELEKEZA' na badala yake huishi kusema 'KUTEKELEZA'. Kwa kweli ni kichefuchefu kwa msomaji ambaye naamini alichaguliwa kushika nafasi aliyonayo kwa kuwa alifaulu vizuri lugha (kigezo muhimu) na lugha anayoongea ndio lugha yetu ta Taifa.

Cha pili ni uelewa wa waandishi na vipindi wanavyopewa. Ni dhambi kubwa kwa presenter kutokuwa na informations za kutosha juu ya nini kinaendelea duniani na nani ni nani na nani kafanya nini. Siku fulani miaka miwili au mitatu iliyopita, somebody Kitenge wa Radio One kwenye kipindi cha michezo aliongea kichefuchefu ambacho kamwe sitasahau.
Mchezaji wa washika bunduki wa London, Arsenal, M'brazil Jose Eduardo dos Santos (kwa mbwembwe nyingi na madaha) amekumbwa na tafrani ya aina yake baada ya mguu wake wa kushoto/kulia kuvunjika.........

Taabu yangu iko kwenye RED. Kama presenter wa kipindi cha michezo ililazimu awe na uelewa wa kutosha juu ya mambo ya michezo. Timu, nchi zinakotoka, majina ya makocha na wachezaji (sisemi wote lkn angalau kwa kiasi fulani) n.k. Haya basi na tuseme ana ugeni na Eduardo da Silva (ambaye ndie mchezaji wa Arsenal aliyeumia) lkn kama mwanahabari, ameshindwa kweli kujua kuwa Eduardo dos Santos aliyemsema ni Rais wa Angola? Huu ni uzembe kazini.

Hapo hapo Radio One, yupo mwingine anaitwa Isack Gamba. Huyu madudu yake yeye ni kwenye matumizi ya lugha. Mimi ninayefahamu fasihi ananichefua vilivyo na sentensi za namna hii "Timu ya soka ya Simba ya DSM leo imefanikiwa kufungwa magoli ......." (ashakhum si maneno machafu) huu ni upumbavu. Unaposema Simba wamefanikiwa kufungwa, ina maana Simba walienda uwanjani lengo likiwa ni kufungwa? Watu wa namna hii wamesoma wapi jamani?

Sasa mimi sioni suala la kumshambulia muanzisha mada. Waandishi wetu ni wazembe na presenters ni absent minded people. Mara ngapi unaangalia tamthilia wanaonesha episode ya jana yake na wala hawashituki?

Hata mkuu wa mkoa wa DSM baadhi yao wanamtamka kama Sadik Meck Sadik sijui kama ni sahihi, ofisini kwake ameandikwa Said Meck Sadiq sasa sijui ni nani hayuko sahihi. Tuache kushambuliana, tushambulie huu ukihiyo makazini.
 
Maandishi kibaaao Pumba tupu!!!
 
Naomba wachangiaji wote mlio mkandia mwenye mada wapi kaandika yume,msiwe wanafiki.
Huu ni ujanja wa kitoto kabisa tena wewe ndio mnakfi namba moja, yaani unaedit heading yako halafu unafunguwa ID nyingine unajiona mjanja kumbe bwegge tu. tunakuangalia tunakusanifu tu.

user-online.png
mdegela

Today 08:55
#17
Junior Member Array

Join Date : 27th February 2012
Posts : 1
 
Back
Top Bottom