Nilimwona mzee Mengi wiki jana kwenye TV, amebadilika. Sio sura ya mzee wetu aliyekuwa na furaha zamani.
Siku hizi hata michango michango, siisikii.
Ule uchaguzi uliharibu mambo mengi sana! Japo mzee alishtuka mwishoni, akajitenga na wazee wa ukuta.
Lakini, it was too late, alishachora mstari, na ukaonekana.
Mwiba mwingine ni kurudishwa kwa mzee wa REA, ambaye alikuwa anaonekana anamzibia asipate kitalu na kufaidi gesi.
ITV kwa kweli wamepwaya sana siku hizi, habari unayoitegemea kuiona kwenye taarifa ya habari, inakuwa haipo.