ITV: Vijiji 119 kukumbwa na njaa mkoani Mwanza

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Zaidi ya wakazi laki nne wa vijiji 119 vya wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza wanakabiliwa na baa la njaa, kufuatia hekta laki moja za mazao ya chakula, yakiwemo Mahindi na Viazi vitamu zilizolimwa wakati wa mvua za vuli msimu wa kilimo wa 2016/2017, kukauka mashambani kutokana na ukame uliokumba wilaya hiyo.
source; ITV Facebook page.
 
Wewe mkuu mchochezi, nani kakupa idhini ya kutangaza baa la njaa? Utatumbuliwa!! Lile jamaa lilishatangaza mapema halitoi chakula cha Msaada!
 
Siyo jambo geni.

Kwenye maghala kumejaa vyakula vya kutosha. Watapatiwa.
 
Hao wapo ikulu, wanachezea nyumbani hivyo watarajie kutunzwa. Kila kona ya nchi ndio kupo hivyo......subra tafadhali. Huwezi ukazuia kuomba/kupokea misaada ya chakula. Mungu hadhihakiwi kabisa, hata kama una kila kitu bado unahitaji kusaidiwa. Hata wafanyabiashara wakubwa japo wana pesa kuna vitu vingine husaidiwa bure na serikali yao, rejea!
 
Siyo jambo geni.

Kwenye maghala kumejaa vyakula vya kutosha. Watapatiwa.
Simu...mbona vyakula kwenye maghala ni vichache SNA havitoshi ndugu yangu..NFR wanayo akiba mdogo..as per BOT report first qourter ya Mwaka huu wa hela.
 
Wazee wa nchi hii hebu mwambieni Mkulu atengue kauli yake maana hasira za mola juu yetu kuhusu njaa zitakuwa hazibebeki. Tunaweza kuchapwa na njaa hapa ili tuu kupimwa mizani ya maneno yake.
Labda kuna watakao kuwa wanaimba "ccm ni ile ile , ooh ni ile ile!" Mpaka wanakata roho kwa njaa.
Au hii inahusiana na ile methali ya "adui yako mwombee njaa?"
 
FB_IMG_1483799526089.jpg
 
Zaidi ya wakazi laki nne wa vijiji 119 vya wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza wanakabiliwa na baa la njaa, kufuatia hekta laki moja za mazao ya chakula, yakiwemo Mahindi na Viazi vitamu zilizolimwa wakati wa mvua za vuli msimu wa kilimo wa 2016/2017, kukauka mashambani kutokana na ukame uliokumba wilaya hiyo.
Mungu atailipia kanda ya ziwa kwa usaliti wao .
 
Kilimo cha kutwgemea mvua sasa hakina tija, twende katika umwagiliaji tu. Wizara ya kilimo waelekeze nguvu huko, fedha (benki ya kilimo) na wataalam wakatumie mito na maziwa yetu vilivyo
 
Waziri wa Kilimo na Chakula is another hopeless creature in this Country.

Juzi anambishia ZZK kuwa hali ya chakula ni nzuri.

Haya huko huko kwenu Mwanza ndio kuna njaa.
 
Zaidi ya wakazi laki nne wa vijiji 119 vya wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza wanakabiliwa na baa la njaa, kufuatia hekta laki moja za mazao ya chakula, yakiwemo Mahindi na Viazi vitamu zilizolimwa wakati wa mvua za vuli msimu wa kilimo wa 2016/2017, kukauka mashambani kutokana na ukame uliokumba wilaya hiyo.
source; ITV Facebook page.

Wewe umeambiwa na nani kuandika controversial information? Huogopi kubambikwa kesi ya uchochezi?

Andiak hivi, pamoja na kukosekana kwa mvua mwaka huu mkoani Mwanza, wananchi wake wote wanachakula tele na wanaomba wapewe taraibu za kukipeleka nchi za nje ili kusaidia wenye njaa.

Unachokiandika hicho sasa hivi utapotea hapa mitandaoni. Angalia sana.
 
Back
Top Bottom