Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,304
- 12,965
Mimi ni mmoja wa watumiaji wa king'amuzi cha Dstv na hivi karibuni nimefurahishwa kwa kituo cha ITV kurusha matangazo yake kupitia king'amuzi hicho cha Dstv. Pamoja na furaha hiyo lakini nakereka sana na jinsi picha za vituo vya TBC, Channel 10, Star TV, ITV na baadhi ya vingine vya nje kurusha matangazo yao huku wakiweka vivuli upande wa juu, chini, pembeni kushoto na kulia ili kupunguza ukubwa wa muonekano wa picha. Kwa kweli mimi huwa nakereka sana kupunguza ukubwa wa picha kwa kuweka vivuli vyeusi hivyo kufanya sreen ionekane ndogo. Imagine mtu ana sreen ya nchi 14 halafu picha inakuja ikwa imepunguzwa ukubwa kwa njia ya kuweka vivuli si ataishia kuchungulia picha kama yuko shimoni? Mimi nataka picha ionekane full screen sio kupunguza kana kwamba mtazamaji hapendi kuaangalia picha ikiwa kubwa. Sasa tunanunua sreen kubwa za nini kama matangazo yanapunguzwa ukubwa?
Nimejaribu kuuliza watu inakuwaje baadhi wakaniambia ni zoom lakini function hiyo haipo kwenye remote yangu. Lakini ninachojiuliza ni kuwa mbona picha za matangazo ya mipira Super sport, Aljazeera, BBC, WBS, nk yanakuja picha zikiwa full sceen? na mbona picha pia za vituo vingine zinaonekana full sreen? Mimi naona setting za hivyo vivuli zinatoka moja kwa moja studio ndio maana sio rahisi kuzizoom. Mimi naomba kwa TV zetu za ndani rekebisheni picha zenu zije zikiwa full sreen vinginevyo mtupe maelezo kama ni moja ya mashrti mliyopewa kupunguza nafasi ya picha kwa kuweka vivuli. Kweli haya mavivuli mnayoweka yana bore sana. Nitafurahi kupata maelezo ya kitaalamu ya kwanini picha zinakuja na margin nyeusi wakati mwingine juu na chini au kushoto na kulia na wakati mwingine pande zote za screen yaani juu, chini, kushoto na kulia,