ITV, TBC, Channel 10 na Star TV: Kwanini mnaweka vivuli ili kupunguza ukubwa wa picha?!

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
12,941
2,000
Mimi ni mmoja wa watumiaji wa king'amuzi cha Dstv na hivi karibuni nimefurahishwa kwa kituo cha ITV kurusha matangazo yake kupitia king'amuzi hicho cha Dstv. Pamoja na furaha hiyo lakini nakereka sana na jinsi picha za vituo vya TBC, Channel 10, Star TV, ITV na baadhi ya vingine vya nje kurusha matangazo yao huku wakiweka vivuli upande wa juu, chini, pembeni kushoto na kulia ili kupunguza ukubwa wa muonekano wa picha. Kwa kweli mimi huwa nakereka sana kupunguza ukubwa wa picha kwa kuweka vivuli vyeusi hivyo kufanya sreen ionekane ndogo. Imagine mtu ana sreen ya nchi 14 halafu picha inakuja ikwa imepunguzwa ukubwa kwa njia ya kuweka vivuli si ataishia kuchungulia picha kama yuko shimoni? Mimi nataka picha ionekane full screen sio kupunguza kana kwamba mtazamaji hapendi kuaangalia picha ikiwa kubwa. Sasa tunanunua sreen kubwa za nini kama matangazo yanapunguzwa ukubwa?

Nimejaribu kuuliza watu inakuwaje baadhi wakaniambia ni zoom lakini function hiyo haipo kwenye remote yangu. Lakini ninachojiuliza ni kuwa mbona picha za matangazo ya mipira Super sport, Aljazeera, BBC, WBS, nk yanakuja picha zikiwa full sceen? na mbona picha pia za vituo vingine zinaonekana full sreen? Mimi naona setting za hivyo vivuli zinatoka moja kwa moja studio ndio maana sio rahisi kuzizoom. Mimi naomba kwa TV zetu za ndani rekebisheni picha zenu zije zikiwa full sreen vinginevyo mtupe maelezo kama ni moja ya mashrti mliyopewa kupunguza nafasi ya picha kwa kuweka vivuli. Kweli haya mavivuli mnayoweka yana bore sana. Nitafurahi kupata maelezo ya kitaalamu ya kwanini picha zinakuja na margin nyeusi wakati mwingine juu na chini au kushoto na kulia na wakati mwingine pande zote za screen yaani juu, chini, kushoto na kulia,
 
Murano

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
2,063
2,000
Mkuu ni zoom hiyo,jaribu kutafuta option ya kukuza picha utaondoa tatizo lako.. nafkiri hizo picha zinaonyesha kwa format frame ya 4:3 Ratio kitu kama hicho..so badili iwe ratio ya 16:9 au something like that.. kama vipi tupia picha nione inaonyeshaje
 
Asante mkuu kwa elimu
 
sijui nini

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
2,552
2,000
kama ni dstv ishu itakuwa ni settings tu ya aspect ratio...ipo kwenye remote ukienda menu, advanced settings, afu tv installation kama skosei ytaona sehem ya aspect ratio(ofcozi inategemea na decoda na remote unayotumia inaweza ikawa ni tofauti na ya kwangu) ila mimi huwa mara nyingi inatokeaga na narekebisha kwa kufanya hivyo..
 
Mapengo 17

R I P
Mar 28, 2014
1,232
0
Mkuu ni zoom hiyo,jaribu kutafuta option ya kukuza picha utaondoa tatizo lako.. nafkiri hizo picha zinaonyesha kwa format frame ya 4:3 Ratio kitu kama hicho..so badili iwe ratio ya 16:9 au something like that.. kama vipi tupia picha nione inaonyeshaje

Mkuu Murano, hapo utakuwa umempoteza mwenzetu, hii iko katika mfumo wa HD (High diffinition) ndio maana inaonekana hivyo inatokana na baadhi ya setting zinazofanywa na mtu anaye hariri (Editor) either iwe kipindi, Makala au filams kuna Option anachangua ndio inatokea hivyo.

Pia kumbuka tumeingia kwenye mfumo wa Digitali kwa ukanda wa Afrika mara nyingi ndivyo inavyokuwa hi9vyo ila sio vipindi vyote ni baadhi tu ya vipindi.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu hata mimi natumia dstv hd kuna baadhi ya channel zipo kwenye mfumo ratio tofauti so ni uamuzi wako kufanya setting za ratio.. ukiachana na ratio ya kipindi kilichotengenezwa na editors.. hata ukiwapigia dstv watakupa maelekezo muruaa
 
Last edited by a moderator:

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
6,534
2,000
Jambo moja la kitaalam ni hili hapa wadau, photographer wengi pamoja na tv station zao bado wana mfumo wa ratio 4:3, hivyo basi pamoja na kujua wapo kwenye mfumo wa digital wao bado wanawaza kurecord kwa ratio hiyo wakijua watazamaji wote screen za ratio 4:3, so kama unajaribu kuzoom na tatizo haliishi daily elewa ni mfumo ulioanzia kwa cameraman kupitia kwa program editor mpaka kwa mrusha matangazo pia ana shida hiyo hiyo.
Kwa wenye tv za standard ratio 4:3 hawaoni tatizo hilo, ila kwa wenye 16:9 ratio ili linaonekana wazi.
mfano;
Ukiwa na camera yako yoyote na imeandikwa full HD hiyo muda wowote inarecord mfumo wa 16:9, but kama haijaandikwa inabidi ufanye settings kuweka hiyo 16:9 ili kupunguza hadha kwa watuaji walio nyumbani kama jamaa yetu hapa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom