ITV: Tarehe 20/4/2018 ilikuwa Kipimajoto au Kipindi Maalumu ?

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Ni kwa sababu mlikirusha hewani kwa namna ya kipekee tofauti na kawaida yake.

Kwa kweli (unless m - prove otherwise) kwa hiko siku hiyo hakikuwa kipindi cha "Kipimajoto" cha kawaida kama ilivyozoeleka na badala yake kile kilikuwa "Kipindi Maalumu" cha ufafanuzi wa ripoti ya CAG iliyoibua upotevu wa Tshs. 1.5T toka kwa kada wa CCM!!

Najiuliza kama ilikuwa kipindi maalumu ni kwa nini ITV hamkutuarifu watazamaji na wasikilizaji wenu mapema na badala yake mkatuhadaa ?

Well. Inawezekana kabisa kuna mtu/watu wengine kuni - challenge kwamba, iweje iwe kipindi maalumu cha ufafanuzi wa ripoti ya CAG wakati hakukuwa na mtu yeyote wa serikali kwa ajili hiyo?

Ni kweli hakuwepo mtu yeyote wa serikali na hususani ofisi ya CAG na kwa hiyo siyo sahihi kusema hivi na kwa mantiki hii waliokuwa manajadili hayo ni watu huru na kwa hiyo, kilikuwa kipindi kama vipindi vingine!!

Hii siyo kweli hata kidogo. Na msiwafanye watazamaji wenu wajinga na hawana utambuzi wa mambo.

Kuna kila dalili kuwa kipindi cha siku hiyo kilitekwa (hacked) na serikali (na nyie wenye TV Station na Radio zenu kwa maana ya Capital Radio na Radio One kuufyata) kwa kukubali kupachikiwa watu wenye mrengo wa kutetea serikali tu.

Hilo ni wazi lilikuwa kosa kubwa la kitaaluma na ni bora mkaomba radhi watazamaji na wasikilizaji wenu iwapo nyie ni waungwana!!

Hili linathibitishwa na haya:

1. Hamkuweka wala kuruhusu simu kupitia namba yenu maarufu (0767 444 701) kwa ajili ya watazamaji na wasikilizaji kuuliza maswali ama kuchangia hoja/mada iliyokuwa mezani kujadiliwa. Hii mimi na wenzangu tuliokuwa tunafuatilia kipindi tuliona kituko na ajabu!!

2. Kulikuwa na mgeni mmoja tu studio (David Kafulila) ambaye ni mwana CCM na kwa lugha rahisi kabisa ni "msemaji asiye rasmi" wa serikali.

Kila mtu aliyefuatilia mjadala huo aliweza kujiridhisha pasipo shaka kabisa kuwa, David Kafulila alikuwa pale kwa kusudi la kuitetea/semea serikali na kuponda wote wanaoichambua ripoti ya CAG kwa kuibua madudu na hususani upotevu wa 1.5T ambao CAG alishindwa na kwa kweli mpaka sasa ameshindwa kuelewa zilipo!!

Ilishangaza kidogo kwani kwa waandaji makini wasio "biased" hasa kwenye hoja ya ripoti ya CAG na kinachoonekana "wizi" ama "ufisadi" wa Tshs. 1.5T kama ulivyoibuliwa na CAG na hata nyie kuuandalia mada ya mjadala katika TV na Radio zenu, ilitegemewa tuone mchanganyiko wa wachokoza/wchangia mada.

Sio dhambi hata kidogo kuwepo Kafulila, lakini binafsi nilitegemea nione na watu kama Zito Kabwe mwenyewe, mtu kutoka ofisi ya CAG, mtaalamu huru wa mambo ya ukaguzi wa mahesabu na uhasibu nk

Lakini kutuletea mtu mmoja mwenye mawazo ya upande mmoja ulikuwa ni mzaha na kuidharau audience yenu. Mngeweza kuwapa jukwaa jingine kueleza mambo yao lakini si kama vile mlivyofanya, kukiuka protokali ya kipindi chenu ambacho kwa kweli kimejijengea umaarufu sana!!

3. Japokuwa kwa upande wa Dodama, kulikuwa na wabunge wawili, Dr Raphael Chegeni (Busega) na Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC na Bi. Naghejwa Kaboyoka (Same Mashariki) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PAC, bado ilikuwa haitoshi kwa sababu hawa ni walewale. Hawakuwa na tofauti na yule aliyekuwa Studio Mikocheni.

Kwa kiasi kidogo sana hawa waheshimiwa wawili kule Dodoma kwa mtazamo wangu, walikuwa na mitazamo iliyokuwa kidogo inaficha hisia zao za "ukada" kuhusu ripoti ya CAG ya mwaka wa fedha 2016/2018 ulioisha Juni 30, 2017.

Kidogo kwa upande wa Raphael Chegeni kwani alijaribu na kujitahidi kwa kila mbinu kuwa "neutral" lakini kiukweli akishindwa kabisa kuitetea kwa hoja serikali hususani kwenye "zimwi" la "ziliko" 1.5T!

Hongera (kwa nionavyo mimi) kwa Mama Naghejwa kwani yeye alioneokana kusimama kwenye kanuni ya "mtazamo huru" itawalayo majadiliano yoyote yale. Nahisi huyu mama siyo mwana CCM.

KWA HIYO, kwa maelezo haya naweza kuhitimisha hoja yangu pasipo shaka kuwa hamkupaswa kukiita kipindi hicho siku hiyo kuwa "KIPIMAJOTO" kama ilivyo kawaida yake kila wiki na badala yake mngekiita "KIPINDI MAALUMU CHA SERIKALI KUPITIA KWA DAVID KAFULILA KUFAFANUA RIPOTI YA CAG" .

Nadhani mngeeleweka kwa watazamaji na wasikilizaji wenu na sisi wengine pengine tusingepoteza muda kufuatilia propaganda hizo.

USHAURI KWA VYOMBO VYA HABARI VYA IPP MEDIA HOUSES:

Kwamba, ninyi ni vyombo huru vya habari na kwa kutumia ubunifu wenu mnafanya biashara yenu kukubalika na mna exist ktk soko la ushindani...

Audience (umma) ndiyo soko lenu. Naamini hampati ruzuku yoyote ya uendeshaji wa media houses zenu. Kumbukeni wanasiasa wanakuja na kupita. Mkikubali kuendeshwa na kutumiwa na wanasiasa ambao wanaibukaga na kupita tu kama upepo, mtakuwa mnaua urithi wa ubunifu kwa watoto wa watoto wenu!!.

Jifunzeni kwa Sahara Communication wamiliki wa kituo cha luninga cha StarTV na kituo cha Radio cha Radio Free Africa (RFA) jinsi wanavyo struggle kurudi sokoni baada ya kuchanganya taaluma na siasa kwa ushawishi wa wanasiasa... Umma hauwaamini na usipoaminiwa na audience ktk tasnia hii, bora kujishughulisha na kazi nyingine!!

Mtapoteza credibility kama mambo yenu yataanza kupakwa shombo ya siasa na siasa. Kuja kuinuka na kurudi mlipokuwa, ni kwa gharama kubwa....

Msidhani kuwa audience ambayo ndiyo soko lenu la bidhaa zenu haioni kuwa mnakengeuka. Tuna akili sana, tunaona sana na itafika wakati mtapuuzwa kabisa!!
 
Pole sana kuwa hadi leo bado unaangalia itvccm, bashite ashafanya yake hapo hutokaa ukapata kitu cha maana.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kwakweli walichemsha!

Vibaya na wasipojirekebisha watawafuata Sahara Media Communication wamiliki wa kituo cha luninga cha StarTV na Radio (RFA) waliko.

Wana struggle kwelikweli kuinuka na kusimama tena kama walivyokuwa hapo awali kama hawajakubali kutumiwa na wanasiasa wajao na kupita!!
 
Back
Top Bottom