ITV Tanzania:Kibanda awaambia Polisi waseme ukweli

KennedyMmari

JF-Expert Member
Dec 12, 2012
979
183
Mwenyektii wa jukwaa la wahariri Absalom Kibanda amerejea nchini baada ya matibabu ya muda mrefu nchini Afrikakusini huku akiomba polisi kueleza ukweli wa yaliyotokea na kuchukua hatua kwa yeyote aliyehusika kwenye unyama aliotendewa.

Source:ITV Tanzania Facebook Page
.
Swali:Kuna ukweli Gani Polisi wameuficha kuhusu kutekwa na kuteswa kwa Kibanda??




Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri na mhariri mtendaji wa new habari absalom kibanda amerejea leo nchini na kulakiwa na watanzania wapenda amani na maendeleo. Wanachi wengi sana walijitokeza huku wengine wakitokwa na machozi ya huruma huku wakiwa hawaamini kumuona tena kibanda akiwa na siha njema namna ile.

Kibanda amewashukuru watanzania kwa dua zao wakati wote tangu apatwe na masibu yale na ameahidi kuelezea mkasa mzima jinsi ulivyokuwa na kutoa leads ya ni nani hasa wahusika wa utesaji dhidi yake...

pole sana kibanda na karibu nyumbani...mungu azidi kukujaala afya njema uendelee kulijenga taifa lako...damu yako haijamwagika bure.
 
skendo kama ile ni ngumu sana kuitengasha na serikali ya mr. dhaifu. ingekuwa ni chama pinzani au mtu binafsi ndiyo kafanya vilee asingemaliza hata wiki angekuwa tayari kova mzee wa mikengeza a.k.a mzee wa kutokelezea kwa kioo angekuwa kashaitisha press conference... hapo jk na serikali yake wanahusika.
 
nimemsikia anasema hawezi kukaa kimya kama dr ulimboka lazima atasema tu na watesaji watajulikana tu.
 
Atasema tu maana mwenzake Uli amekula kitu cha kuziba mdomo yeye hawezi kukubali maana amepata ulemavu!inasikitishaa sana!jipange na kulipua bomu!hata ikibidi akiwa uhamishoni ubalozi usa au uk akaombe hifadhi!maana wale wanajua kila kitu hata waliohusika wanawajua!wanajua fitna zaidi ya tiss wetu !wanajua ukweli woote
 
Hata mwakyembe nae alisema hv hv ila hadi leo kmy!kwn had polic waseme !!?we kama unajua kilichokutokea c useme tujue,au km hutak piga kmy mana uckute unamaskendo yko na watu huko ukafumuliwa!!
 
nilimsikia anasema kwanini ktk hii miaka nane ambayo jk amekaa madarakani kumekuwa na matukio mengi ya ukatili kwa waandishi wa habari? anasema hawezi kusubiri asemewe kama wengine hivyo atalipua bomu soon. sisi yetu macho na masikio
 
Natumaini naye atatafutiwa fungu la kutosha ili atulie, nchi hii inaweza kukufanyia unyama na kukutajirisha at the same time. Hiyo bahati wengine haituangukii. Tusubiri hayo mabomu hata ikiwa kwa karne nyingi, tutaendelea kusubiri mpaka tuwajue watesaji.
 
Labda hataki hilo jicho lililobaki.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Una maana wale watoa kucha na meno bila ganzi watamrudia tena,ili waje wamnyofoe hilo jicho la pili lililobaki?!

Na pamoja na mzee wa movie ya kichaa wa Kenya,kuwa hadi leo,baada ya miezi mitatu hajamkamata hata mtuhumiwa mmoja,wa tukio la kutekwa kwa Kibanda,bado hata hivyo,JK,amemtunukia utumishi uliotukuka na amempandisha na cheo!!
 
Wanaosema ukweli hawasubiri kusemewa

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hata mwakyembe nae alisema hv hv ila hadi leo kmy!kwn had polic waseme !!?we kama unajua kilichokutokea c useme tujue,au km hutak piga kmy mana uckute unamaskendo yko na watu huko ukafumuliwa!!

Dr. Mwakyembe alishaweka bayana kwenye maelezo yake ya kurasa 8 kwenda polisi. Alitaja magaidi waliotoka (Somalia) yamkini, Al-Shababu waliopangwa wamuuwe. Muda wote wakiwa hapa nchini walitumia magari ya kampuni ya ujenzi ya Caspian Construction (ni kampuni ya Rostam Aziz,) yamkini hata Bashe anayafahamu magari yaliyohusika. Piia magari ya TISS yalitumika kuwabeba wale magaidi kutoka Somalia.

Maelezo ya Dr. Mwakyembe yaliishia ofisini kwa DCI Manumba hadi kesho.
 
Awabane wampe Dau la kutosha washitaki baada ya makabidhiano.Nani kakuambia walioshindwa kuua wakulipe na usahau,halafu waendelee na hayo mauaji.Bora wangeacha.

Ila Mungu wa Israel ni Soo..hawa wana wa jehanum,wamemwaga damu za watu...sana.Hadi sasa wanajikuta wakishindwa wamalizia watu.
 
skendo kama ile ni ngumu sana kuitengasha na serikali ya mr. dhaifu. ingekuwa ni chama pinzani au mtu binafsi ndiyo kafanya vilee asingemaliza hata wiki angekuwa tayari kova mzee wa mikengeza a.k.a mzee wa kutokelezea kwa kioo angekuwa kashaitisha press conference... hapo jk na serikali yake wanahusika.

Peleka ushahidi polisi kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa jinai [the criminal procedure act]... sio unapayuka tu. una uhakika JK anahusika??? are you sure? Leta ushahidi wako hapa jamvini au peleka polisi hq.
 
Kibanda amshukuru tu Mungu kwa viungo aliyobakiwa nayo, japo kafanywa kilema.
Kwa serikali yetu sikivu, au dhaifu madai yake ni mazito mno.. sio rahisi kuyatekeleza.
Labda basi waseme tu ni Chadema imefanya, hilo rahisi, na kumtafutia tuhumu Mchadema yeyote. Vinginevyo Mungu aendelee kukulinda Kibanda, japo umefanywa kilema. Ipo siku, nayo yaja ambapo yote yaliyo sirini yatafichuliwa. Endelea kumshukuru Muumba wako. Pole lakini.
 
Karibu nyumbani mwenyekiti.... Tunasubiri maelezo yako kwa hamu kubwa kama polizia watashindwA kusema ukweli...
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom