Elections 2010 ITV Tangazeni matokeo ya Urais mnavyoyapata

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
ITV hamuwatendei wananchi haki kwa kuzuia matokeo ya Urais ambayo yanatangazwa pamona na yale ya wabunge. Tangazeni matokeo hayo yanavyokuja kutoka majimboni. Kwanza ni kwa sababu mtawasaidia wananchi kujua nini kinaendelea na mtaondoa wasiwasi na vile vile mtasaidia kupunguza watu kufikiria Tume inachakachua.

Sasa kama nyinyi ndiyo vyombo vya habari na mnapata matokeo halali kutoka majimbo kwanini msiyatangaze huku mnayajumlisha tuone kama yanalingana na yale yanayotangazwa na tume?

You must be independent enough, mbona wenzenu Mwananchi wanafanya hivyo?

Kama Kikwete kashinda matokeo yenu na ya tume hayawezi kupishana! so do the needful.
 
Kweli ITV hawatutendei haki namsikiliza Masako live anavyo wakatiza kauli watoa habari wanapotaka kutoa matokeo ya urais hadi anaboa kabisa. Sielewi kwanini anawazuia wakati matokeo yameshatolewa vituoni, ila nasikia Chadema kama chama kinakusanya matokeo yote ya vituoni ndipo kitoe tamko kwa hiyo kama NEC watatangaza tofauti watakuwa wanajitafutia matatizo makubwa nawaomba wasije wakathubutu kufanya hivyo.
 
ahsante sana mzee mwanakijiji kunbe umeliona hilo. jana nilikuwa naangalia star tv toka asubuhi walikuwa wanatangaza kwamba lema kashinda arusha lkn itv wao wanasema eti mchuano bd mkali sijui wanaogopa nini? sasa wanatangaza nini km hawatoi matokeo mapema? waache kutangaza basi
 
wamezuiliwa kufanya hivyo na CCM ili waendelee kuchakachua ITV wanashiriki uchakachuaji kwa njia hiyo
 
UWT umeaagiza reporter wake wasitangaze matokeo ya URAIS

SHAME ON YOU ITV :rip::rip::rip::rip:ITV
 
ITV MWAKA HUU AMMEWAFANYIA WATANZANIA KITU KIBAYA SANA,TULIKUWA TUNA WAAMINI SANA LAKINI IMANI YETU IMESHAPOTEA SIJUI MENGI WAMEMWOGOPESHA NA NINI! Habari zote mtakazo kuwa mnatangaza baada ya uchaguzi sitoziamini tena.MLIMANI tv na SAUTI YA UJELUMANI Ndizo sosi zangu.
 
Nimekuwa nafuatilia Matokeo ya Uchaguzi kupitia TV na Radio lakini kinachonishangaza ni Kwamba Katika majimbo ambayo CCM inashinda Matokeo ya Urais Yanawekwa wazi ila Kule ambako Upinzani Unashinda wanatangaza tu Ubunge Lakini Matokeo ya Urais hayatangazwi

Naomba Matokeo ya Urais

Mbeya Mjini
Iringa Mjingi
Moshi Mjini
Mwanza
Musoma Mjini
Kigoma

Mnaweza kuendelea

Huko tumetangaziwa Ubunge tu ila Urais hawajatangaza,

Je ni Strategy ya NEC Kuchakachua
 
Back
Top Bottom