ITV: Rudieni tangazo hili mara kwa mara! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ITV: Rudieni tangazo hili mara kwa mara!

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Tikerra, Oct 12, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ITV wanarusha tangazo moja matata sana,kwakweli limeni-impress sana.Ni tangazo ambalo ni extract kutoka kwenye hotuba mbalimbali za baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere.Katika extract hiyo, mwalimu anamshanga jamaa aliyefurahi kupata kipande cha chupa kwa kudanganywa kwamba ndiyo alimasi,na tapeli akachukua alimasi halisi.Katika hali isiyokuwa ya kawaida, yule jamaa aliyechukua kipande cha chupa, ambae mwalimu alimwita zuzu,aliendelea kushangilia kana kwamba ndiye kapata alimasi.Nalipenda tangazo hili kwa vile linaeleza hali halisi tunayopitia hivi sasa. ITV naomba mlitangaze tangazo hili mara kwa mara, labda litasaidia kwa kiasi fulani.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Jana usiku nimeangalia hotuba ya marehemu mwl Nyerere kituo cha ITV na nimeshangaa sana kama huyu mtu hakuwa nabii wa kisiasa wa nchi hii.
  Hotuba hii aliitoa wakati wa mchakato wa kutafuta rais wa awamu ya tatu.
  Ni ajabu kwamba mengi kati ya aliyoyazungumzia yameonekana kuanzia kwa aliyempigia kampeni hadi sasa tunayaona yale yale.
  Sijui kabisa kama hawa viongozi wetu wa leo wanayaangalia haya.
  Naomba nipewe kopi ya hotuba hiyo kama inaweza kupatikana hapa jf au ikiwezekana ichezwe na ITV kila siku mara moja.
  Ilikuwa ina predict nini hakitakiwi katika nchi hii na kikifanyika nini matokeo yake.
  Nayaona sasa katika kanchi ketu haka.
   
 3. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mchukia fisadi, Hata mimi kuna hotuba moja ambayo Mwl. Nyerere aliitoa Mbeya wakati wa sherehe za Mei Mosi nadhani ilikuwa 1992 au 93 nayo ina maneno makali yenye ujumbe ambao hawa viongozi wetu waliopo madarakani sas hivi kama watakuwa wanaisikiliza nina imani watajiona wazi kuwa wanacheza na madaraka na si kufanya kazi..

  Kwa kweli Mwl. kilikuwa kichwa ambacho sijaona mfano wake mpaka muda huu hapa Tanzania.
   
 4. K

  Kunda Member

  #4
  Oct 13, 2008
  Joined: Jun 10, 2008
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba kufahamishwa jinsi ya kupata copy za hotuba ya Mwl. Nyerere.
   
 5. M

  Mundu JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2008
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Nimeisikiliza ile hotuba kwenye ITV, jamaa anaongea kwa utani hivi lakini anagusa kwenye pointi kabisa. Ameongelea mpasuko wa muungano ambao hadi leo haujapatiwa majibu. Ameeleza matatizo ya viongozi kutokuheshimu katiba, hadi leo yanasumbua. Amezungumzia kuzingatia utawala wa sheria.... Hili limenigusa sana... kwahili wale wote waliohusika na wizi wa fedha za EPA sasa hivi wangekuwa ndani na viboko kumi na viwili... na wakitoka wanalamba viboko kumi na viwili wakaonyeshe familia zao. Suala la kuwaacha wezi na walarushwa halikuwa na simile kabisa na halitakiwi kuzungumzwa kwenye vikao vya bao... ni wahusika kuadabishwa kwa mujibu wa sheria.

  Sidhani kama Rais wetu huyu tuliyenaye anayo ile hotuba ya mwalimu... kwani kinachofanyika sasa utafikiri mwalimu alimsema yeye!!! Go spend your quality time to understand those words of wisdom bro!
   
 6. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wote walionitangulia hapo juu kwa asilimia 100, kweli Marehemu Baba wa Taifa alikuwa kiongozi na alizaliwa kuongoza. Achana na hawa wa sasa ambao mara nyingi uongozi wao naulinganisha na ze comedy.

  Kitu kingine ambacho napenda kukiongelea hapa ni kwamba, kesho ni siku ya kumbukumbu ya miaka 9 ya kifo cha kipenzi cha wengi Marehemu baba wa Taifa, napenda kutoa wito kwa vyombo vya habari hasa Televisins kwamba tungependa kuona mnawahoji wananchi wa kawaida ni jinsi gani wanamkumbuka Baba wa taifa, na wala siyo kuwahoji MAFISADI.

  Nitashangaa sana kuona mnamuhoji CHENGE au LOWASA ni jinsi gani anavyomkumbuka Mwalimu. Na bila shaka hawa MAFISADI wataongea kwa uchungu wa KINAFIKI kuhusu jinsi walivyompenda sana Mwl. na jinsi wanavyojisikia vibaya kutokuwa naye leo hii. UNAFIKI MKUBWA SANA.
   
Loading...