ITV rekebisheni maswali ya kipima joto

Bonson

Senior Member
Apr 20, 2013
183
147
Kwanza nianze kwa kukipongeza kituo cha ITV kwa kazi nzuri mnayofanya kuhabarisha umma wa Tanzania kwa umahiri mkubwa. Pamoja na pongezi hizo; naomba mfanye marekebisho katika kipindi chenu cha KIPIMA JOTO. Sijui ni nani anaeandaa maswali yenu; kwa kweli ni maswali ambayo hayaeleweki na mengine yanakuwa na majibu ya moja kwa moja (rhetorical questions). Endapo mnataka kweli kupima hali ya mambo katika jamii, basi ulizeni maswali ya kufikirisha.

Nitolee mfano swali lililoulizwa jana (Dec 26/2016): "JE WANAOJENGA GEREJI BUBU MITAANI WAKO JUU YA SHERIA?" This is crazy!! Tayari wote tunajua hakuna aliye juu ya sheria!!

Nawatakia Mwaka Mpya wa Baraka na Pia mje na maswali ya maana 2017.
 
Hata mimi huwa nashangaa, maswali ambayo majibu yake yako moja kwa moja, kwa ufupi wanauliza majibu. Pia wanapotoa takwimu waseme asilimia fulani ya idadi fulani ya watu. Kusema tu asilimia peke yake haitoshi kuonesha takwimu.
 
Hili swala hata mie nilisgawahi kulisemea ila naona bado ubadilikaji wao ni kama mwendo wa kobe.., Leading Questions hazifai katika kufanya utafiti wa jambo katika jamii.
 
kweli maswali yao yana bias,lakin bias hyo inalenga kuikosoa serikali au watu wanaofanya makosa,me naona wanafanya kazi ya u-watchdog vizuri tu.
 
Lakini wajifunze pia kufahamu ipi inapaswa kuwa lead story leo kundi kubwa la wananchi wamechoma mashine kadhaa za kuvuta maji na wameandamana na marungu na mapanga kwenda kufanya jinai hiyo iliyobarikiwa na viongozi wa serikali za mitaa matokeo yake imekuwa stori ya nne sijui tano huko waka lead na hadithi hadithi tu STEVEN CHUWA badilika tambua story inayofaa kubeba habari yako...halafu mapicha kujirudiarudia pia mnakera mfano story ya morogoro hilo cut away la basi lilioandikwa master j utadhani promo kha! audiovisual editor mvivu au waandishi wavivu kuwaletea picha za kutosha tv ni picha,mazuri hatusifii tupo hapa kukosoa tu
 
Eti "Je kutupa takataka hovyo kunasababisha kuenea kwa magonjwa mfano kipindupindu na kuhara?" Afu utakuta 30% eti wamejibu hapana. Nahisi takwimu wanazotoa ni za kupikwa kama wale nanihii waliosema 96% ya watanzania wanampenda bwana yule.
 
Ingekua vzur km wangekua wanauluza maswali yanayoibua majibu ya kero fulani miongoni mwa watazamaji wao. Kwa mfano "NINI KIFANYIKE KUZUIA UJENZI WA GEREJI BUBU MTAANI" hapo wangekua wanakusanya maoni mengi sana kuliko maswal ya muongozo.
 
Kwanza nianze kwa kukipongeza kituo cha ITV kwa kazi nzuri mnayofanya kuhabarisha umma wa Tanzania kwa umahiri mkubwa. Pamoja na pongezi hizo; naomba mfanye marekebisho katika kipindi chenu cha KIPIMA JOTO. Sijui ni nani anaeandaa maswali yenu; kwa kweli ni maswali ambayo hayaeleweki na mengine yanakuwa na majibu ya moja kwa moja (rhetorical questions). Endapo mnataka kweli kupima hali ya mambo katika jamii, basi ulizeni maswali ya kufikirisha.

Nitolee mfano swali lililoulizwa jana (Dec 26/2016): "JE WANAOJENGA GEREJI BUBU MITAANI WAKO JUU YA SHERIA?" This is crazy!! Tayari wote tunajua hakuna aliye juu ya sheria!!

Nawatakia Mwaka Mpya wa Baraka na Pia mje na maswali ya maana 2017.

Naomba nikupe tu ushauri ndugu yangu. Kama kweli ni mpenzi wa habari zilizochambuliwa kwa kina fanya kuangalia kupitia Azam Tv 2, otherwise km hautumii decorder yao. jamaa wana habari nzur na zilizochambuliwa vzr. Kuna watu wenye weledi mkubwa wa habari kama Charlea Hilal, Raymond Nyamuhula, Rose Mlutu, Ivonna Kamuntu, Fatma Almasi Nyangasa na wengine wengi. Iam sure ukiangalia siku moja hautaacha kuwafatilia hawa jamaa.
Lakin kama watumia digitech, au ting pole endelea kula vipima joto
 
Eti "Je kutupa takataka hovyo kunasababisha kuenea kwa magonjwa mfano kipindupindu na kuhara?" Afu utakuta 30% eti wamejibu hapana. Nahisi takwimu wanazotoa ni za kupikwa kama wale nanihii waliosema 96% ya watanzania wanampenda bwana yule.
Mara nyingi wanauliza majibu sio maswali....!! Sijajua huwa wana maana gani au wanalenga nini?
 
Naomba nikupe tu ushauri ndugu yangu. Kama kweli ni mpenzi wa habari zilizochambuliwa kwa kina fanya kuangalia kupitia Azam Tv 2, otherwise km hautumii decorder yao. jamaa wana habari nzur na zilizochambuliwa vzr. Kuna watu wenye weledi mkubwa wa habari kama Charlea Hilal, Raymond Nyamuhula, Rose Mlutu, Ivonna Kamuntu, Fatma Almasi Nyangasa na wengine wengi. Iam sure ukiangalia siku moja hautaacha kuwafatilia hawa jamaa.
Lakin kama watumia digitech, au ting pole endelea kula vipima joto
Duuuh; asante kwa ushauri. ITV imefanya kazi nzuri sana kwa miaka mingi; inabidi tuwakosoe wabadilike wasijeelekea mwelekeo wa TBC... hahahahha!!
 
Mie kero yangu kubwa kwao ni habari za kimataifa......yaani ni vipande vya seconds 4 au 5 utadhani umeme umekatika, kwa hapa sio vibaya mkiwaia star tv.
 
Hii chanell kuwa na swali la kipima joto ni zuri kijamii, kama kweli wana nia ya kubadilika kwa kuzingatia mawazo haya walete kipima joto chenye kwenda shule, vinginevyo sioni faida ya kushiriki kujibu maswali yao maana yanakuwa yamejijibu tayari
 
Swali letu la kipimajoto ''Je mazingira machafu ndo sababu ya kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu Dar es Salaam?''
Andika N kama jibu lako ni ndiyo, H kama jibu lako ni hapana na S kama jibu lako ni sijui.
 
Back
Top Bottom