Gerad2008
JF-Expert Member
- Jun 9, 2009
- 583
- 287
Tangu ilipoanzishwa radio one miaka ya 1994 na baadaye ITV nilikuwa napenda sana kusikiliza habari zao kwa sababu iliingia hewani wakati wengi wetu tukiwa tunajua idhaa moja ya RTD. Ilipoanza ilikuwa na mambo mengi ya maana sana na news zake zilikuwa very enlightening.
Siku za hivi karibuni ITV na radio one vimekuwa vituo vya very boring na kwa sababu habari zao nyingi ni za kujirudia rudia. Kwa mfano ukiangalia au kusikiliza taarifa ya habari ya jioni saa mbili habari hiyo hiyo ndiyo itakayo kuwa kwenye kipindi cha NIPASHE cha saa 12:30 asubuhi na kwenye taarifa ya habari ya saa 1 asubuhi. Hali hii inakera na inafanya nione kama ninakula kiporo cha habari za jana ambazo zimeshapita. Hivi ni kwamba wameshindwa kutafuta habari kama zamani au ndo historia ya ITV/radio one inakaribia kufutika. Hata habari ambazo ITV inazitoa siku hizi si habari ambazo zinastahili kutolewa na kituo kikubwa kama ITV kwani inaonekana kabisa kwamba au hawana bajeti ya kutafuta habari au hawana competent team ya kutafuta habari. Siku hizi ni kama umeshaangalia ITV jioni hakuna sababu ya kusikiliza Nipashe asubuhi.
Kitu kingine ambacho kina ua kabisa hivi vituo ni ile tabia ya kutaka kuifurahisha serikali kwa kutoa habari ambazo zitaifurahisha serikali zaidi. Ni kama ITV inatumia muda mwingi kuisadia TBC kutangaza mambo ya chama tawala bila kujua wanajimaliza taratibu.
Siku za nyuma ilikuwa ngumu kuacha kuingalia taarifa habari ya ITV lakini imeshindikana kuendelea kuangalia taarifa zao kwani sio informative bali ujinga tu kwa mfano ufunguzi wa shule za chekechea, mashindano ya quran, rais kukabidhi zawadi ya mbuzi kwa watoto yatima, rais kutembelea Lindi na Mtwara, mama salma akutana na wake za mabalozi, kurudishwa kwa vyura wa kihansi, wazee wa Dar wafanya mashindano ya kukimbiza kuku n.k mnaweza kuongezea
Ninamshauri mmiliki wa hiki kituo au aboreshe safu ya watafuta habari aui kama kimemshinda basi akifunge kuliko kilivyo sasa kwani kinaendelea
kupoteza kabisa mvuto kwa wengi wetu. Ni lazima tuseme ukweli kwamba enzi za akina Nevile Meena,Jery Muro, Akyoo, Mnete, n.k taarifa habari ikianza tulikuwa tunakimbilia ilipo TV ili tupate news . Siku hizi imepoteza mvuto kabisa