ITV/RADIO One na Viporo vya Habari

Gerad2008

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
583
287
Tangu ilipoanzishwa radio one miaka ya 1994 na baadaye ITV nilikuwa napenda sana kusikiliza habari zao kwa sababu iliingia hewani wakati wengi wetu tukiwa tunajua idhaa moja ya RTD. Ilipoanza ilikuwa na mambo mengi ya maana sana na news zake zilikuwa very enlightening.

Siku za hivi karibuni ITV na radio one vimekuwa vituo vya very boring na kwa sababu habari zao nyingi ni za kujirudia rudia. Kwa mfano ukiangalia au kusikiliza taarifa ya habari ya jioni saa mbili habari hiyo hiyo ndiyo itakayo kuwa kwenye kipindi cha NIPASHE cha saa 12:30 asubuhi na kwenye taarifa ya habari ya saa 1 asubuhi. Hali hii inakera na inafanya nione kama ninakula kiporo cha habari za jana ambazo zimeshapita. Hivi ni kwamba wameshindwa kutafuta habari kama zamani au ndo historia ya ITV/radio one inakaribia kufutika. Hata habari ambazo ITV inazitoa siku hizi si habari ambazo zinastahili kutolewa na kituo kikubwa kama ITV kwani inaonekana kabisa kwamba au hawana bajeti ya kutafuta habari au hawana competent team ya kutafuta habari. Siku hizi ni kama umeshaangalia ITV jioni hakuna sababu ya kusikiliza Nipashe asubuhi.
Kitu kingine ambacho kina ua kabisa hivi vituo ni ile tabia ya kutaka kuifurahisha serikali kwa kutoa habari ambazo zitaifurahisha serikali zaidi. Ni kama ITV inatumia muda mwingi kuisadia TBC kutangaza mambo ya chama tawala bila kujua wanajimaliza taratibu.
Siku za nyuma ilikuwa ngumu kuacha kuingalia taarifa habari ya ITV lakini imeshindikana kuendelea kuangalia taarifa zao kwani sio informative bali ujinga tu kwa mfano ufunguzi wa shule za chekechea, mashindano ya quran, rais kukabidhi zawadi ya mbuzi kwa watoto yatima, rais kutembelea Lindi na Mtwara, mama salma akutana na wake za mabalozi, kurudishwa kwa vyura wa kihansi, wazee wa Dar wafanya mashindano ya kukimbiza kuku n.k mnaweza kuongezea

Ninamshauri mmiliki wa hiki kituo au aboreshe safu ya watafuta habari aui kama kimemshinda basi akifunge kuliko kilivyo sasa kwani kinaendelea
kupoteza kabisa mvuto kwa wengi wetu. Ni lazima tuseme ukweli kwamba enzi za akina Nevile Meena,Jery Muro, Akyoo, Mnete, n.k taarifa habari ikianza tulikuwa tunakimbilia ilipo TV ili tupate news . Siku hizi imepoteza mvuto kabisa
 
taizo ni mhariri, steven chuwa na wengine.. wajeuri sana..nimecheka sana hiyo rais na mbuzi wa idi.. nahisi hawasomi alama za nyakati..contents zao ni vimeo muda mwingune hurudia rudi habari kama FILAMU
 
nina wasiwasi kama mfumo wa digital unavyoanza local stations zetu zitabaki bila kazi. Mfano sasa hivi kila mwenye decoder anatune local stations wakati wa habari tu saa mbili labda! Napo ndio NTV, Citizen na zingine za Africa Mashariki hazijafunua matangazo yao bado
taizo ni mhariri, steven chuwa na wengine.. wajeuri sana..nimecheka sana hiyo rais na mbuzi wa idi.. nahisi hawasomi alama za nyakati..contents zao ni vimeo muda mwingune hurudia rudi habari kama FILAMU
 
nina wasiwasi kama mfumo wa digital unavyoanza local stations zetu zitabaki bila kazi. Mfano sasa hivi kila mwenye decoder anatune local stations wakati wa habari tu saa mbili labda! Napo ndio NTV, Citizen na zingine za Africa Mashariki hazijafunua matangazo yao bado

We subiri kifo kinawanyemelea kwani ilivyo sasa wanaelekea mortuary
 
Radio one ndio kabisa wanatangaza kwa imla kama RTD enzi hizo.wanavipindi vilivyotungwa na enzi za akina charles hillary,John Dilinga,Abdalah Majura! Majina ya vipindi yale yale maudhui yale yale! At least vipindi vya michezo!
 
hata CHANNEL TEN,TBC,STAR TV ni hivyo hivyo
Wahariri wengi hawajali wajibu wao.Labda kunufaika na mijadala ya asubuhi.
 
No comments, ni bora kuangalia muziki c2c kuliko kuangalia ITV coz hamna cha maana utakacho pata
 
ukiwa na decoder channel za bongo unazisahau kabisa,wanasingizia vifaa lakini wapi,ndo maana radio zote saa 3 asubuhi wameweka vipind kama vya akina dina wa clouds! Hatuna vichwa kabisa redioni na tv!
 
Kiukweli it is no longer a choice of people na unaweza tu kuwaangalia na kuwasikiliza hawa jamaa pale tu unpokosa kingine cha kuangalia. kama hicho kipindi cha NIPASHE cha saa 12:30 asubuhi ni upuuzi mtupu siku nimesikiliza kwa bahati mbaya nilibaki kusonya tu. Njoo kwenye taarifa za habari kwa mfano saa saba mchana hakuna issu kabisa. Ndani ya ushindani huu wa sasa nayo itapotezewa tu kama RTD.
 
watangazaji wa radio one/ITV wanatangaza tu kupata ugali wao lakini hakuna incentive ya maana kwa mbunifu,mfano clouds pamoja na kutukera mara nying lakini watangazaji wanafaidika na ubunifu wao thru matangazo.
 
Sikilizeni mejik, hasa kile kipindi cha orest kawau na mashaka nzowa. Mtu mzima kibwana dachi huwa anafunga kazi. Unaingia supa mix. Kati hapo kwa watoto. Unakuja mejik sundown, na siku inakuwa imeisha
 
Back
Top Bottom