VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
TBC1 ni kituo cha luninga cha serikali. ITV ni kituo binafsi. Sifa kubwa ya vituo vya luninga vya serikali ni kutangaza habari za upande mmoja. Upande wa serikali tu ambao hujumuisha upande wa chama tawala. Ndivyo wafanyavyo TBC1. ITV walitegemewa kuwa tofauti.
Leo ITV wameripoti kuhusu mambo ya hapa Zanzibar. Wameongea na Kamishna wa Polisi hapa na kuonesha ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani,Charles Kitwanga. Wote hao ni wa serikali. Wananchi wa kawaida wameachwaje kando kuhusu hali ya hapa?
ITV inaamini na kuaminisha kuwa,kutokana na kauli za upande wa serikali,hali hapa ni shwari kuelekea uchaguzi wa Jumapili? ITV wanapaswa kujirekebisha. Wanapaswa kwenda hatua moja mbele. Kupata maoni au maelezo ya upande wa pili. Upande wa wananchi wa kawaida!
Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Zanzibar)