ITV na Ufinyu wa Habari

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
Habari za kazi wanajamvi,

Mimi ni mtazamaji mzuri wa ITV online kwa kuwa siko Tanzania. Jambo moja linalonikera sana ni kwamba taarifa zinazotolewa na ITV zimekuwa finyu zisizokuwa na uchambuzi au 'analysis' ya kutosha. Wanapoongelea jambo lolote hawalifanyii uchambuzi wa kina kama ambavyo unapaswa kufanywa na vyombo vingine vya habari. Muda uliopo wa Taarifa ya Habari ni mrefu wa kutosha kwamba wangeweza kuchambua yale wanayoyatangaza. Mifano halisi ipo kadhaa, mmojawapo ni wanapoonyesha kampeni za uchaguzi Igunga. Hatuhitaji tu kuona yaliyojiri kwa siku hiyo, bali ingekuwa vyema wakatumia dakika chache kuchambua yaliyojiri.

Mfano wa pili juzi walipozungumzia 'typhoon' iliyotokea Philippines. Kwanza wao wameita typhoon kwa kiswahili kuwa ni kimbunga, ambayo siyo sahihi. Tafsiri ya neno 'typhoon' ni tufani na siyo kimbunga. Kimbunga ni 'cyclone' na ni upepo mkali usioambatana na mvua. Kimbunga kinaweza kuezua nyumba lakini hakileti mafuriko!

Mfano wa tatu ni kuhusu kifo cha Prof. Wangari Maathai wa Kenya. ITV walitangaza tu kuwa Prof Maathai amefariki dunia baada ya kuugua kansa. Kwa mtu muhimu kama huyu, aliyekuwa mwanamke wa kwanza mwafrika kupokea tuzo ya Nobel, nilifikiri ITV wangetumia muda kiasi kutoa wasifu wake, hata kumwita mtu aliyemfahamu na kuongelea kwa kifupi kuhusu Prof. Maathai.

Hii yote ni dalili ya kuwa ITV inapokea tu taarifa na kuzitangaza (broadcast) bila utafiti wa kina. Na ikumbukwe kuwa ITV ilikuwa TV station ya kwanza (kama sikosei wakuu) kuanza kazi ya kurusha matangazo hapa Tanzania (Bara). Nilitumaini kuwa itakuwa na uzoefu zaidi wa kazi hiyo na kuifanya iwe bora zaidi kuliko hata TV zingine zilizofuata. Watazamaji tutaendelea kuangalia, lakini tungependa kuona wanajisahihisha, ili kuifanya ITV kuwa kweli chombo cha kutoa habari za uhakika na zenye uchambuzi wa kina. Nina imani ya kuwa uwezo wa kufanya hivyo wanao.
 
Mkuu ni ukweli kabisa hata mimi nilikuwa naangalia taarifa za itv, yaani ni kama muktasari wa habari, hazina mvuto hata kama habari ni ya muhimu,yaani utafikiri ni kama wanaharaka kuwahi kwenye sherehe, januari mwaka huu nilimsikia mama mhauville akiifananisha itv na cnn, duu maana nilikuwa nakunywa chai aliposema hivyo tu nilipaliwa, yaani ningemshauri hawatake radhi cnn, itv 80% ya vipindi vyake vya kucopy toka nje, uchambuzi wa habari sifuri, yaani to be honest naona kipindi kizuri itv ni kipimajoto ijumaa basi vingine haaa hata wasingeonesha poa tu.Siku hizi naangalia tv za kenya kama ktn na kbc jamaa wako fit kwenye habari na uchambuzi wao.Habari za bongo nasikiliza REDIO
 
Kwenye michezo, kama Simba imeshinda siku hiyo, basi mtegemee haitatangazwa, mtasikia tennis, basketball na michezo ya jadi kama bao. Labda awe mtangazaji mwingine, si Kitenge!
 
ITV wanahitaji kuajiri wana habari wenye uwezo na wawalipe vizuri. Mimi bado naitegemea sana ITV kwa taarifa ya habari, ingawa kama alivyodokeza aliyeanzisha thread hii, hawafanyi analysis ya kutosha. Waache 'coverage' ya warsha na makongamano waende kwenye matukio yanayowagusa wananchi moja kwa moja. Upande wa michezo pia wanahitaji ku-improve. Kwa mfano wanaporipoti kuwa Simba imeifunga Yanga, tuone move na magoli yaliyofungwa sio kuonesha clip ya mpira umetoka au unarushwa. Naamini Mhaville ana uwezo mkubwa wa kufanya changes kwa ajili ya ku-improve zaidi content ya ITV.
 
Itv na vituo vingine vya hapa ni kama unavoiskia voice of tabora au radio abood,,,,,,,,,huwez kupata jipya waache kuonesha tnathilia za akina jumong waichambue habari,,,,,,,
 
Mimi binafsi station za kibongo zinanikera. Nimetenga muda wangu nasubiria taarifa ya habari then wananiletea summary, inakera sana wandugu.
 
Tatizo kubwa la ITV ni cheap labour. Mmiliki wa hiki kituo ana uwezo mkubwa sana na anaweza kukifanya the best in East and central Africa kama akiamua kuacha ubahili. Kinachomponza ni malengo ya kuanzisha ITV Vs expectations za watazamaji. iInawezekana lengo lake ni kupata faida kupitia commercials na siyo kupoteza muda kutafuta habari na wachambuzi wenye elimu ya kutosha while expectations za watazamaji ni kuwa full informed na siyo kuonjeshwa habari. Mmiliki wa ITV atoke out of box ya ubahili aajiri wasomi wenye uwezo wa kuchambua mambo badala ya kuajiri cheap labour ili awalipe mshahara kidogo.
 
Mkuu ni ukweli kabisa hata mimi nilikuwa naangalia taarifa za itv, yaani ni kama muktasari wa habari, hazina mvuto hata kama habari ni ya muhimu,yaani utafikiri ni kama wanaharaka kuwahi kwenye sherehe, januari mwaka huu nilimsikia mama mhauville akiifananisha itv na cnn, duu maana nilikuwa nakunywa chai aliposema hivyo tu nilipaliwa, yaani ningemshauri hawatake radhi cnn, itv 80% ya vipindi vyake vya kucopy toka nje, uchambuzi wa habari sifuri, yaani to be honest naona kipindi kizuri itv ni kipimajoto ijumaa basi vingine haaa hata wasingeonesha poa tu.Siku hizi naangalia tv za kenya kama ktn na kbc jamaa wako fit kwenye habari na uchambuzi wao.Habari za bongo nasikiliza REDIO

Jaribu na Citizen naikubali sana mkuu nadhani inawafunika hao uliowataja especially kwenye habari saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki.
 
Back
Top Bottom