ITV na TBC kuhusu ugojwa wa ebola mkoani Kagera nani mkweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ITV na TBC kuhusu ugojwa wa ebola mkoani Kagera nani mkweli?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by R.B, Aug 5, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,168
  Likes Received: 1,103
  Trophy Points: 280
  Nimesikilza tarifa ya habari kuhusu ,mgojwa anayedhaniwa ana ugojwa wa EBOLA;

  TBC wamemuoji msaidizi wa mganga mkuu yeye kakanusha.

  ITV wamemuoji mganga wa KARAGWE mgojwa alipo hospitali ,anakili ni kweli ana dalili zote;


  Naomba serikali itegue kitendawili hiki mkoa kagera. kuna magojwa mengi yametokea Uganda yanaathiri,

  MAZAO ; MNYAUKO WA MIGOMBA

  UGOJWA WA UKIMWI;

  Chonde chonde wabunge na mawaziri kuweni serious
   

  Attached Files:

  • ITV.png
   ITV.png
   File size:
   130.5 KB
   Views:
   404
 2. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo ni ukosefu wa uwajibikaji.
   
 3. anjnr

  anjnr JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 483
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  TBC ni Janga lingine, mimi nilishaachana nayo, kila habari lazima waikarabati
   
 4. k

  kundaseni meena Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wakuu muwe waelewa basi! mganga mkuu ITV amesema kuna mgonjwa mwenye dalili za ebola lakini bado wanaendelea na kuchukua vipimo na kuongeza tahadhali, TBC afisa afya amesema hakuna mgonjwa wa ebola aliyeripotiwa na huo ndio ukweli maana kuwa na dalili za ebola haimaanishi kwamba unaugonjwa wa ebola kwani magojwa yote ya VIRAL HAEMORRHAGIC FEVER yana dalili sawa na mengi zaidi ya kumi sasa mlitaka afisa afya alitangazie taifa ugonjwa wa ebola umeingia Tanzania kwa ushahidi wa dalili tu. kuweni wavumilivu kwani baada ya kupata vipimo vya maabara kila kitu kitakuwa wazi.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Natamani ungeliangalia suala hili na kwa upande wa pili. Ni hatari kwa jinsi huyo afisa alivyokuwa-conclusive kuwa hakuna mgonjwa wa ebola wakati uchunguzi bado unaendelea. Kama uchunguzi haijakamilika si vena kusema conclyusively iwapo kuna ugonjwa au hakuna. yeye amesema hakuna ugonjwa huo, je kamauchunguzi ukionyesha kuwa huyo mgonjwa anayechunguza anaugua ebola, atasema nini?
  Nadhani na yeye angekuwa precautious na kusema kuwa mpaka hivi sasa ni vigumu kueleza kinagaubaga iwapo kuna ebola au la na kuomba watu wawe na subira wakati uchunguzi unaendelea.
   
 6. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,589
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  [video=youtube_share;9Nu18gmYrDE]http://youtu.be/9Nu18gmYrDE[/video]
   
 7. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ebu tuondolee kichufuchefu wewe. Ulisikiliza pande zote au ndo unaiwakilisha TBCCM hapa!!! Mimi nilisikiliza tangu mchana braeaking news ya redio one by saa 6 alafu nkaangalia ITV habari na kumuona live huyo afsa saa 2 TBC. Nilivyomuona alikuwa kwanza anajibu kama sukule tu. Alisema kuna mtu aliandika humu, JF, bila kujaua kuwa ni taarifa sahihi zilizokuwa zimetoka moja kwa moja kwenye source kupitia Redio One. Pili alionekana kulaumu kuwa waandishi wanatoa taarifa bila kuwa na uhakika.

  Huyu Afsa alikuwa na mapungufu yafuatayo:
  1. alionekana wazi kutokuwa amefika kule alipo mgonjwa
  2. alipinga moja kwa moja ata bila kusema kuwa uchunguzi unaendeleea
  3. hakuwa na mawasiliano na mtoa habari kwani hakujua kuwa habari ilitolewa moja kwa moja na mganga wa Karagwe.
  nahic huyu ata kwenye mgomo wa madaktari alikuwa msaliti.
   
 8. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tunaiomba Wizara ya Afya ifanye juhudi za makusudi kuzuia/kudhibiti kuinga na kuenea kwa ugonjwa huu, siasa haiwezi kusaidia lolote. Hili siyo suala la kisiasa bali uhai wa wanadamu.
   
 9. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Nguvu zaidi zinahitajika kupambama na ebola

  [​IMG]


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] MIONGONI mwa habari kubwa zilizopo kwenye gazeti hili ni kuingia kwa ugonjwa wa ebola hapa nchini katika Mkoa wa Kagera ambapo mtoto mmoja wa miaka sita anadaiwa kuwa na dalili za ugonjwa huo.
  Ugonjwa huo unaripotiwa kutokea nchini Uganda ambako mpaka sasa umeua watu 14 na sita wanaendelea na matibabu huku wataalamu wakihangaika kuzuia maambukizi yake.
  Taarifa hizi zinakuja siku chache baada ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutoa tahadhari juu ya ugonjwa huo hasa kwa wakazi wa mikoa iliyo jirani na Uganda ambayo ni Mara, Mwanza, Kagera, Kigoma na Rukwa.
  Kwa mujibu wa taarifa za wizara, chanzo chake ni virusi vya ebola na dalili zake ni homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuuma kichwa, na vidonda kooni.
  Wataalamu wa afya wanabainisha kuwa dalili hizo mara nyingi hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi, figo na ini kushindwa kufanya kazi na kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa damu ndani na nje mwilini.
  Wataalamu hao pia wanasema ugonjwa huo huenea kwa maambukizi ya kasi na unaenea kati ya mtu na mtu kwa njia za kugusa damu na majimaji kutoka mwilini mwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huona kugusa maiti ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa huu.
  Ebola pia humpata mtu aliyegusa wanyama walioambukizwa (mizoga na wanyama hai) kama sokwe na swala wa msituni.
  Wizara ya Afya imedokeza kuwa ugonjwa huo mpaka sasa hauna tiba wala chanjo, hivyo ni vema wananchi wakawa makini na ugonjwa huo hasa wanapomuona mtu mwenye dalili hizo.
  Taarifa za ugonjwa huu zimetushtua sana kwakuwa wananchi wengi hawana uelewa wa kutosha juu ya masuala ya afya na maeneo mengi yapo mbali na vituo vya afya.
  Tungependa serikali iweke nguvu nyingi na ikiwezekana ipeleke wataalamu zaidi wa afya kwenye maeneo yaliyo na hatari ya kuupata ugonjwa huu.
  Tumezoea kuiona serikali ikifanya kazi kwa utaratibu wa zima moto, ambapo hungoja mpaka jambo litokee ndipo hutuma wataalamu wake kwenye maeneo husika.
  Tunaamini kuwa huu si wakati wa kufanya kazi kwa mazoea, ugonjwa wa ebola ni hatari hivyo hata mapambano yake yanahitajika yawe makubwa zaidi.
  Serikali isipofanya jitihada kubwa katika kupambana na ugonjwa huo watu wengi watapukutika, wananchi wanaitegemea zaidi serikali iwanusuru katika janga hili.
  Tunawaomba wananchi watoe taarifa kwa waganga wakuu wote wa mikoa na wilaya walio karibu nao mara wanapoona kuna mtu ana dalili hizo kama ilivyofanyika huko Kyerwa.

  Source: Tanzania Daima 5/8/2012

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 10. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Na wewe nawe, TBCcm unaangalia ya nini?
   
 11. k

  kundaseni meena Member

  #11
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  uko sahihi.
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  TBC uhongo wa uhakika!
   
 13. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2014
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Avatar yako ahahahahaaaaaaaaaa!
   
 14. rushanju

  rushanju JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2014
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 2,343
  Likes Received: 1,057
  Trophy Points: 280
  Kukanusha ndo utamaduni na utendaji wa viongozi watu wengi. Anzia kwanza Ikulu na wizara zote kila jambo ni kukanusha. Angalia pia suala la kupotea watoto hapa DSM na kauli za Kova. Huyo ofisa wa Kagera yuko kazini na pale anaonekana kutekeleza uongozi bora chini ya serikali ya chama tawala. Nadhani hats hii post wakisoma watakanusha.
   
 15. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2014
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,032
  Likes Received: 37,800
  Trophy Points: 280
  Tuwe makini hii inaweza ikawa ni mbinu ya kupunguza nguvu habari za UKAWA na katiba mpya kwa ujumla.

  Refer uzoefu wako.
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Oct 19, 2014
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hii habari ya 2012 nani kaiibua huko ilikokuwa??
   
 17. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2014
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,512
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Hapa sengerema mtu amekufa kwa dalili zote za Ebora...viongozi wanakanusha na wakati huohuo wamewaweka karantini Dr & nurses waliomhudumia huku wakiacha watu kuendelea na mazishi ya kawaida...upuuzi tu
   
 18. ladyisa

  ladyisa JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2014
  Joined: Aug 23, 2014
  Messages: 663
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hiyo avatar kweli ni shida
   
 19. Deo Corleone

  Deo Corleone JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2014
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 14,671
  Likes Received: 2,545
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. bily

  bily JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2014
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 8,028
  Likes Received: 3,938
  Trophy Points: 280
  TBC is fourth enemies which our country should fight for after Ignorance,Poverty and Diseases.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...