ITV na maswali ya kipima joto-- napata taabu sikiliza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ITV na maswali ya kipima joto-- napata taabu sikiliza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nicholas, Jun 1, 2012.

 1. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli ITV nimeipenda ktk kurusha habari live na vipindi vya Masako kwani huwa maswali yake tofauti na waandishi wengine tz huwa yana kuwa mind provoking na mwansiasa kilaza jasho linatoka na hata akiachiwa punzi wasikilizaji wanajua kashindwa.

  Cha kusikitisha ni ktk maswali yao ya kipima joto, na vipindi vyao vingine km malumbano ya hoja, vinakuwa na mada zinazonpa taabu kuzipenda au hata kuamini kuwa zimetunngwa na mtu anayejua nachotaka. Nyingi zina haya:

  -Too obvious na swali linalofuatia linakuwa awkward hata km statement ya mwazo imelitoa thamani swali linalofautia.

  -Maswali mengine ni too directing and one one way ingawa wao wanayapa 3 options.

  -wale jamaa wao wa mitaani huwa wanahoji watu wa aina moja, either asiojua kabisa na wa upande mmoja.au hata mmoja halafu wanaconclude kuwa maoni wa baadhi ya watu jijini.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ingekuwa ni mtihani wa research ITV wangefeli vibaya sana. Badala ya kuuliza swali wao 'wanalisha' watu majibu'
  Kwa mfano wanauliza; "Watu wanaokiuka sheria, je, waadhibiwe?
  Ni vigumu kuelewa elimu ya watu wanaondaa hayo maswali, itoshe tu kusema ITV wanatia aibu.
   
 3. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Haha , km hapa km tayari ni kosa kutokana na sheria, adhabu ni obvious....hapa angalau wangelekeza swali ktk aina na kiwango cha adhabu..angalu wangeleta hata ka sense.Maswali ya Kikwete ,palipo na ushahidi bado adhabu haipo wazi
   
 4. b

  bia JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sijaona fact katika hoja zenu hapa..lile ni kama swali linaloulizwa kwa m2 yeyote mtanzania ajibu kwa maoni yake,na hata kama hujaulizwa wewe unapaswa kujiuliza na kujijibu bs jibu upatalo ndilo wanalotaka uwape ijapo ngumu kuwafikia wote.pole kwa kutatizika
   
 5. P

  Professa Member

  #5
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijawahi ona maswali mabovu kama ya kipima joto. Binafsi nafikiria wanaojibu maswali ya kipima joto kwa njia ya message ni wafanyakazi wa ITV peke yao, haiingii akilini kama kuna mwananchi wa kawaida anaweza akapoteza fedha yake kwa ajili ya upuuzi wao. Are they really serious? I don't think so. Even mada zao za kwenye malumbano ya hoja huwa napata tabu sana. Kama leo mada, "Viongozi wanaotoa matamko, ahadi na vitisho bila utekelezaji, je huu ni uwajibikaji?". Matokeo yake, mara nyingi sana kwenye malumbano ya hoja watu wanaamua kuanzisha ka sub-topic kao ka kudiscuss kwa maana main topic either ni too obvious, not clear au nonsense.
   
 6. r

  rugeruga New Member

  #6
  Jun 1, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi huwa sitaki hata kusikia swali la kipima joto, huwa nabadilisha station haraka inapofikia time ya swali!
   
 7. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Maswali yao yote yana majibu tayari. "Wanaotorosha wanyama hai nje ya nchi, je ni wazalendo?". Hivi haya si ni majaribu, atayejibu ndio labda ni mtoroshaji mwenyewe!
   
 8. H

  Hurricane Member

  #8
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa kweli hawa jamaa hata mimi kiwango chao cha ufahamu huwa kinanitatiza. Haiingii akilini kwa mtu mwerevu kuuliza maswali ya kijinga na kipumbavu kama ya hawa jamaa wa ITV. They are realy bogus. Na wanaudhi kusema ukweli, basi tu. Ningekuwa na jinsi hivyo vipindi wasingerusha kabisa.
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Yapo mambo mengi lakini makubwa mawili yaliyonifanya nibadilishe channel ni: swali la kipima joto, na George Marato.
  Kwenye kipima joto nirudie, ITV hawaulizi swali, wanauliza majibu. Hii ni aibu yetu sote watanzania maana haiwezekani organisation nzima isiwe na mtu anayeona hilo. Huwezi kuuliza "aliyefanya kosa aadhibiwe?

  Kuhusu George Marato, nahisi ITV wameamua kutoka nje ya ethics za journalism. Mtangazaji habari anajigeuza kuwa habari kwa kuigiliza sauti tena hata kwa mambo yaliyojaa huzuni.
   
 10. o

  oyaoya JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli mengi ya maswali yao hayana mvuto wala changamoto. Halafu katika tafiti kuna 'sample space' kujua hao wanaowakilisha wana uzito gani kwa idadi yote.
  Nimefuatilia sana matokeo wanayotangaza na nadhani wapiga kura wao hawazid 10 kwa siku. Haiingii akilini kuwakilisha watazamaji zaidi ya laki tano!
  Ni vema wangetafuta namna ingine ya kuwashirikisha watazamaji wao au swali moja lichukue muda kidogo badala ya kila siku kuibuka na mada mpya matokeo yake ndo "je, wasioweza kulipa 200 Kivuko cha Kigamboni wapige mbizi?"
   
 11. K

  Kimbito nyama Senior Member

  #11
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kuwa kipimajoto cha ITV kama wewe ni mtafiti hakikidhi, lakini ni vizuri sana ukanyambulisha malengo ya ITV kwenye kipimajoto nini? nadhani wanataka hata mtu ambaye hana shule kabisa aweze kufunguka na kujibu. Mimi naona labda kuna tatizo jingine la dislike yako/yenu, pengeine kwa kuwa kuwa wamekuwa huru sana kurusha matangazo bila kujali shinikizo la serikali, kwani hadi Mtwara vijijini sasa tunaona mambo yanayoendelea kwenye taarifa zao LAKINI TBC ambayo inapaswa kuwa ya Tifa inachuja habario kwa uoga
   
 12. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mkuu acha ushabiki bana hawa watu wanafanyakazi chini ya kiwango tarajiwa ndo maana ya hoja hii........pale ni sehemu ambayo kama itatumika vizuri kero nyingi za wananchi zitakuwa aired na kujadiliwa bana sio kuuliza eti "Wanaokatisha ruti za daladala je Sumatra wawajibishwe?" sasa hapo kuna malumbano gani au kuna joto gani la kupimwa?????

  Mzee Mengi ana heshima na anapata tuzo nyingi sana ni wakati sasa aangalie uwezekano wa kuwapa hawa watu na kituo chake hadhi inayomstahiki yeye.........yaani afanane nacho.....specifically ITV.....kwa kuanza na vipindi hivyo na ile ya asubuhi pale wanapohoji wageni.....huwa wanapwaya saaana na wanaonekana kuwa obsessed na outweighed na baadhi ya waalikwa

  Kwa mfano; Aajiri watu wa fani mbalimbali ili kunapokuwa na mahojiano na say waziri wa sheria pale dakika arobaini na tano basi huyu awe anauliza maswali ya kitaalamu haswa yenye contradictions akiwa pamoja na Semunyu ili kupata ladha.......sio kama Kibonde (m sorry to mention) anapohoji kilaaa kitu kuhusu nyumba wakati yeye si mtaalamu wa hiyo fani .....yaani watazamaji wanapata maoni ya muhojiwa basing on knowledge na utashi wa muhojaji......akiamua mapazia haya.....kesho tiles twendee...... hata kama kuna editor still hawezi kuwa mzuri katika kila fani

  Wanajitahidi sana ila wanaweza kufanya vizuri zaid ya hapo walipo sasa
   
 13. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Haki ya Mungu mtoa mada leo umepatia. Hoja nzuri sana umeibua. Kama kuna maswali ya kijinga kabisa katika ulimwengu huu, basi ni ya kipima joto ITV. NImewahi kuzozana na mke wangu kwa kutobadili stesheni ya TV baada ya kipindi cha kipima joto kuwadia. Sikipendi kabisa. Maswali ni ya kijinga hakuna mfano wake hapa duniani. Swali kama, "Je, watendaji wasiwajibika, wawajibishwe?" NI swali gani hili? Ujinga mtupu. Kama kweli Mengi anasoma humu JF, basi abadili haraka sana aina ya maswali maana bila shaka ni yeye aliyeyabariki.
   
 14. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Options ni NDIO/HAPANA/SIJUI(N/H/S). Najua nyie ndio mmezoea jibu mitihani iliyokosewa ,kwa vile unajua hilo swali litoka mwaka fulani basi unamsaidia kujibu mtunvi feki wa kibongo.But what if swali limekosea ktk structure na logic in asuch a way hakuna jibu.Na hapa simaanishi yale mswali ya maltiple choic yenye ALL OF THE ABOVE,NONE OF THE ABOVE.


  Kuna maswali mengi sana hayapo proper hata university za kibongo na smart kids wanaoamini kile wanachokijua wnashindwa jibu, na hawawezi jibu uongo ili wapate maxi, mbaya hakuna wa kumweleza arekebishe kuanzia mwalimu hadi baraza.Kwani time haipo on his/her side na uelewa wa wasomi wabishi wa kibongo hasa wenye experience hauna tofauti na wabunge wa ccm wataleta madhara.

  E.g Suppose upo safi ktk physics na unajisomea beyond the class wakati mwalimu anasubiri hadi baraza la mitihani lipitishe kitu kipaya na kuwatangazia.Wewe una hakina kuwa tayari kamati za wanasayansi zimepitisha kitu kipya na kimeshaanza ingia ktk real life na comsumer products zinafanya kazi halafu unakutana na swali la kipuuzi km hili:

  How many states of matter are there?

  1.30
  2.1
  3. 3
  4.14

  kwa haraka utaona mtunzi mzembe kaweka figure anazofikiri kuwa zitakupa maxi za chee km unakumbuka alichokufundisha au common sense ya wabongo inavyowatuma.na hapa atakuwa anamaanisha 3.Yaani gaseous,solid, na liquid.

  kwa haraka unajua kuna Plasma, Neutrons, etc,lakini hat akam hukumbuki nyingine bado hizo figure zote si sahihi, unajaribu rudi uone hata km kaweka neno Common, popular au equivalent yake ktk swali, unakuja halipo na km lingekuwepo bado plasma ni popular ktk jamii haswa ktk dispaly screen, ktk nuclear plants, na neutrons ni popular ka stronomy...unapata shida kwani tayari upo mbele ya elimu ya kibongo... una kwama na unahisi kuwa somewhere watawaambia kuwa kuna swali lina makosa yanatajwa mengine.Then unapata taabu ..unahisi kuwa kwa ujinga wa walimu wetu wanakulazimisha uchague 3.

  Hapa ndipo utaona kwanini wabongo ni taabu tunamjibia hadi Mungu kwa assumptions,kwanini smart kids wanakuwa bored na elimu yetu.Unajikuta unahitaji ama umfurahishe mwalimu kwa kumpa jibu alipendalo na baadaya kujikuta umefikia hatua ya kufanya kila kitu km yeyote apendavyo na si km fikra na mawazo mapya yako yanavyoweza chambua na kubuni.

  Kwa hiyo ndugu yangu bongo kuna vingi vinaboa: kuanzia waandishi km akina Kibonde na Nkamia, na hao wa kipimajoto, ktk majibu ya viongozi za dini,, ktk Bunge,vitabu vyetu, project zetu zinazonadiwa sana lakin hazitoki nje ya incubators/nursery ktk governement, ktk familia ktk jamii forum pia kuna posting za hivyo, na wanaopost wanaamini wapo sahihi sana kiasi ch akutukana wengine na kuomba ban.Sasa km unapata muda ktk TV zetu at any particular time unaweza ukashindwa pata TV ya kuangalia.
  Unakuja show mawaziri wanawake wanaocheza style ya kikongo wana matumbo mabaya,na sehemu nyingine za mwili zipo nje na wanakata mauno kwa style ambayo hata kicheche anajua ilitakiwa iwe ya faragha, halfu kuna waziri anaonekana kuwa alihudhuria, then unaingia ktk taarabu, unakuta wamevaa ndio ila wamezisisha make-ups na wanacheza bila step, halafu wanajifagili apora mtu mme wake, ukirudi kwingine kuna Hemed kapewa jina la kikristu ktk movie na videm vya kibongo, vinashuka yai la kizaramo. huwezi tofautisha "lap" na "rap", "right " na "light" ,and the sort unapata taabu tena.Napat ashida kujua anamaanisha nini anaposema "Thats light" wakati anapesa kidole kwa maringo ktk chumba cha wageni ila upande wa kidole kuna taa, na masungumzo yanamaanisha "Thats Right".Na movie in kiswahili na kithungu.Na lengo lao ni kuuza hadi nje.assume mthungu hakuelewa masngumzo ktk kiswahili.
   
 15. m

  mjasiria JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 3,790
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  hahahahahah qwa qwa qwa mkuu umenivunja mbavu sana lol
   
 16. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  kuna siku waliuliza je viongozi wanaofilisi mali za umma wanafanya vizuri?,mi nikajibu makusudi ndiyo
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,616
  Trophy Points: 280
  Maswali hayo yanaitwa "leading questions" ili kutengeneza jibu la ndiyo, hapana au sijui. Maswali yanawekwa simple, obvious na straight forward ili ku hamasisha wengi wajitokeze kujibu ili nao wavune pesa kwa kutumia zile number za mavuno!.
   
 18. ARV

  ARV JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 180
  Maswali ya kipimajoto ITV
  1.Kundi linalosababisha vurugu zanzibar, lipo juu ya sheria?
  2.Mawaziri walioboronga, je waondolewe?
  3.Wananchi wanaotiririsha maji machafu barabarani, Je washitakiwe?
  4.Wazanzibar kuchoma makanisa,Je wanavunja sheria?
  5.Viongozi wa vijiji walioiba fedha za ruzuku ya pamba, Je washtakiwe?

  Etc....etc...etc......
   
 19. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #19
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Leading to what?ktk survey hakuna hicho kitu.majibu hayo ili yasiwe biased yanahitaji kuto-leading the target to any of the answer,but to the understang of the question ili wajibu kwa mtazamo wao na si wa researcher.

  Kuwa simple si kuwa biased.ikiwa biased basi hiyo survey itakuwa namalengo tofauti...mf. km kunahitajika kiini macho kuwa palipigwa kura ,ila mshindi piga ua lazima awe fulani, basi panakuwa na hizi leading au hata obvious rigging.(biaseness) ,otherwise bora ujijazie tuu hizo kura. Au utoe statement yako.

  Sishangai ukiwa na fikra za intelectuals wa mlimani.wengi nawasikia majukwaani wakitoa definition ya Katiba kwa maneno fulani ambayo si specific na yanayokuwa any meaning.Ni watu waliozoea kuulizwa maswali yaleyale na kuto amajibu yaleyale .Ndio maana swali likiwa limekosewa hata km kwa nia ya kutega wabongo watajibu jibu walilolikariri na mara nyingi na walimu wao wanakuwa walikosea kweli ila nia yao ilikuwa ni kuliuliza km mwanafunzi alivyotegemea. ha..ha. hawa jamaa ni vilaza.


  Imekaaje ukimuuliza demu anayekudanganya na kukuchuna sana."..Je ..Mpenzi nahitaji kuamini kuwa unanipenda sana...?" jibu N- km ni ndio, hapana H- kama ni hapana , na S- km hujui...then conclusion majibu ya mpezi wangu ni kuwa Ndio.Disclaimer....haya ni majibu ya mpenzi/honey/mboni ya jicho/malaika wangu na si ya kwangu...
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Maswali ya ITV ni biashara, utalojibu umeliwa, kila jibu shillingi ngapi? 150 nadhani.
   
Loading...