ITV na kuisafisha Barick-North Mara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ITV na kuisafisha Barick-North Mara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by carmel, Sep 18, 2009.

 1. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa wiki hii nimeona taarifa kama mbili zikiripotiwa na Steven Chua wa ITV aliyeko Nyamongo huko Tarime - Mara kuhusu ile ishu ya uchafuzi wa mazingira ulioleta mgogoro na wananchi.

  Kilichonishangaza ni ambavyo huyu jamaa anaripoti hizi habari, jamani wote tulishuhudia watu na mifugo walivyoathirika hadi wabunge na mawaziri wakaenda huko. Sina uhakika ni nini kilifanyika baada ya wataaalamu kibao kwenda huko lakini inaonekana wazi kuwa kuna jitihada mahususi zinafanywa na ITV kuisafisha Barrick na kutupa lawama zote kwa wananchi as if they deserve whatever happened to them.

  Mimi sijaelewa kweli barick wana mkono mrefu, yani ni maji marefu hawashikiki especially kwa nchi kama TZ yenye viongozi bongolala, ila inaudhi na inauma kutupa lawama zote kwa wananchi.

  Na HAWA WAANDISHI WA HABARI MBONA VIGEUGEU HIVI? LEO WANA-REPORT Hivi kesho wana-change, tutafika kweli?
   
 2. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alichoripoti Steven Chuwa ni cha ukweli kabisa. Mimi nilikuwa huko wiki 2 tu zilizopita, lile "jamvi" ni kweli lilichukuliwa na wananchi wanaozunguka mgodi huo na wameezekea nyumba zao na hivyo kufanya maji yatiririke kwenda mto Tigite na sehemu zingine. Hebu na sisi kabla ya kutoa lawama, tuwaelimishe wananchi madhara ya kuiba jamvi lile linalozuia maji kutiririka. Muulize Afisa Uhusiano wa mgodi Ndugu Masanda Omutima ambaye ni mzaliwa halisi wa Nyamongo atakueleza ukweli wala hana cha kuficha.

  Pamoja kwamba inatia uchungu kuona wananchi wamepata madhara ya kiafya, lakini ni matokeo ya wachache wao kuwa na tamaa ya kujichukulia mali zisizo zao na ambazo ziko pale kwa ajili ya kulinda afya zao ndiyo maana wakadhurika. Mgodi haujawashitaki wananchi wahusika ambao lile jamvi linaonekana katika mapaa ya nyumba zao na wengine wamefanya uzio katika mazizi yao ya ng'ombe na hivyo kuwaachia Serikali ya kijiji ishughulike nao. Wao wanaendelea na kazi ya kutandika jamvi jingine kuzuia uvujaji wa maji.

  ITV imeleta hali halisi ya mambo yalivyo. Tusitake kupotosha umma.
   
 3. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yaani hiyo kitu nimeiona mtu and I felt the same way kuwa wanatumika ili kuisafisha Barrick.Yaani sijui hawa activists wetu waliokuwa wanafuatilia hili suala wamefikia wapi au tuseme report zilizotolewa na ITV wamezichukuliaje?
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwa nini wakati wizi huo wa lile zulia unafanyika Barrick walikaa kimya tena kwa muda mrefu tu! Hawakujua madhara yake na hivyo kuwatahadharisha watu.

  Kwa nini Barrick hawakuweka ulinzi, mabango ya tahadhari eneo lile ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wakazi wa eneo lile?

  Namfahamu Chuwa na waandishi wa aina yake kuwa ni wapenda bahasha za khaki sana tu.
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kweli hii inadhihirisha kwamba watu wengine mmelishwa limbwata na barrick.hivi mtu mwenye akili timamu na mawazo huru unaweza ukasimama kutetea ufirauni uliofanywa na barrick north mara dhidi ya watu wa nyamongo? wewe hizo wiki mbili ulizokuwa huko ulifika kwenye mabwawa yanayotiririsha kemikali au ulipelekwa alikopelekwa kagasheki?au unajaribu kudanganya umma hapa kwa sababu zako binafsi.

  watu wangapi nyamongo wameezekea hayo mazuria ya barrick?miaka yote kabla ya barrick nyamongo ilikuwepo na itaendelea kuwepo tena bila kutegemea hisani ya barrick.

  hivi unadhani kama wananchi wasingemtonya kagasheki unadhani ukweli ungejulikana lini?si mlishaanza kuwatisha wananchi na kuwakamata na kuwaweka ndani?unadhani yule mwandishi wa mtanzania aliyeripoti kwa ukamilifu uharibifu unaofanywa na barrick na kisha kusababisha torture kwa watu wa nyamongo mngekuwa mnapiga porojo hapa?

  yaani mtu unapita nyamongo na kukaa baa na kupata bia zako mbili tatu halafu unakuja hapa na kujidai ulikuwa nyamongo na kuleta ushuhuda wa uongo. huyo msemaji wa mgodi unategemea atasema nini kama sio kutumikia kibarua chake?

  Startv waliwahi kurusha kipindi cha dira ya mnyonge kikielezea jinsi mambo yalivyo nyamongo wakaweka ukweli wote hadharani.unafikiri hatujui juhudi zinazofanywa na barrick kwa kushirikiana na serikali ili kuficha ukweli.

  sio kila mara mnakuja hapa na maneno mbofu mbofu ilimradi muonekane mnajua kila ktu kumbe mnaongea utumbo tu.

  kama kuna mtu kaiba jamvi akamatwe ashitakiwe kwa mujibu wa sheria, kinyume na hapo muache madharau yenu na muendelee kuwa watumwa wa wazungu wa barrick, maana wamewageuza kuwa makasuku mnaimba kila wanachowaambia.

  watanzania muamke usingizini, muondokane na mawazo duni mnatetea hata ujinga.

  Nyamongo hawadanganyiki!
   
 6. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ni jukumu lao kuweka ulinzi around maeneo hayo, maana hao wachache ambao wameiba kama wangedhibitiwa kabla hawajaiba madhara yasingewakuta watu wengi ambao hawahusiki na wizi huo. hapa hakuna cha kutetea, wawe responsible and thats it. huyo masanda o0mutima unaemsema si mzaliwa wa tarime, ni mjita huo na yeye anachosema kwangu mimi hakina uzito maana ni mwajiriwa wa barick ambaye atafanya chochote ili kutetea unga wake, the same kwa yule afisa uhusiano mwingine nani sijui aliyekuwa anatetea kwa nguvu kwamba madhara yale hayajaletwa na barick. Sasa hata wewe ndo wale walewale vibaraka wa barick hamjali madhara kwa binadamu, mifugo wala mazingira as long as mnapata milion 1.30 kwa mwezi huku dhahabu yote inaenda ulaya, what a shame.
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Yale yale ya Mwizi akikamatwa auliwe - Miafrika Bwana!!!
   
 8. Z

  Zurich Member

  #8
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Watanzania wenzangu, Madhara yanayosababishwa na Barrick (chemical seepage), yanaathiri mazingira (maji, viumbe na mimiea) na afya za watu (human health), na yatakuwa ni vizazi na vizazi, hapa swala ni uwajibikaji ili kupunguza athari maana tayari zipo, na sio baadhi ya watu kuja hapa na kujaribu kutetea.

  Wazungu watachimba dhahabu na itakapokwisha wataondoka, watatuachia mashimo, umasikini, maji taka na magonjwa ya muda mrefu(genetic). Serikali na wanamazingira wa Tanzania wasaidie kwa dhamira ya dhati kutatua hili tatizo na sio tu kwa nyamongo lakini na sehemu zingine ambazo kuna hawa watu tunaowaita wawekezaji. La sivyo itafika kipindi, ambapo, tunakuwa na mito, au visima, lakini hatuwezi kutumia maji yake maana yamechafuliwa na kemikali.

  Itabidi maji ya kunywa tununue dukani, napata wivu ninapoona nchi kama Switzerland, kila baada ya hatua 50 hivi, unakutana na spring water (fountain), haya ni maji yanatoka bombani, ni maji safi na salama, tena ya baridi, ni maji yanayotoka milimani moja kwa moja hivyo kama una kiu, you just tape and drink na huna haja ya kuchemsha. Maana mazingira ni safi.

  Tujifunze ndugu zangu!
   
 9. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Yaani wewe ulikuwa huko wiki mbili (tu?) zilizopita na sasa unahakika kabisa kuwa taarifa ya ITV ni ya ukweli? Umeishi North Mara kwa muda gani? umefanya uchunguzi kwa muda gani? uchunguzi wako ulihusisha nini na nani? uchunguzi wako ulidhaminiwa na nani au nini?

  Watu kama nyie mngekuwepo wakati wa Karl Peters nadhani mngeuza hata miili yenu kwa wakoloni.
   
Loading...