ITV Mnachotufanyia Kwenye Isidingo, Is Not Fair At All!. Msitufanye Tuanze Kumkumbuka Mzee Reginald Mengi This Soon!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
31,752
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
31,752 2,000
Wanabodi,

Mimi ni mshabiki wa tamthilia za ITV Tangu imeanzishwa, walianza na "Egoli" Place of Gold, ndipo wakaja na "Isidingo" The Needy.

Kitu ambacho ITV imejijengea heshima kubwa, ni ile concistance yake, Isidingo ni saa 1:30 usiku. Kwa vile naipenda sana tamthilia ya Isidingo and I can't afford to miss it, kumenifanya niwe a very good father, kila saa 1:30 jioni lazima niko home, unless otherwise.

Ikitokea kwa sababu yoyote nimemiss episode ya jioni, kesho yake asubuhi saa 3:30 nitaangalia marudio nikiwa popote kupitia simu yangu kwa kutumia ile ITV online kwenye play store.

Kitu ambacho I never miss ni marudio ya wiki nzima, Jumamosi usiku kuanzia Saa 5:00 usiku, baada ya kumuangalia Zomboko na Hawavumi lakini Wamo.

Wiki hii nilikuwa busy hivyo sikuweza kuangalia Isidingo wiki nzima, hivyo jana jioni nikasubiri marudio ya wiki, hayakuwepo, bila hata scroll ya kuapologize.

Baada ya kukosa marudio ya jana
marudio mengine ya wiki ni Jumapili saa 4:00 asubuhi. Muda huo ni muda wangu wa kanisani huwa nasali misa ya pili. Lakini kutokana na jana kutokuwepo marudio ya wiki, leo ilinibidi nijihimu kuamka saa 11:00 alfajiri kusali misa ya kwanza saa12:00 asubuhi hadi saa 3:00 ili saa 4:00 niangalie marudio ya wiki,

Ilipofika saa 4:00 kuwasha ITV, duh...!. Isidingo haipo!. Kulikuwa sijui na likipindi gani, kwa vile nilipania Isidingo, hata wangeonyesha kipindi kizuri vipi, mimi bado ningeona ni likipindi tuu!.

Where is the ITV concistance?. Ukiwa fan wa tamthilia fulani, unakuwa na addiction, ukikosa unapata withdrawer symptoms ya hasira na kukasirika, ingekuwa sababu ni live program, huwa tunaelewa na tunavumia, lakini kuondoa Isidingo kuweka recorded program yoyote, sio kututendea haki sisi watazamaji wenu watiifu.

Wito kwa menejmenti ya ITV, tunaomba mtutendee haki sisi watazamaji wenu, kipindi fulani kwenye series kisipokuwepo kwa sababu yoyote, tujulisheni kwa scroll.
Hata kama alipokuwepo Mzee alikuwa hafanyi lolote kwenye programming na scheduling, hatukuzoea kuona mambo kama haya, sasa kwa vile Mzee Mengi hayupo, halafu, yanatokea mambo kama haya, msitufanye tukaanza kumkumbuka Mzee Mengi, kuwa haya sasa ndio yanatokea kwa vile Mzee hayupo!.

Japo baada ya hicho kipindi, Isidingo ilikuja kuonyeshwa, two episodes za mwanzo zilikuwa skipped, missing two episodes, is a big loss kwa mfuatiliaji wa haya makitu. Matatizo kama haya hakuna kabisa kwenye DSTV, kwa kutumia Explorer, unarekodi episodes zote na utaangalia at your own time, ITV hawana PVR, na kwenye DSTV hawapo, what a loss?.

Msitufanyie hivi.
P.
 

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Messages
4,502
Points
2,000

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2014
4,502 2,000
Isidingo the best soap opera ever

Mimi pia ni addict wa Isidingo...siku ITV wakiachana na soap hii ndio mwisho wa kuwaangalia maana huwa nawacheki kwa sababu ya pgm hii hata niwe foleni nawacheki online ila ni kweli reliability imeanza kuyumba kwenye programming...jipangeni azam MUX inakuja na Uhai TV huenda akawa competitor wenu mkubwa...Uhai wakinunua Rhythm City soaps mmekwisha.
 

sosoliso

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Messages
8,374
Points
2,000

sosoliso

JF-Expert Member
Joined May 6, 2009
8,374 2,000
Since tumenunua tv 97, nimeikuta ikirushwa enzi hizo ITV unaishika kwa kutumia antena aina ya Sonnet..

Hadi sasa na familia, ipo tu.
Mkuu umenikumbusha mbali sana hizo antenna za Sonnet.. Kabla ya World cup Marekani 1994, tulinunua pale Golo Store mtaa wa Uhuru zilipoingia tuu..
 

OS Cordis

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Messages
8,625
Points
2,000

OS Cordis

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2016
8,625 2,000
Mkuu umenikumbusha mbali sana hizo antenna za Sonnet.. Kabla ya World cup Marekani 1994, tulinunua pale Golo Store mtaa wa Uhuru zilipoingia tuu..
Ndio ilikuwa kiboko ya analog, KBC, UBC na channel kibao za Kenya zilikuwa zinakamata kwa uzuri kabisa.

Maisha yanaenda kasi sana mkuu..
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
31,752
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
31,752 2,000
Niliangalia sana Egoli.
Isidingo nimeshindwa kutokana na nature ya kazi
Mkuu St. Ivuga, kumbe na wewe ni wa longi, Egoli ilipokatishwa niliumia sana, ndipo nafasi yake ikachukuliwa na Isindingo.

Lakini Egoli iliendelea kwenye SABC 3 kwa miaka mingi mbele.
P
 

Forum statistics

Threads 1,355,187
Members 518,609
Posts 33,102,899
Top