ITV mmekuwa zilipendwa. Azam imewapiga bao la kisigino

hayaland

JF-Expert Member
May 4, 2012
712
399
Itv ni moja ya kituo cha television kilichokuwa kizuri mno hasa kwenye eneo la taarifa ya habari hapa chini. Ulipokuwa unaikosa hiyo taarifa inakuuma sana moyoni.Ila kwa kipindi hiki kituo hiki kinaanza kufa kwani taarifa zao za zamani za kiuchunguzi haziko tena,Na mbadala wake imeibuka Kituo kimoja matata sana nayo ni Azam TV, ni moja ya kituo cha tv ambacho ukiangalia taarifa zake huna hamu ya kusoma magazeti ya kesho yake wanakuwa wamemaliza kazi.Taarifa zao zinasisimua hadi raha. Vituo vinavyoelekea kufa kifo cha mende ni Itv, na Channel 10 kwisha kabisa.
 
Ni kweli mkuu kiukweli taarifa zao hazina mvuto siku hizi,wabadilike bhana ili tuwe na vituo kibao vyenye ushindani,itv walikuwa wako poa sana ila tunataka waamke warudi kama zamani.
 
Hio Ndio faida ya kujifanya ITV ni CONSERVATIVE,wapambane na hali yao TU.
 
Hawa Azam wana ramba ramba nmekuwa nikiwasikia kusifika sana hasa katika nyanja za habari, hivi bado hawajakamatia namba DSTV kweli niprove hilo au nikagonge kwa jirani?
 
Nlikua naipenda Sana hii station Lakin siku hiz big NO haina ubunifu wanafanya kaz kwa mazoea business as usual baba mkubwa angalia hii kitu rudisha heshima yako mzee wangu
 
Azam inawatazamaji wangapi hiyo ni TV inaishia kisarawe huwezi ifananisha na itv itv kwa vyombo vya habari hapa tz inajitahidi ukilinganisha na vyombo vingine vya habari japo maboresho ni muhimu kushauri
 
Kwa sasa ITV imekuwa sawa na TBC tu, yaani n ni copy and Paste. Kwa sasa ITV wao habari kuu ni Magufuli na serikali yake tu, Magufuli akienda hata Kanisani kusali basi siku hiyo ni habari kuu kwa ITV, hapo wataanza kumuonyesha akipiga magoti, akitoa sadaka mpaka akilishwa mkate(Ekaristi) nk.

Nina hisi huenda Mengi ni mkwepa kodi mkubwa sana, na ameshasoma alama za nyakati hivyo anajipendeka kwa mkubwa ili kuepuka Kibano.
 
Si kweli,Azam wanaonakana nchi nzima kupitia ving'amuzi vyao,kagera,kigoma mwanza iko poa sana ukiwa na kifaa hivyo.
 
Itv ni moja ya kituo cha television kilichokuwa kizuri mno hasa kwenye eneo la taarifa ya habari hapa chini. Ulipokuwa unaikosa hiyo taarifa inakuuma sana moyoni.Ila kwa kipindi hiki kituo hiki kinaanza kufa kwani taarifa zao za zamani za kiuchunguzi haziko tena,Na mbadala wake imeibuka Kituo kimoja matata sana nayo ni Azam TV, ni moja ya kituo cha tv ambacho ukiangalia taarifa zake huna hamu ya kusoma magazeti ya kesho yake wanakuwa wamemaliza kazi.Taarifa zao zinasisimua hadi raha. Vituo vinavyoelekea kufa kifo cha mende ni Itv, na Channel 10 kwisha kabisa.

Du!Chanel 10 inasakamwa!!
 
kama hawasifii north empire party na watu wake maana ndio ufalme wenye hasira kitakufa lakini kama wapo kati hakifi!
 
Kule yupo Mzee Tido,Mzee mwenye uzoefu wake toka BBC LONDON, ninyi mlimuona wa nini alipokuwa TBC yenu zilipendwa, Azamu wakamuona wa maana kabisa,acha Azam wawachape tu
 
Azam inawatazamaji wangapi hiyo ni TV inaishia kisarawe huwezi ifananisha na itv itv kwa vyombo vya habari hapa tz inajitahidi ukilinganisha na vyombo vingine vya habari japo maboresho ni muhimu kushauri

Si kweli,Azam wanaonakana nchi nzima kupitia ving'amuzi vyao,kagera,kigoma mwanza iko poa sana ukiwa na kifaa hivyo.
 
Kwa ufupi ni kwamba azam TV wamekuja kusambaratisha media za bongo na nchi jirani.siri yao ni uwekezaji mkubwa wa mtaji na kufahamu mahitaji ya mfuatiliaji wa media...
 
Back
Top Bottom