Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,582
Wanabodi,
Nilikuwa naangalia taarifa ya habari ya ITV leo asubuhi na kukutana na habari hii ya ITV kulitangaza Live Bunge la Afrika Mashariki, (japo habari yenyewe ni ndefu zaidi ya dakika 5 ambayo ni kinyume cha kanuni za Radio/TV News Clip), habari hii ni habari njema sana kwa Watanzania, sio tuu ili kulifahamu zaidi hili Bunge la Afrika Mashariki, bali pia Watanzania watapata fursa ya kuufahamu zaidi Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Tukubali, tukatae, Watanzania tuko nyuma nyuma katika kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana kwa Mtangamano wa Afrika Mashariki, hivyo kitendo cha vyombo vya habari vya IPP, kulitangaza live vikao vya Bunge la Afrika Mashariki, kinastahili pongezi za dhati!.
Na kwakufanya hivyo, Kituo cha ITV sasa, licha ya kuwa ni chombo cha habari cha binafsi, kwa kulitangaza live Bunge la Afrika Mashariki, ITV sasa inafanya kazi ambayo ingepaswa kufanywa na vyombo vya habari vya umma, hivyo sasa ITV ni zaidi ya Televisheni ya Taifa!.
Tangu kuasisiwa kwa Jumuiya mpya ya Afrika Mashariki na kuundwa kwa Bunge la Afrika Mashariki, hii ndio mara ya kwanza katika maisha ya bunge hili, kuendesha kikao chake jijini Dar es Salaam.
Japo siko ndani ya Sekretariati ya Afrika Mashariki, EALA, au Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, naamini EALA walituma maombi kwa Televisheni ya Taifa (TBC) kuiomba TBC kulitangaza live bunge hili, TBC itakuwa ilitoa majibu kuwa hili haliwezekani kwa sababu kikao hiki cha EALA kitakuwa kinakwenda sambamba na vikao vya Bunge la Katiba ambavyo TBC inalitangaza live, hivyo its logical kwa TBC haiwezi kutangaza live mabunge mawili yaliyo sehemu tofauti kwa wakati mmoja!, hivyo EALA wakapeleka maombi kwa Mzee Mengi, wakakubaliwa!.
Kwa maoni yangu, licha ya TBC kulitangaza live Bunge la Katiba, bado TBC has the capacity kulitangaza live na Bunge la Afrika Mashariki kupitia Chaneli yake ya pili ya TBC 2, kwa sababu hata ITV wenyewe unaweza kukuta watalitangaza Bunge hili la Afrika Mashariki kupitia EATV ili kupunguza loss of revenue kama watatumia ITV kulitangaza Bunge hili, then watafuta vipindi vyote kwa siku zote hizo za bunge hilo, kitu ambacho I don't ni kitu rahisi!.
Hongera sana Mzee Reginald Mengi, Hongera vyombo vya habari vya IPP, Hongera ITV!,
Jee mtakubaliana na mimi kuwa sasa ITV ni zaidi ya TBC?!.
Wasalaam.
Pasco
====http://youtu.be/Skuo2Bk2VoA=========================
[video=youtube_share;Skuo2Bk2VoA]http://youtu.be/Skuo2Bk2VoA[/video]

Dr Reginald Mengi amesema ushirikiano wa Afrika mashariki uwe wa wananchi wa nchi wanachama
Mwenyekiti mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi amewataka wabunge wa bunge la Afrika mashiriki kuhahikisha kuwa ushirikiano wa Afrika mashariki hauwi wa viongozi pekee bali uwe wa wananchi wa nchi wanachama.
Mwenyekiti mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa chakula cha mchana alichowaandalia wabunge wa bunge la Afrika mashariki baada ya kutembelea vyombo vya habari vya IPP kushuhudia jinsi vinavyofanya kazi.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo spika wa bunge hilo Mhe. Dr. Margareth Ziwa ameviomba vyombo vya habari sema wabunge wa Afrika mashariki wanao kama wabunge wana majukumueliza mwenyekiti wa wabunge wa afrika mashariki kutoka tanzania Mhe. Adam Kimbisa ameomba vyombo vya habari vya ipp na tanzania kwa ujumla vifuatilie shughuli za bunge hilo litakalofanya vikao vyao kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam ili kuwawezesha wananchi kufahamu kinachojili bungeni humo.
Kamati ya uongozi ya bunge la Afrika mashariki imetembelea vyombo vya habari vya IPP na kujionena namna vinavyofanya kazi ambapo spika wa bunge hilo Mh Margret ziwa ameviomba vyombo hivyo kuripoti mkutano wa bunge hilo unaotarajiwa kuanza jumatano ya wiki ijayo jijini Dar es Salaam.
Ziara ya wabunge hao imeanzia katika ofisi za The Guardian ambapo walipokewa na mkurugenzi mtendaji bw kiondo mshana ambapo aliwatembeza katika maeneo mbalimbali ya kampuni hiyo na kuwapatia maelezo huku akiita ziara ya wabunge hao ni tukio la heshima kwa kampuni za ipp na nchi kwa jumla.
Baada ya kutembelea katika upande wa uchapishaji wa magazeti wabunge hao walitembelea vituo vya utangazani vya east african televisheni na redio, redio one na capital redio kisha itv na kupatiwa maelezzo kutoka kwa wakuu wa idara.
Mwenyekiti wa chapter ya Tanzania katika bunge hilo mh adamu kimbisa amesema umefika wakati kwa vyombo vya habari kufuatilia kwa kina mambo yanayofanywa katika bunge hilo kama kweli ipo nia ya dhati ya kuona jumuiya ya afrika mashariki inakuwa.
Kwa upande wake Mh spika amesema wao kama wabunge wanajukumu kubwa la kusimamia na kuweka mambo sawa japo wao kama binadamu kuna mambo yanaweza yasiwe sawa na hivyo ndio nafasi nzuri kwa vyombo vya habari kulisaidia bunge na jumuiya kwa ujumla kukua.