ITV kipima joto,mbona kila siku sura ni zile zile?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,171
144,737
Ukifuatilia kipindi hiki utagundua kuwa kuna baadhi ya sura zinazoonekana karibu kila kipindi.

Sura zinazoonekana kubadilika ni zile za meza kuu lakini kwa wachangiaji wengine utazani kuna watu fulani wana hati miliki na kipindi hiki.

Kama watu wengine hawajitokezi,je ITV mnachukua hatua gani kupata uwakilishi mpana zaidi?

Sometimes nahisi kuna watu wanajiandaa kugombea ubunge kwahiyo wanatumia kipindi hiki kujinadi na ndio maana kila siku wamo.

Kama kutakuwa kuna watu wanakosa nafasi ya kushiriki ili hali wengine karibu kila kipindi wapo,basi hapa patakuwa na tatizo, tofauti na hapo, nawaunga mkono hao wanaoshiriki karibu kila siku maana ndio wanaojitokeza na kufanikisha kipindi hicho.

Mnaojua ukweli tunaomba mtusaidie pengine mimi ndio sielewi.
 
Back
Top Bottom