Johnsecond
JF-Expert Member
- May 4, 2010
- 1,076
- 211
Wakati msomaji wa taarifa ya habari saa mbili usiku jana anasoma alisema hivi "Mengi amesema kuwa watanzania waige mfano wa rais kikwete katika kuchukia umaskini" wakati najiandaa kumuondoa Mengi kwenye list yangu ya watu ambao niliwaamini angalau kidogo, mengi akawekwa hewani hakusema kitu chochote wala kutaja jina la kikwete na aliongelea kitu tofauti kabisa. Hivi hili hawa ITV hamkuliona wakati mnaandaa taarifa ya habari??? Taarifa ya habari hata sisi ambao sio professionals wa habari tunaweza kuwafundisha, wasomaji wa taarifa ya habari huwa hawana mvuto, wamenuna, wanamawazo mengi mpaka wanakosea kosea. Waigeni TBC japo wanaripoti utumbo lakini wanatabasamu hata kidogo . . .