ITV ina mpango wa kuyumbisha uamuzi wa Tendwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ITV ina mpango wa kuyumbisha uamuzi wa Tendwa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Sep 2, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]Wana-JF:[/FONT]

  [FONT=&quot]Kesho (Ijumaa), kituo cha televisheni cha ITV katika kipindi chake cha Kipima Joto saa 3 usiku, mada kuu itakuwa ni Sheria ya Matumizi ya Fedha katika kampeni iliyotiwa saini na JK April mwaka huu. [/FONT]

  [FONT=&quot]Ni sheria ambayo tayari imeanza kuwekwa majaribuni na iwapo makali yake au la yanaweza kujulikana wiki ijayo kutokana na maamuzi ya Msajili wa Vyama katika pingamizi la Chadema dhidi ya JK.[/FONT]

  [FONT=&quot]Mimi sipingi kwa ITV kufanya mjadala huo ambao wananchi pia wamearifiwa kuchangia kwa simu, ila nina wasiwasi wa timing ya kipindi hicho wakati huu ambapo maamuzi ya Tendwa yanasubiriwa.[/FONT]

  [FONT=&quot]Sote tumeshajua ule upande ITV unaegemea katika kampeni hizi (CCM) na hofu yangu ni kwamba pengine kipindi hicho kimeandaliwa maalum katika ku-influence maamuzi ya Msajili wa Vyama katika pingamizi hilo la kihistoiria.[/FONT]

  [FONT=&quot]Nina maana hapa ingawa mada ni Sheria hiyo yote kwa ujumla, lakini ni dhahihiri watakaojadili hawataacha kutia mkazo katika hilo pingamizi. Hivyo watoa mada wanaweza kuwa wameandaliwa ili ku-influence uamuzi. Hawa ni pamoja na wale "watakaopiga simu."[/FONT]

  [FONT=&quot]Ingefaa kipindi hiki kingeahirishwa hadi baada ya ruling ya Tendwa.[/FONT]
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,964
  Trophy Points: 280
  Marksman una akili sana kwa kuona kitu kama hicho kuwa kinakuja, ni kweli unavyosema vipindi kama hivi vya kabla ya tukio fulani huwa vina influence fulani kwenye maamuzi hasa ya kisheria.

  Ila kwa nchi kama yetu ambayo si democractic kitu hicho huwa hakipo kwa vile tayari maamuzi huwa yameshafikiwa. Kwa mfano suala hili la pingamizi lilivyo ni dhahiri wengi kama siyo wote tunajua nini ambacho Tendwa ataongea ndiyo maana hata Chadema siku ya kwanza walitoa caution kama hiyo.

  ITV na vyombo vya IPP wanajulikana kwa umangimeza, utakumbuka hata uchaguzi wa 1995 sikumoja kabla ya kupiga kura walituwekea picha za mapigano ya Rwanda, kwa hiyo sioni ajabu ila waelewe kwamba hata waandishi wa habari waliokuwa wana engineer vita vya Rwanda wakati huu wanajuta magerezani.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kwani namba ya hicho kipindi chao kikiwa hewani ni ngapi au nizungumze na nani ili na mimi niwe mgeni wa kutoa mawazo yangu?
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,053
  Likes Received: 3,962
  Trophy Points: 280
  Kwanza ITV (CCM) wanaweza wasirushe watu hewani live yaani wa-filter kwanza "matusi"! tena kwa mtindo huu wa kujisajili namba wanaweza kukutafuta baadae UWT! heheheh Uhuru wa kujieleza huo!
   
 5. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jamani mwenye namba ya kipindi hicho atupatie kabla ya hiyo kesho ili tuweze kujianda na maswali yetu... Maana wanaweza waka waanda watu wao... MM nikipata nitakutumia kwa SMS
   
 7. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ili nalo linawezekana kabisa endapo watataka kufanya usanii
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kipima joto, kina mahojiano siku hizi?
   
 9. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,200
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Ooh my God... Freemasons in the battle once again. Haven help our nation!!
   
 10. K

  KIFARU BOMOA Member

  #10
  Sep 2, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama wao CCM watakua wamearifiwa kuchangia hoja kwa simu na nyinyi mnangoja nini kuchangia hoja zenu kwa kuisaidia chadema? Mmekalia chuki tu, siasa zenyewe hamzijui. Mimi ningewashauri kuelimisha umma juu ya KILIMO KWANZA, na kuachana na mambo ya siasa. Naimekuaje leo hii ITV inaegemea upande wa CCM wakati IPP na ITV na CHADEMA wanakula sahani moja? Na kuhusu pingamizi hilo ni la kawaida tu, pingamizi nyingi zimeshakuja kwa CCM na si za msingi, itakuaje pingamizi hilo liwe la kihistoria? Usiwe na hofu kaka. CCM ni chama makini, na imepita kwenye mambo mengi, CCM nambari 1!!!!!!
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  We ni mgeni hapa na ni mgeni wa siasa naomba usichangie pumba hapa badala yake kaa pembeni soma mijadla ya great thinkers na ujifunze. Baada ya mwaka rudi uchangie utakuwa umeshajifunza.
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Namba hutolewa wakati wa kipindi kikiwa hewani. wataonesha kwenye kioo cha TV yako shekhe. wala usihangaike kuitafuta mda huu maana wanaweza hata kubadili namba wale.
   
 13. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  ITV(ccm) wamezidi kwa uzandinki

  Kuna watu wataojiwa bila ya kupiga simu na watu hao wameandaliwa
  upigaji wa simu unaweza kuwa controlled mana wapigaji simu watakuwa wanajulikana
   
 14. R

  Ramos JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama watakaokuwepo ni watu aina ya Palamagamba Sibudi, ntajua kabisa kimeandaliwa kuibeba CCM...
   
 15. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama kipindi hicho kweli kitaruhusu watu kupiga simu na kutoa maoni yao, ni vyema kujiandaa kwa kuisoma na kuielewa sheria hiyo kipengele kwa kipengele.

  Naishauri CHADEMA ichukue hatua za kulinda haki yake ya kimsingi ili kipindi hicho isitumike kubadilisha maamuzi ya Msajili wa vyama vya siasa. Njia ninazopendekeza ni:

  1. Kuandaa wanasheria watakaokitathmini kipindi hicho ili kama kikikuika misingi ya sheria ITV ichukuliwe hatua
  2. Kujiandaa wenyewe kwa kuwa na watu watakaopiga simu na kutoa maoni yenye ufafanuzi wa kina
  3. Kuhakikisha kuwa madhara yoyote yanayoweza kutokea kutokana na kurushwa kwa kipindi hicho yanafanyiwa kazi, ili kuzua kupotea kwa haki
  Itakuwa busara na haki kwa watanzania kama ITV itaheshimu haki za watu wote na kuepuka kupotosha sheria kadiri inavyowezekana. Njia ya kuhakikisha hilo, ni kutumia wanasheria mahiri wasio na upendeleo kwa upande wowote. Kama ikiwezekana, Mabere Marando na Tundu Lissu pia waalikwe ili ku-balance mjadala.

  Ni ushauri tu.
   
Loading...