ITV ahsanteni kwa kutupa coverage nzima ya kumbukumbu ya kifo cha Mw. Nyerere

Kwa kweli mmefanya jambo jema sana maana kuna watu hawakuona tukio zima mwaka 1999
pamoja nakulia kipindi kiima lakini ni jambo la heri kuweka kumbukumbu hii. na hakika hata wale ambao hawakushuhudia wameshuhudia kipeni cha wengi alivyoliliwa. ile siku ilikuwa ya ajabu.itv fanyeni mpango mtuuie hiyo kandaili tuwawekee vitukuu vyetu kumbukumbu ya kiongoi shujaa wa tanxania, afrika na dunia kwa ujumla.
 
Ni kweli ITV nawapongeza sana jinsi walivyoitendea haki siku ya kumbukumbu ya Mwalimu.

Jana kuna mazungumzo ya Mwalimu na waandishi wa habari aliyafanya yalinishangaza sana na kwa kweli huyu bwana alikua Mwalimu kweli kweli.

Akizungumzia kuhusu umuhimu wa katiba na kuheshimu katiba na akasema yeyote atakaeichezea katiba asiachwe hivi hivi. Hasa hasa lilikua ni suala la zanzibar kujiunga na OIC.

Akasema kama viongozi wanavunja katiba tusiwaache hivi hivi tuwapinge na kuwakemea na tuhakikishe hatua zinachukuliwa kurekebisha kadhia hiyo katika nchi na wahusika wachukuliwe hatua. Akasema hata wakiwa wakali na hawataki kuambiwa ukweli tusiogope, akasema kama wakiwa wakali na tukaogopa kuwakemea basi kuna siku moja tutakuja kutawaliwa na kiongozi ambae ni dikteta ambae atafanya mambo yake tu na kupuuza katiba. Nilishangaa sana huyu mzee kuyaona haya mambo miaka mingi iliyopita utafikiri aliisha maisha ya mbele kabla yetu na kuona kinacho kuja na ndio maana akatuasa namna hilo.

Asante sana Mwalimu kwa uzalendo huo wa nchi yako kipenzi Tanzania.
 
Maneno ya Mwalimu Nyerere yanaishi hadi leo tumeweza kuyashuhudia
 
Mwalimu alikuwa Jabari. Ameiongoza tanzania kwa miaka 24 akitegemea kilimo tu kuendelea uchumi na kuhudumia huduma zote za kijazi Ikiwemo ujenzi wa viwanda, uendeshaji na usimamizi wa reli TRC na Tazara, Air Tanzania, Meli baharini na maziwani, shule na vyuo na hospital. Kutoa pembejeo kwa wakulima n.k. Bado aliweza kuendesha vita vya ukombozi kusini mwa africa.

Mwalimu amejenga nchi ya UMOJA wa kitaifa yenyewe kutumia luggage moja na kupunguza ubaguzi wa kidin na kikabila ndani ya Muungano kati ya tanganyika na Zanzibar.

Kwa ufupi tanzania ya leo inafursa nyingi zaidi Ikiwemo uchumi wa Madini, Utalii, Biashara, Kilimo, Gas na Mafuta lakini bado inajishindwa na imebaki Kumalizia Yale yaliyofanywa na awamu ya Kwanza.

Naamini Mhe Magufuli ameanza kuonyesha njia kama nchi kusimamia rasilimali zetu ili tujenge na kuimarisha uchumi wa taifa letu na kupiga hatua zaidi za kimaendeleo.

Hongera Mwl NYERERE na Serikali yote ya awamu ya Kwanza.
 
Back
Top Bottom