Itungwe Sheria upesi Timu Kubwa inayocheza Mechi ya Ligi Kuu Uwanja wa Mkapa Mkapa Usiku ikishinda Goli 1 tu isiruhusiwe Kuutumia tena

KEROZENE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
6,119
2,000
Ni aibu Kubwa Timu imetumia karibia Tsh Bilioni 1 za Kitanzania Kusajili Wachezaji wakubwa kisha wakichexa Uwanja mzuri wa Benjamin Mkapa wanashinda Kagoli Kamoja tu.

Mnatusumbua kuja Kuwatizama halafu mnawatia tu Hasara Serikali kwa Kutumia Umeme wao kwa Mpira mbovu na wenye Kagoli Kamoja tu wakati kuna Timu nyingine Bora, Kubwa na iliyobarikiwa na Mungu ingebahatika kucheza na Migodi Usukumani FC jana ingeshinda Magoli 9 au 13.

Haingii Akilini Mchezaji ambaye Jumamosi Mbili zilizopita ametoka Kufunga Goli Gumu ( lililosaidiwa na Mganga wa Kienyeji aliyejificha Vyumbani kwa Mkapa Stadium ) leo hii Kanda ya Ziwa na Temeke Dar es Salaam anakosa Magoli ya wazi na mepesi ambayo hata Mimi Mightier ( japo ni Veterani ) ila nikiwa nacheza Leaders Club, Fire na Ubungo kila Weekend na akina Bakari Malima ( Jembe Ulaya ) huwa nafunga hadi natamani hata nirejee Ujanani na nikachukue namba ya Mtu huku Khalid Aucho akinisetia tu na Miauta yake na Pasi zake za Upendo.
 

dem boy

JF-Expert Member
Nov 4, 2016
4,210
2,000
Umesema kweli,siku ile ile Yanga ilipoifunga Simba goli moja tu ilitakiwa ipigwe marufu kuutumia uwanja wa mkapa....mtu unakutana na kigoli kibichi kabisa badala ya kukipelekea moto kisawa sawa we unakipiga moja chali.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom