It's always a good idea to have 2nd and even 3rd opinion

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Posted Date::12/15/2007
Mwanamke atumia ARV miaka tisa bila UKIMWI

Alipwa fidia Sh 2.6 bilioni

BOSTON, Marekani
Mwananchi

MWANAMKE mmoja, Audrey Serrano amelipwa fidia ya Dola za Marekani milioni 2.5 (zaidi ya Sh 2.6 bilioni za Tanzania) kutokana na makosa ya madaktari yaliyoonyesha kuwa ana virusi vya ukimwi na kutumia dawa kwa miaka tisa wakati hakuwa ameambukizwa.

Jumatano ya wiki hii mahakama ya Worcester Superior jijini Boston, Marekani ilimwamuru daktari aliyempima na kutoa dawa hizo mama huyo, kumlipa kiasi hicho cha fedha.

Mwanamke huyo amekuwa akiishi kwa miaka tisa akijua ameambukizwa virusi vya ukimwi kabla hajapima tena na kujikuta hana virusi vya ukimwi na hivyo kumfungulia mashtaka daktari huyo.

Katika kesi yake ya madai mwanamke huyo alisema kuwa, amepata madhara makubwa mwilini mwake kufuatia kutumia mchanganyiko wa dawa za kuongeza siku, ikiwemo kuvimba tumbo, kupungua uzito, msongo na uchovu wa mwili.

Alifafanua kuwa alipungua uzito kutokana na wasiwasi kuwa muda wowote anaweza kufariki kutokana na kuugua ugonjwa wa ukimwi.

Wakili wa mwanamke huyo, David Angueira aliieleza mahakama kuwa makosa hayo ya kitabibu hakuwahi kuyaona na daktari aliyemhudumia mteja wake alimpa mgonjwa dawa kwa kuangalia historia yake badala ya kujali vipimo.

Wakati wa kesi, mshtakiwa, Dk Kwan Lai, alijitetea kuwa mama huyo alipofika kupima alimueleza kuwa aliwahi kujihusiha na ukahaba, mumewe alikufa kwa ukimwi na kwamba alikuwa anaumwa kifua, ambacho kinahusishwa na ukiwmi.

Hata hivyo, mwanamke huyo alikana kuwahi kujihusiaha na ukahaba lakini akakiri kuwa bwana wake alikuwa na virusi vya ukimwi. Pia alikana kumueleza daktari kuwa alikuwa anaumwa kifua.

Mwaka 2003 mwanamke huyo alipima virusi vya ukimwi baada ya mpenzi wake kufariki kutokana na ugonjwa huo mwaka 1994.

Ninakwenda kumalizi masomo yangu na nitaendelea kuwasaidia watu wengine, Serrano alilieambia Shirika la Habari la AP kwa njia ya simu na kufafanua kuwa atamtafuta daktari mwingine wa kumsaidia.

Mama huyo alikuwa akiugua ugonjwa wa kifua na hivyo kulazimika kupima virusi vya ukimwi Januari 4, 2004 na majibu yalipotoka yalionyesha kuwa ameathirika kwa ugonjwa huo.

Aidha wakili wa mwanamke huyo alidai fidia ya dola za Marekani 3.7 milioni ikiwa ni pamoja na fidia ya usumbufu alioupata mwanamke huyo kutoka kwa jamii, lakini mahakama ikaidhinisha Dola 2.5 milioni.
 
Back
Top Bottom