Wanabodi hakuna jambo lolote linalohusu masuala ya kifedha linalofanyika wilayani Itilima bila kuwa na harufu ya upigaji, tangu watu wamalize uandikishaji hawajapewa fedha yao, ukiwauliza wanakuambia wanasubiri mwongozo toka tamisemi. Aisee oneni aibu basi mbona wilaya nyingine wamepewa?
UPDATE :
mpaka Muda huu wilaya ya Itilima haijalipa waandikishaji wake wa wapiga kura tangu zoezi liishe tar. 17/10/2019 wakiulizwa wanasema mfumo wa malipo unasumbua, yaani kweli huo mfumo wa malipo unasumbua wilayani Itilima tu??? Mamlaka zinazohusika tunaomba wachukue hatua katika hili kabla watu hawajaandamana jumatatu tar 28/10/2019 kuelekea ofisi za halmashauri ya wilaya kudai chao, hii itakuwa ni aibu kubwa!!