Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Kuna watu ukiwashukuru kwa kusema "asante" wanasema "karibu". Bila ya shaka hawa wanatafsiri kutoka Kiingereza pale mtu anaposema "thank you" na anajibiwa "you are welcome". Lakini kuna wengine wakishukuriwa hivyo wanasema "asante kushukuru" na hawa mara inaonekana wanatafsiri ile ya Kisukuma ambapo mtu akisema "wabeja" anajibiwa "wajeba kulumba".
Binafsi naamini jibu la asante ni hilo la Kisukuma na siyo "karibu". Waingereza walipokuwa wanasema "you are welcome" watu wengi hawajui kuwa walikuwa wanasema "you are welcome to say thanks" ni sawa na kusema "It is good for you to say thanks". Sasa kwa Kiswahili mtu anaposema "Karibu" anajaribu kusema hicho hicho cha Kiingereza "Unakaribishwa kushukuru"; "ni vizuri kushukuru" n.k
Ni kwa sababu hiyo naamini kusema "asante kushukuru" inasema hasa mwitikio wa yule anayeshukuriwa; yeye mwenyewe anashukuru kwa mtu kumshukuru. Kwamba amepata kheri ya kuona kuwa amestahili shukrani. Hivyo akisema "asante kushukuru" anaeleza zaidi hisia zake kama mwitiko wa 'asante' kuliko akisema "karibu" tu kwani 'karibu" ina maana ya kumwita mtu kujongea jirani kuliko kuonesha hisia ya kufurahia shukrani iliyotolewa.
Mtu akikushuru mwambie "asante kushukuru" siyo "karibu"
Kwa sababu ukisema "karibu" na yeye akisema "asante" na wewe utasema "karibu"......halafu ikawa jioni ikawa asubuhi...
Hoja..!!