Itikio la "Asante" siyo "karibu"

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Kuna watu ukiwashukuru kwa kusema "asante" wanasema "karibu". Bila ya shaka hawa wanatafsiri kutoka Kiingereza pale mtu anaposema "thank you" na anajibiwa "you are welcome". Lakini kuna wengine wakishukuriwa hivyo wanasema "asante kushukuru" na hawa mara inaonekana wanatafsiri ile ya Kisukuma ambapo mtu akisema "wabeja" anajibiwa "wajeba kulumba".

Binafsi naamini jibu la asante ni hilo la Kisukuma na siyo "karibu". Waingereza walipokuwa wanasema "you are welcome" watu wengi hawajui kuwa walikuwa wanasema "you are welcome to say thanks" ni sawa na kusema "It is good for you to say thanks". Sasa kwa Kiswahili mtu anaposema "Karibu" anajaribu kusema hicho hicho cha Kiingereza "Unakaribishwa kushukuru"; "ni vizuri kushukuru" n.k

Ni kwa sababu hiyo naamini kusema "asante kushukuru" inasema hasa mwitikio wa yule anayeshukuriwa; yeye mwenyewe anashukuru kwa mtu kumshukuru. Kwamba amepata kheri ya kuona kuwa amestahili shukrani. Hivyo akisema "asante kushukuru" anaeleza zaidi hisia zake kama mwitiko wa 'asante' kuliko akisema "karibu" tu kwani 'karibu" ina maana ya kumwita mtu kujongea jirani kuliko kuonesha hisia ya kufurahia shukrani iliyotolewa.

Mtu akikushuru mwambie "asante kushukuru" siyo "karibu"

Kwa sababu ukisema "karibu" na yeye akisema "asante" na wewe utasema "karibu"......halafu ikawa jioni ikawa asubuhi...

Hoja..!!
 
Asante kushukuru ni sahihi
na wala haikuanzia kwa wasukuma
hata watu wa Zanzibar na pwani walikuwa wanatumia hii kwa miaka mingi tu
 
Asante kushukuru ni sahihi
na wala haikuanzia kwa wasukuma
hata watu wa Zanzibar na pwani walikuwa wanatumia hii kwa miaka mingi tu

Mi nimeshangaa hata kwa Wanyasa. Nimekuwa na Wanyasa kadhaa pia wao wanasema hivyo. Hasa sijui wanaiga kwa watu wa huku au nao ni namna yao.
 
Mi nimeshangaa hata kwa Wanyasa. Nimekuwa na Wanyasa kadhaa pia wao wanasema hivyo. Hasa sijui wanaiga kwa watu wa huku au nao ni namna yao.

Itakuwa ya kwao pia
waafrika ni kawaida hii kujibu hivyo
Mwanakijiji ni msukuma anajifagilia tu
 
Asante kushukuru ni sahihi
na wala haikuanzia kwa wasukuma
hata watu wa Zanzibar na pwani walikuwa wanatumia hii kwa miaka mingi tu
hata mimi nakubali halikuanzia huko usukumani.....
hata mimi wakati nipo kijijini kwetu kule Peramiho, enzi hizo sijawahi kutoka kwenda sehemu nyingine yoyote, na hata waliokuwa wamenizunguka pia walikuwa hawajatoka, nilikuwa najua jibu la asante ni asante kushukuru.........
 
Karibu aisee
upoo?
 
Mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmm!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom