Mzalendo wa ukweli
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 559
- 149
Ukitazama kwa umakini alama zilizopo katika bendera ya CCM utagundua kuna alama ya jembe na nyundo; jembe likiwakilisha wananchi wakulima na nyundo ikiwakilisha wafanyakazi. Hii ilikuwa na maana kuwa CCM kilikuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi wakati kinaanzishwa. Kilijikita katikk kutetea haki za wafanyakazi na wakulima kwa ujumla. Na kwa kipindi hiki itikadi/ideology kuu ya chama ilikwa ni siasa ya ujamaa na kujitegemea.
Swali langu kwa sasa ni kuwa kwa sasa itikadi ya chama hiki kwa uwazi kabisa ni ipi? Je ni chama cha wafanyakazi na wakulima bado au ni cha kibepari zaidi?
Swali langu kwa sasa ni kuwa kwa sasa itikadi ya chama hiki kwa uwazi kabisa ni ipi? Je ni chama cha wafanyakazi na wakulima bado au ni cha kibepari zaidi?