Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,550
- 46,090
Jana ulizuka mjadala kuhusu katazo la Spika kwa wabunge kutokuvaa tai nyekundu wakati Rais akiwa bungeni leo. Watetezi wa katazo hilo walisema ni suala la Itifaki.
Jambo jingine ambalo niliwahi kuambiwa ni Itifaki ni kwamba mtu mwingine hatakiwi kuongea na hadhira baada ya Rais kumaliza kuongea na hadhira hiyo na yeye akiwepo bado katika hadhira hiyo.
Muda wote niliamini inaweza kuwa kweli ni Itifaki mpaka leo nilipoona kuna mazungumzo mengine marefu kutoka kwa mbunge na Spika baada ya Rais kumaliza hotuba yake.
Je ni sahihi kiitifaki kwa jambo hilo lilofanyika leo bungeni?