Itifaki imekaaje? Makamu wa rais kuingia uwanjani kabla ya waziri mkuu!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,593
36,012
Pengine watu wa itifaki mngetusaidia hili! Au ndo mwendelezo wa nchi yetu kupuuza puuza tu mambo kama wanavyoipuuza katiba ya nchi!

Leo Zanzibar wakati wa viongozi wakuu kuingia kwa kiitifaki uwanjani wakati wa sherehe za 'mapinduzi yao' ndipo makamu wa rais akatangulia kuingia kisha waziri mkuu akafuata kabla ya Magufuli na Shein wa mwisho!

Hili linaweza kuibua maswali hasa ikizingatiwa kuwa makamu wa rais ni jinsia yake! Au labda lipo lingine la zaidi? Anyway mnaweza kutujuza!
 
Kwani ITIFAKI NI NINI NA IMEWEKWA NA NANI KWA AJILI YA NANI???

Ukijibu HAYO maswali ntakuelewesha vizuri na utaelewa.
 
Pengine watu wa itifaki mngetusaidia hili! Au ndo mwendelezo wa nchi yetu kupuuza puuza tu mambo kama wanavyoipuuza katiba ya nchi!

Leo Zanzibar wakati wa viongozi wakuu kuingia kwa kiitifaki uwanjani wakati wa sherehe za 'mapinduzi yao' ndipo makamu wa rais akatangulia kuingia kisha waziri mkuu akafuata kabla ya Magufuli na Shein wa mwisho!

Hili linaweza kuibua maswali hasa ikizingatiwa kuwa makamu wa rais ni jinsia yake! Au labda lipo lingine la zaidi? Anyway mnaweza kutujuza!
Protokali ya bara ni tofauti na potokali ya Zenj.

Mfano muungano wetu ni union, yenye seikali mbili, rais wa JMT ndio overall akifuatiwa na VP kisha PM, ndipo anafuata rais wa Zanzibar na wale makamo wake wawili. Hata kwenye katiba, katiba ya JMT ndio supreme, na katiba nyingine zote zinafuatia!. Ki nchi, Tanzania pekee ndio nchi, Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT.

Lakini kwenye maadhimisho, kule Zanzibar, rais wa Zanzibar ambayo sio nchi, ndie top, chini yake anakuja rais wa JMT, VP, PM, wale makamo wao wawili.

Leo nilikuwa naangalia maadhimisho kule Zanzibar, kiukweli protokali ilikuwa sifuri!. Kikawaida baada ya wale viongozi wakuu wa nchi, na wastaafu wao, walitakiwa kufuata viongozi wa mihimili ya dola, kisha viongozi wa vyombo vya dola, kule nimeshuhudia Spika wa BLW akitangulia, kisha CDF, ndipo akafuatiwa na Spika wetu!. Hii inamaanisha maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar sio sherehe ya kitaifa, bali ni sherehe ya kijitaifa cha Zanzibar. Viongozi rasmi wa JMT ni rais, makamo na wazii mkuu, ila kwa Zanziba, wazii mkuu is nothing kwao, kama alivyo rais wa Zanzibar is nothing kwenye setup ya muungano bali heshima tuu!. Tena katiba ya JMT haiwatambui kabisa wale makamo wawili wa Zanzibar mpaka kesho, tunawaacomodate huku baa kiheshima tuu, but they are nothing!.

Pasco
 
Mkuu mimi mwenyewe ile cjaielewa kabisa na hii ya magufuli kuingia kabla ya shein
 
Muungano wa nchi 2 zenye marais 2 zenye amiri jeshi 2, na bado misisiemu inatuaminisha kilichopo ni sahihi wala hakuna kasoro.Hili ni lijipu na Magufuli hawezi kuliacha kamwe namwaminia analitafutia taiming nzuri tu,eidha twende kwenye serikali 1 au 3.
 
Vipi wale wabunge vihelehe wa Bunge la katiba ,waliokuwa wanasema,katiba CHAKACHUZI imewajali wanawake na Wazanzibar?
 
Leo nimeona Wanajeshi wakila kiapo cha utii kwa Raisi wa Zanzibar, wakimalizia kwa kusema himaaa himaaa Zanzibaaaaa
Na amri za kigwaride kwa kijerumani
Nimeshangazwa sana
Nadhani utakuwa umechanganya kati ya wale migambo wa JKU na KMKM, na sio JWTZ!. JW walikuwa pale kwa ajili ya Amiri Jeshi Mkuu na sio kwa ajili ya rais wa ule mkoa wa kisheshi wa Zanzibar!.

Pasco
 
Nadhani utakuwa umechanganya kati ya wale migambo wa JKU na KMKM, na sio JWTZ!. JW walikuwa pale kwa ajili ya Amiri Jeshi Mkuu na sio kwa ajili ya rais wa ule mkoa wa kisheshi wa Zanzibar!.

Pasco
Duh, mkuu unaichukia znz na hiki kimuungano kama mimi!? Nashukuru kama tupo wengi
 
Back
Top Bottom