Itatokea nini kama 'SIMBA' akiwala na kuwamaliza wanyama wote porini? Madhara ya CCM vs CCM

winnerian

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
335
530
Ikiwa bunge lijalo ni la CCM tupu na limetokana na kuua wapinzani wote porini (Tanzania) haya ndio madhara yanayoenda kutokea ambayo wayajuao ni wachache.

1. Wananchi kukosa wawakilishi wao bungeni. Wawakilishi kwa maaana ya watetezi wao, kwasababu wote waliopita kupitia CCM hawana ubavu au kujiamini kufanya/kusema kinyume na serikali kwasababu ndio iliyowawekea kifua wakapita bila kujali matokeo ya kura halisi za wahanchi. Kile kitaakacho amuliwa na serikali (Raisi na baraza la mawaziri ambao kimsingi ni watu wachache ambao ni mawaziri 21 na raisi 1 jumla watu 22) basi kitapitishwa bila kupingwa na bila kujali maslahi ya Taifa la Tanzania, Chama kwanza Taifa baadae.

2. CCM hii itajipanga kuwaridhisha wananchi kwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ili kurudisha imani na upendo wa chama kwa wananchi. PESA ZA KUTEKELEZA MIRADI HII HAZIPO NA HAZITAKUWEPO kwasababu uchumi wetu bado ni mdogo kuweza kufanya mambo makubwa kwa mkupuo, hivyo CCM hii ya 2020 - 2025 inaenda kukopa kupita uwezo wa nchi wa kukopesheka. Italazimika ikope kutoka China kwa kisingizio cha masharti nafuu. Huu mkopo utakua ni muendelezo wa mkopo wa ccm ya 2015 - 2020. Kutokana na haya yote Taifa la Tanzania litaingia katika kundi la nchi zenye mkopo mkubwa na itafikia hatua nchi haitaweza kukopesheka tena na hii itasababisha mfumuko wa bei kupanda kwa gharama za maisha pamoja na serikali zijazo (2025 na kuendelea) kushindwa kutekeleza majukumu yake jambo ambalo litapeleka watakao kuja kutawala mbeleni wafikirie kuuza kipande cha nchi kwa makoloni husasani China. China itatuwala kibishara na hatimae hatakuwa na namna nyingine zaidi ya kutii masharti yao magumu na gandamizi kuliko tunavyodhania.

Madhara ya masharti nafuu ni pamoja na kuruhusu zabuni zote nyeti (zile ambazo zimetengewa fungu kubwa kupewa wazabuni wa wakichina. Mfano zabuni za ujenzi wa barabara hili hali serikali ikijitetea wazabuni wa ndani hawana uwezo na ni wababaishaji); Zipo zabuni nyingi nyeti na kubwa ambazo kama zingalipewa wazawa/watanzania halisi basi kiasi kikubwa cha fedha kingelibaki hapa ndani kufanya mzungoko wa pesa kuwa mkubwa, hili nalo halitakea kwakua hakuna wa kwenda kulisemea hili katika bunge lijalo.

3. Sheria nyingi kandamizi kwa wananchi wa Tanzania zinaenda kupitishwa bila kupingwa wala kujadiliwa. Watakaopitisha sheria hizi ni wabunge wa CCM ambao hawakuchaguliwa na wananchi bali wamepitishwa kwa ubavu wa serikali. Madhara ya sheria kandamizi kwa wananchi ni pamoja na kudumaza uchumi wa wananchi huku serikali ikizidi kujilimbikizia ukwasi na kudumaza wananchi wake. Tusahau kabisa habari ya kuzalisha matajiri wazawa kwakua sera zetu hazihungi mkono juhudi za mtu binafsi.

4. Rushwa inaenda kuongezeka mara dufu zaidi kuwahi kutokea. Mfano ukapewa tender mahali labda ya ujenzi wa nyumba halafu aliyekupa ile tender akukabidhi pesa zote tuseme taslimu milioni mia nane (800,000,000.00), kisha aondoke zake bila kurudi wala kujali ujenzi unaendeleaje; jiulize mwenyewe nini kitakachotokea. Majibu yangu katika hili, bila usimamizi madhubuti utajengewa nyumba ya chini ya viwango kwasababu utawekewa vifaa na material dhaifu mnoo ili kusave pesa nyingi iwezakanvyo kwa yule uliempa tender. Kwahivyo katika serikali ya 2020 - 2015 rushwa itatawala sana maana Raisi hawezi kuwa na macho kila kona kila sehemu na kila idara.

5. Kwa ujumla wa mambo yote yaliyosemwa hapo juu, Tanzania kama Taifa litazidi kuwa na wananchi wenye akili za kushikiwa na wasio jiamini katika lolote katika haya yafuatayo.

a) Kiuchumi wananchi watazidi kudidimia - Mfano Taifa halitazilisha matajiri (Billionares) wazawa, badala yake wazo potoful la kutegemea majizi na manyonyaji kwa jina la wawekezaji litazidi kudumishwa na kukumbatiwa.

b) Wananchi wa Tanzania watabaki kuitwa na kuaminishwa wao ni wanyonge na maskini kama ambavyo Raisi ameendelea kuwaita mara kadhaa katika mikutano ya adhara.

c) Wanafakia wakubwa wa uchimi na miundo mbinu yetu watazidi kuwa wachina kwasababu wao ndio watakaozidi kufanya biashara kubwa katika Taifa letu na wao ndio watakaozidi kupata zabuni kubwa kubwa hilii hali wananchi wa Tanzania wakibakia kama vibarua na waajiriwa kwa wachina.

d) Taifa litazidi kugawanyika na kupata mpasuko wa kiitikadi, uchama na udini. Yameshaanza kuonekana kwa uchache ikiwa ni kwa mfano wa wale Mashekhe wawili, maneo ya Raisi kwamba msipo mchagua wa ccm basi hamtapata maendeleo, ukanda n.k.

Kwasasa kama muandishi wa makala hii sioni ni wapi suluhisho litatoka kwasababu watanzania wengi hawana uelewa wa mambo haya kutokana na mfumo wa CCM kuendelea kuwalea na kuwakuza watanzania katika mfumo gandamizi kimawazo na kifikra kwamba mawazo ya mwenyeketi ya dumu, kidumu CCM na mambo yafananayo na haya. Kwa ujumla itachukua muda mrefu kwa watanzania kupata uelewa mpana juu ya taif lao na itakuwa ni too late.

Nimalizie kwa kusema "Fisi wakikosa mizoga porini, hulana wenyewe"
 
Naiona tz kama ulaya miaka 5 inayokuja
Uwezakano huo upo lakini binadamu tumeumbwa na tamaa pamoja na ubinafsi. Ukiwa peke yako mahali utajilia vinono kwanza kisha mabaki utawaachia wengine wayakute. Elewa hata hili.
 
Ngoja tutulize akili kwanza.... Rais akisha apishwa tutajua tu njia gani tutapita.... Mbona sgr tulikwepa, kuhusu hao wabunge wala wasikutishe.... Magufuli ni yule yule.. Akuna mtu atakula rushwa afu tutamuacha tu, hata akiwa spika... Au general wa jeshi tutamfukuza sana.... Hata kwenye chama tutamfukuza
 
Yaache yauane tu. Tangu lini maccm yakawa na faida kwa Taifa? Yapo siku zote kwa ajili ya maslahi yao tu wenyewe, familia zao na marafiki wao.
 
Ngoja tutulize akili kwanza.... Rais akisha apishwa tutajua tu njia gani tutapita.... Mbona sgr tulikwepa, kuhusu hao wabunge wala wasikutishe.... Magufuli ni yule yule.. Akuna mtu atakula rushwa afu tutamuacha tu, hata akiwa spika... Au general wa jeshi tutamfukuza sana.... Hata kwenye chama tutamfukuza
Haya ndio mawazo ya watanzania IITA (Inteligent Immature Tanzanian Adult), ambapo kwa ujumla wao wanafanya zaidi ya 89.90% kwasasa. Unaweza kuona ni kwa jinsi gani Taifa bado lipo gizani.
 
Adui namba moja wa taifa letu sio umasikini, maradhi wala ujinga kama baba wa taifa alivyosema ila adui namba moja wa taifa letu ni MWANACHAMA HAI au MFU WA CCM

Chukua hili kutoka kwangu
 
Adui namba moja wa taifa letu sio umasikini, maradhi wala ujinga kama baba wa taifa alivyosema ila adui namba moja wa taifa letu ni MWANACHAMA HAI au MFU WA CCM

Chukua hili kutoka kwangu
Na hii inatokana na mfumo wake wa kuzidi kuamini katika dhana ya kuwafanya wananchi wake maskini, wanyonge, wasiojiamini katika kujieleza, kuogopa kupoteza dola na mambo yafananayo na hayo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom