Itambue wilaya ya Ileje na fursa zilizopo

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
279
1,000
ITAMBUE WILAYA YA ILEJE NA FURSA ZILIZOPO.

Na Elius Ndabila.
0768239284

UTANGULIZI.
Wilaya ya Ileje inapatikana katika Mkoa wa Songwe, mkoa ambao ni matokeo baada ya kuugawa mkoa wa Mbeya. Wilaya ya Ileje ni kati ya Wilaya nne zinazounda mkoa wa Songwe ambazo ni Momba, Mbozi, Songwe na Ileje yenyewe. Wilaya ya Ileje inakadiliwa kuwa na watu zaidi ya 150000. Wilaya ya Ileje ina kanda tatu kijiografia ambazo ambazo zinatofautiana kiuoto. Kanda hizo ni ukanda wa Umalila ambao unaundwa na kata za Ibaba na Itale. Ukanda wa Undali unaunganishwa na kata za Ngulilo, Luswisi, Lubanda, Sange, Ngulugulu, Kafule, Ikinga, Malangali, Kalembo na Bupigu. Wakati huo huo ukanda wa Bulambya unajumuisha kata za Isongole, Chitete, Mbebe, Mlale, Ndola na Itumba. Wapo wanaojaribu kuziweka kata za Ibaba kwenye ukanda wa Undali, lakini kwa usahihi na ushahidi wa kihistoria ni ukanda wa Umalila.

Wilaya ya Ileje upande wa kaskazini inapakana na Mbeya vijijini na Wilaya ya Rungwe, upande wa Mashariki inapakana na Wilaya ya Kyela, kaskazini magharibi inapakana na Wilaya ya Mbozi na kusini ikizungukwa na nchi za Zambia na Malawi, huku mpaka wake ukiwa mkubwa kwa upande wa Malawi.

KISIASA.

Wilaya ya Ileje inaongozwa na Chama Cha Mapinduzi na haijawahi kuongozwa na Chama chochote kwa upande wa Ubunge. Mbunge wake wa sasa ni Mhe Godfrey Kasekenya Msongwe ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi. Watangulizi wake ni Mhe Janet Zebedayo Mbene, Mhe Aliko Nikusuma Kibona, Mh Gidion Asimulike Cheyo, Marehemu Steven Andendekisye Kibona na Marehemu Mbembela. Mhe Mbene ni mwanamke wa kwanza kushinda nafasi ya Ubunge kwa jimbo la Ileje na mkoa wa Mbeya na Songwe kwa ujumla.

Kiutawala, Wilaya ya Ileje ipo chini ya himaya ya Mkuu wa Wilaya Mhe Nicodemus MKUDE na Mkurugezi Haji MNASI. Huku halmashauri ikiongozwa na Mhe UBATIZO SONGA Diwani wa Kata ya Bupigu. Makao makuu ya Wilaya yanapatikana Kata Ya Itumba.

Kwa ujumla leo pamoja na kukupa ufahamu juu ya Wilaya hii, lakini ninataka niwapitishe kidogo kwenye baadhi ya fursa adhimu zinazopatikana kwenye Wilaya hii iliyojaliwa rutuba nzuri na jiografia ya kuvutia. Serikali ya awamu ya sita inaamini katika uwekezaji ili kufikia Maendeleo endelevu. Ni wajibu wetu kuwafungua macho na masikio juu ya fursa zilizopo Tanzania. Leo nitajikita zaidi kukuonyesha fursa za Wilaya ya Ileje.

KATA NA FURSA ZINAZOPATIKANA.

Kama nilivyokwisha sema hapo juu fursa zinazopatikana ni nyingi na zinatofautiana kutoka kata moja kwenda kata nyingine. Leo nitajitahidi kuzitaja fursa kadhaa ijapo kwa umhimu wake kwa wale watakao taka kwenda kuwekeza Ilje Mkoani Songwe. Kabla ya kuzitaja fursa hizo naomba uzitambue kwanza hizo kata zinazounda Wilaya hiyo kuwa ni kata 18 ambazo ni kwa majina ni Ngulilo, Luswisi, Lubanda, Sange, Ngulugulu, Kafule, Ikinga, Malangali, Kalembo, Bupigu, Isongole, Chitete, Mbebe, Mlale, Itumba, Ndola, Itale na Ibaba.

Baada ya kuzijua kata hizo kwa majina, basi nikuwekee fursa zinazopatikana kwenye kata hizo. Fursa hizo nitazigawa kikanda. Ikumbukwe kuwa hapo awali nilikutajia kuwa kuna kanda mahusi tatu, Undali, Ulambya na Umalila.

UWANDA WA UNDALI.

Uwanda huu ni maarufu kwa kilimo cha mazao ya chakula na biashara. Ni ukanda wenye mvua za kutosha. Ni ukanda ambao umefunikwa na milima ya kuvutia ambayo inaruhusu kilimo. Uwanda huu hustawi vizuri Kahawa, Iliki, Migomba, Nanasi, Mapalachichi, Mihogo, Pilipili, Mahindi, Magimbi, Miti ya Mbao n.k. Ifahamike kuwa iliki bora na inayopendwa Duniani inatoka Ileje. Lakini hata kahawa ya Ileje inasifiwa kuwa na ubora mkubwa hii ni kutokana na uoto wa asili unapotikana huko ambao huifanya ladha hiyo ya kahawa kuwa tofauti.

Kata za Ikinga, Kafule na Ngulugulu pamoja na uzalishaji mkubwa wa Ndizi, pia ni wakulima wakubwa wa zao la Iliki(cardamom) na Kahawa. Wakati kata za Sange, Ngulilo, Lubanda na Luswisi nje na kutegemea sana zao la Mbao, lakini pia wananchi wake wanalima sana Nanasi, Ndizi, Viazi aina zote, yaani mviringo(irish potatoes) na Viazi vitamu, Mihogo, Pilipili na Mapalachichi. Haya ni mazao ambayo kwa kipekee yanazalishwa sana kama mazao ya biashara.

UKANDA WA UMALILA,

Uwanda huu wa Umalila unaundwa na kata za Ibaba na Itale ambazo kijiografia zina eneo kubwa la kiutawala. Ni kata ambazo zinarutuba ambayo karibia mazao yote yanazalishwa vizuri na Wananchi wake kushindwa kufanya chaguo sahihi la kitu gani wazalishe sana kwa kuwa rutuba inakubali karibia mazao yote yanayolimwa Ileje. Kwa Kiwango Kikubwa ina udongo wa tifutifu na eneo dogo udogo wa kichanga na mfinyanzi hasa vijiji vya shuba na Itega. Mazao yanayozalishwa kwa wingi ni Mahindi, Ngano, Ulezi, Mtama, Vitungu, Miwa, Nyanya, Pareto, Mapalachichi, Ndizi, Maembe, kahawa Miti ya ,Mbao n.k
Zao kubwa wanalotegemea kwa sasa kwa biashara ni Pareto, Kahawa, Miwa, Maharage, Njegele, Tunisia, palachichi na Mbao. Kwa sasa kata ya Itale ndiyo naweza kusema inaongoza kwa uzalishaji mkubwa wa Palachichi, huku Ibaba wakizalisha zaidi Pareto, Palachichi na Mbao. Asilimia kubwa ya mbao zinazotoka Ileje basi hutoka huko.

-lUWANDA WA ULAMBYA,

Ukanda huundwa na kata za Ndola, Mlale, Itumba, Mbebe, Chitete, Isongole na Itumba. Hizi ni kata ambazo zinategemea sana kilimo cha msimu ijapo yapo maeneo huzalisha muda wote kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji. Ulambya ni maarufu kwa kuzalisha sana Mahindi, Kalanga, Mahalage, Mpunga, Maembe, Mtama na Ulezi. Ni ukweli uliowazi kuwa mahindi yenye unga bora na pendwa hulimwa Ulambya. Karanga bora na ambazo zinahitajika sana zinapatika Ulambya wengi wakipenda kuziita kalanga za malawi.Wakati kata za Mbebe na Chitete hubebwa zaidi na kilimo cha Umwagiliaji msimu wa kiangazi lakini bado kipindi Cha mvua hupata mvua nyingi. Kilimo cha uwanda huu huanza miezi ya October na hutegemea mvua tofauti na uwanda wa Umalila na Undali ambako aridhi ni owevu muda wote. Pia kata chache kati ya hizi hutegemea sana Mto Songwe ambao ndio mpaka wa Malawi na Tanzania kwa kilimo cha umwagiliaji.

Kata za Kalembo ni kata ambazo karibia zinachukua uoto wa nyanda zote, hivyo hupelekea kuzalisha mazao mchanganyiko, ijapo zinamezwa zaidi na ukanda wa Undali huku Bupigu ikiwa inamezwa na ukanda wa Ulambya.

Pamoja na fursa hizo hapo, pia Ileje inazo fursa zingine ambazo endapo zitatumika ipasavyo zinaweza kuchochea Maendeleo ya Wilaya na Taifa kwa ujumla.

Nje na fursa zote zilizotajwa Ileje pia aridhi yake ni maarufu kwa uzalishaji wa Mbogamboga kwani aridhi yake ni nzuri sana. Wakati wa utawala wa Mhe Mbene aliwahi kusema anafikiria namna ya kushawishi wawekezaji ili waje kulima mbogamboga na kuutumia Uwanja wa Songwe airport kusafishia. Lakini inasadikika ni wilaya ambayo imezungukwa na madini ambayo bado hayajafanyiwa utafiti, ijapo ukionana na wazee wanasema zamani walikuwa wakichimba kwa njia za asili kabla ya serikali kupiga marufuku. Hadi sasa Madini yanayozalishwa kwa Wingi na kuitangaza Wilaya ya Ileje ni MAKAA YA MAWE yanayozalishwa kata ya Ikinga Wilayani Ileje. Mgodi huu ambao ni maarufu kwa Mgodi wa Kiwila Coal Mine (Kaburu) Upo Kata ya ikinga Wilayani Ileje, Ijapo bado Wananchi wa Ileje hawajafaidika na uzalishaji huu moja kwa moja. Lakini pia ukipata fursa ya kuongea na wazee wanakwambia Ileje kuna Madini mengi mbali na makaa ya mawe.

Ileje pia inatajwa kuwa na nyani weupe ambao kwa Tanzania hupatikani huko tu. Hawa nyani weupe ambao ni kivutio Kikubwa cha Utalii wanapatikana kata ya Sange. Sange huko pia kuna maporomoko ya maji yaani Sange water fall.

Tanzania ya viwanda inategemea sana uwekezaji, Uchumi wakati unategemea sana uwekezaji. Hivyo Watanzania tunayo aridhi ya kutosha. Tutumie aridhi tuliyopewa na Mungu kuwekeza ili kuendana na kasi ya sera ya nchi. Nitakuwa ninawaletea makala toka Wilaya tofauti nchini ili kutambulisha fursa tunazoweza kuzitumia. Tanzania ni tajiri, alitusisitiza Hayati Dkt John Magufuli. Twendeni Ileje kusaka fursa.
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
107,251
2,000

Ujinga ni mzigo.
Hiyo namba yako ya simu inahusiana na nini na Ileje?
 
luck

JF-Expert Member
Oct 3, 2009
1,172

mbona hujaelezea mambo ya uchawi. niliwahi kuskia watu wa huko wanaabudu uchawi hadi hatari.
 
Abuu Dharr

JF-Expert Member
Dec 28, 2017
2,787

Asante Chief kwa somo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom