Itakuwa vipi Qaddafi akikimbilia Tanzania?

Atajihifadhi pale Dodoma kwenye msikiti anaodai kajenga yeye kumbe umejengwa kwa hela za mafuta ya Walibya. Hata hivyo mashinikizo ya Walibya yatafanya tumrejeshe kwao akakabiliane na adhabu kali ya kunyongwa kwa madhila aliyowafanyia Walibya wenzake.
 
Atafikia kwa Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabaan anasema Gaddafi ni mtu mzuri tu kwa vile alijenga msikiti Dodoma.

Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi ndivyo isivyowezekana kwa huyu jamaa kukimbilia Tanzania. Ben Ali (Tunisia) na Mobarak (Misri) wanaweza kusamehewa lakini huyu juha anayewainukia na kumwaga damu za watu wake mwenyewe hakika mauti inamwandama.

Anayo mawili tu; na la nafuu zaidi kwake ni The Hague vinginevyo kitanzi kinamsubiri nchini kwake mwenyewe. Uchaguzi anao yeye mwenyewe. Enyi viongozi madhalimu jifunzeni kusoma alama za nyakati kwani viburi vya madaraka ni vya kitambo tu hata kama kitambo chenyewe ni sawa na umri wa mwanadamu lakini hatima yake haki itashinda hata kama itakawia kwa muda gani.
 
Akimbilie tu na madola/mahela yake kwani hiyo ni kuvuja kwa pakacha.. nafuuu ya mchukuzi.... Lakini kwa uharisia sidhani kama atakuja au kukimbilia Tanzania maana imeripotiwa na vyombo vya habari kwamba baadhi ya watoto wake wako kwa chavez venezuela kisiwa cha margarita labda na yeye atakimbilia huko...Chavez ni wazi anaziweza propoganda za west na pia atajua namna ya kukabiliana na hao wanaomtaka Gadafi...
 
Qaddafi yupi mnayemuongelea hapa? Ni yule mwenye bar kule yombo buza au huyu wa Libya? Walibya hawezi kuja kwani ninaamini kwa dhati kabisa wananchi wa Libya hawawezi kumuondoa.that is true story
 
hawezi kuja hapa,atakimbilia Venezuela kwa Charvez au zimbabwe kwa rafiki yake Mugabe,lakini akija hapa atataka kuwa mtawala wa hapa.kwani ujinga wake wa kufikiri ndio uliomsukuma kufanyia watu wake madudu.Amekataliwa na wananchi wake.waarabu wameamka wanataka demokrasia na utawala wa haki,visingizio vya kuwa wanapigania udhalimu wa serikali za magharibi dhidi ya waarabu,hali huku wanawekeza,wakitumbua na kuficha fedha zao katika mabenki katika nchi za magharibu umekwisha.Game over kizazi kipya hakidanganyiki.
 
Akija tutampa ashike urais wa JMT hadi uchaguzi wa 2015, kwa sasa urais uko kwenye Auto..
 
Hainashaka atafikia dodoma, kule kajenga Msikiti mkubwa, namwonea huruma yule baba, mkwara wote ule na mabodigadi wake wa kike teh!
 
atafute nini huku? Wakati wa vita vya Tanzania na Uganda alimsapoti Idd Amini ili atuchape lakini akachemsha. Nina ushahidi wa mizinga na bunduki zilizotoka Libya kuwapiga watanzania. Kudadeki kwavile walikuwa wageni wa njia na nchi kwa ujumla wakachapya vibaya mmno. Reference Video for Tanzania and Uganda war. Akija tu nakumbushia kudadekiiiiiiiii
 
Qaddafi yupi mnayemuongelea hapa? Ni yule mwenye bar kule yombo buza au huyu wa Libya? Walibya hawezi kuja kwani ninaamini kwa dhati kabisa wananchi wa Libya hawawezi kumuondoa.that is true story

lazima aondoke. imeandikwa hiyo.

mpaka sasa yeye ni Rais wa Tripoli, siyo Libya.

Miji inaanguka mikononi mwa wapinzani, viongozi waandamizi wanaasi, maofisa wa jeshi wanaasi, raia wa nchi rafiki wanaondoka, tena wengine wanachukuliwa kimafia kama walivyochukuliwa raia wa uingereza kwa ndege ambayo ilipasua anga za libya bila hata rada za libya kujua. amebaki na support ya watu wa kabila lake na ndugu zake tu.
 
Qaddafi yupi mnayemuongelea hapa? Ni yule mwenye bar kule yombo buza au huyu wa Libya? Walibya hawezi kuja kwani ninaamini kwa dhati kabisa wananchi wa Libya hawawezi kumuondoa.that is true story

acha ufutuhi kwenye jukwaa serious. Sishangai ni madhara ya shule za kata
 
atafute nini huku? Wakati wa vita vya Tanzania na Uganda alimsapoti Idd Amini ili atuchape lakini akachemsha. Nina ushahidi wa mizinga na bunduki zilizotoka Libya kuwapiga watanzania. Kudadeki kwavile walikuwa wageni wa njia na nchi kwa ujumla wakachapya vibaya mmno. Reference Video for Tanzania and Uganda war. Akija tu nakumbushia kudadekiiiiiiiii

hilo neno la mwisho linaonesha we ni kizazi cha mkapa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom