Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Teyari tumesikia taarifa juu ya Rais Samia kukutana na viongozi wa vyama vya siasa hapa nchini katika siku na tarehe ambayo bado haijawekwa wazi kwa umma huku mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Bwana Freeman Mbowe akiwa mahabusu kwa kesi inayolalamikiwa kuwa ni ya kubambikiziwa.
Kwa hali ilivyo, ni wazi mkutano huo utafanyika huku Mwenyekiti huyo wa CHADEMA ndani kwani si rahisi atoke mapema unless kuwe na maahikinikizo makubwa ya ndani na nje ya nchi kwani danadana za kesi yake tayari zimeshaanza na bila shaka zitaendelea.
Swali ni je, katika mazingira haya, itakuwa sahihi kwa CHADEMA kushiriki katika hayo mazungumzo huko mwenyekiti akiwa ndani kwa kesi inayodaiwa kuwa ni ya kubambikiziwa?
Au itakuwa ni busara kwa CHADEMA kugomea mazungumzo hayo kama shinikizo la kutaka Mbowe atendewe haki katika hiyo kesi au kwa sharit la kutakai kes hiyo ifutwe kama haiwezi kuendesha.kwa haki?
Binafsi naamini kitendo cha Mbowe kuongoza harakati za kudai katiba mpya pamoja na yeye kufunguliwa hii kesi inayopingwa Karibu kila kona ya hii dunia, ni moja ya mambo yaliyoisukuma serikali kukutana na wapinzani katika harakati za kujisafisha mbele ya.umma wa watanzania na dunia kwa ujumla, hivyo ushirika wa CHADEMA katika mazungumzo haya ni muhimu sana.
Sasa narudia swali langu hili:
Je, CHADEMA washiriki hayo mazungumzo wakiwa na agenda ya kutaka Mbowe afutiwe hiyo kesi inayodaiwa kuwa ni ya kubambikiziwa au wasishiriki kabisa kama shinikizo la kutaka Mbowe aachiwe au atendewe haki katika hiyo kesi?
Nawasilisha.