IT Professionals in Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IT Professionals in Tanzania

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Fundi, Feb 13, 2009.

 1. F

  Fundi New Member

  #1
  Feb 13, 2009
  Joined: Mar 2, 2008
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I know that:-
  Engineers are registered by ERB
  Contractors are registered by CRB
  Accountants are registered by NBAA?

  I would like to know who registers IT professional in Tanzania.
   
 2. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,283
  Trophy Points: 280
  Mkubwa thats good idea we need to form IT organiztion
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  hiyo tunaipigania kila siku watu wako kimya tutaendelea kuitumikia kenya kwa mtindo huu milele
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,189
  Trophy Points: 280
  Haya ni mambo ya ukiritimba, ni kama guilds za miaka ya mwisho ya karne ya 19 Ulaya.Kazi ya NBAA ni nini zaidi ya kuhakikisha namba ya wahasibu inaendelea kuwa ndogo kwa kuweka mitihani iliyo overly restrictive?

  Nature ya IT iko global, na tayari kuna global organizations zinazoweza kuku register na kuku certify (Microsoft, Cisco etc) sasa sioni umuhimu wa kuwa na ukiritimba mwingine Tanzania.

  Unless unaniambia kuwa unataka kuwepo na networking body, ambayo inakuwa tofauti kabisa na NBAA kwani NBAA inaamua nani anakuwa mhasibu na nai hawezi kuwa, kuwa na chombo kama NBAA kwa IT professionals kunaenda kinyume na spirit nzima ya "bottom-up" ya IT sasa hivi (open source, wikinomics etc).

  Huu ni mfano wa "herd like" groupthink iliyokosa innovation, tunataka an organization like NBAA just to keep up with the Joneses without assessing what IT really needs.If IT is to flourish, we need no petty guilds and more innovation, and this is certainly not innovation.

  Fat cats have done enough damage to our country.Let's not shortchange IT, it is bigger than these "little town blues".
   
  Last edited: Feb 13, 2009
 5. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Sioni faida ya kuwa na kitu kama hicho, sana sana itaongeza rushwa na kuoneana.
   
 6. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,283
  Trophy Points: 280
  Yes mkubwa but at least kuwe network kupeana michongo na dili mbalimbali
   
 7. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #7
  Feb 15, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sisi utajuanae bila social networking kama hizo ? Utatambulikaje ? Kenya wanayo yao sasa hivi kila graduate anatakiwa awe mwanachama na wafanyakazi wengi wanakuwa recruited kutoka kule kutokana na perfomance zao
   
 8. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Jamani hiyo association ipo na inafanya kazi hadi leo, na uchaguzi huwa unafanyika kama kawaida. Pengine tu haijatangazwa sana ndio maana wengi humu wanaonekana hawaifahamu. Website hii hapa

  Tanzania Information Technology Association - Home

  Haya basi jiungeni mliokuwa bado.
   
 9. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Kama ni kama networking tool sina pingamizi, lakini kama ni kutoa leseni kama za Engineers hapo ndo sitaki.
   
 10. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Labda kama nimekosea,si hii inayoitwa TAT?? mmmh kule ni kutiana aibu watu wa IT,hakuna la maana nililoona,kila link underconstruction,hakuna information yeyote ya maana,Mission na vission haviendani na nini website inatoa kazi ni kulist registration fees tu,jamani siasa hadi huku kwetu kwenye It?
  angalia viongozi:
  1 Dr. Jabiri Kuwe Bakari The Open University of Tanzania Chairman
  2 Mr. Mulembwa Munaku Computer Science Department-UDSM Vice Chairman
  3 Ms. Elizabeth Mkoba Tanzania Education Authority Executive Secretary
  4 Mr. Adam Mambi MKURABITA Vice Executive Secretary
  5 Mr. Frank Goyayi
  Baada ya kuangalia hawa viongozi nikagundua kitu,IT ya sasa si ile ya miaka 40,IT Expert wa sasa anajua jinsi ya kutumia IT yake ili ikindhi matakwa ya jamii na si tu kuprogram kama ilivyokuwa zamani ndio maana utakuta siku hizi kwenye IT kuna hadi Accounting,OB,Finance nk.
  Wito,watu wote wa IT tukae chini tuokoe hili jahazi jamani.
   

  Attached Files:

  • TAT1.JPG
   TAT1.JPG
   File size:
   132.8 KB
   Views:
   84
 11. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Opaque nadhani utakuwa unawajua hawa watu,hata form yao haifanyi kazi,natamani nilie hapa.ngoja niishie hapa la sivyo nitatoa maneno ya mbali bure...
   
 12. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,283
  Trophy Points: 280
  Mbona member wako wachache mno, imeanzishwa mwaka huu nini? na watu wengi hawaifahamu
   
 13. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #13
  Feb 15, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Itakuwa ni ya watu wachache wamekaa huko aliko wakaombea pesa wakafanya kitu kama icho now its gone si unaona hata mahala kwa office hakuna ??
   
 14. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Shy kwa leo naungana na wewe,inaonekana kwamba hakuna kinachoendelea,ni kweli inawezekana kabisa washalamba mshiko thenwakatimka,ila wakae mkao wa kula.ukweli utagundulika tuu.Nakumbuka kuna usemi unasema Huwezi kuwafaya wapumbavu watu wote kwa wakati wote.
   
 15. F

  Fundi New Member

  #15
  Feb 18, 2009
  Joined: Mar 2, 2008
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawashukuru kwa michango yenu mizuri kuhusu swala hili.

  Lengo la kuwa na chombo cha kusajili IT professional lengo lake siyo kuongeza urasimu. Nafahamu jinsi waTanzania tusivyopenda kuendeleza wenzetu, amabapo walimu husifika kwa kuwa na idadi kubwa ya wanfunzi walioshindwa mtihani kuliko waliofaulu.

  Nitawapa mfano wa Japan amabapo wanachombo kinachosimamia IT nchi nzima, kinaitwa IT Strategic Head Quaters. Malengo ya chombo hiki ni:
  ‘In light of the urgency to adapt ourselves to the world's rapid and drastic changes in the socio-economic structure caused by the utilization of information and telecommunications technology, in order to promote measures for forming an advanced information and telecommunications network society expeditiously and intensively, in January 2001, the Strategic Headquarters for the Promotion of an Advanced Information and Telecommunications Network Society (IT Strategic Headquarters) was established within the Cabinet’.

  CEO wa kitengo hiki ni Waziri Mkuu!

  Chini yake kuna vyombo vingine kinachofanya navyo kazi. Kimojawapo kinaitwa IT Coordinator. Hiki ndiyo husajili wataalam wa IT. Kinaadaa mafunzo (professional training), kinatoa ushauri serikalini na makampuni kwa kuwatumia waliosajiliwa (hakiwalipi, kama ni malipo ni huko walikotoa ushauri). Wataalam hupangwa kwa ngazi kulingana na mafanikio yao katika kazi walizofanya, pamoja na kufaulu mafunzo yanayotolewa na chombo hiki.

  Vyombo hivi viliundwa kwa kupitishwa sheria husika. Ona mfano wa sheria ya kuanzisha IT Strategic HQ.

  Tusikate tamaa kwa sababu mambo yetu hayaendi vizuri kwa sasa. Tuishauri serikali iunde chombo hiki, chenye mamlaka na kuweka wataalam wa IT wakiongoze kwa manufaa ya nchi. Hiki ndiyo kitakuwa kinatoa ushauri kwa serikali ifanye nini kuboresha ukuzaji matumizi ya Tehama.

  Ninaishia hapo kwa leo.
   
 16. C

  CottonEyeJoe JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2009
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Why dont we start an informal network right here on JF in the form of a thread, candidates can begin by posting the Cv or professional profiles, (even if its by using Forum names), and we can take it from there and see how this thing grows. Kuna thread ya kutafuta kazi, why shouldnt there be one ya wapiga kazi wa IT? alternativley we can develop a blog like site like Maro's ya kazi except this one would have professionals and could categorize them in their disciplines or specialisms (databases, software engineering, networking, web design, etc)....
   
 17. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #17
  Feb 22, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Cottoneye

  hiyo itapendeza sana nafikiri tunaweza kuanza mimi na wewe tuwe mfano wengine watufuatie unaonaje ?? Mimi niko tayari kuanzisha mkakati huo hata sasa hivi kesho hata kesho kutwa
   
 18. C

  CottonEyeJoe JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2009
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Twende kazi!!!....ila due to the fact kwamba unauzoefu mkubwa zaidi kwenye hili (from what i can see!!) ningekuomba u-take the lead on this...am willing to support in any way!!!!
   
 19. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #19
  Feb 23, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nianze KIVIPI KWANZA UMEONGEA NA MODERATOR KUSIKIA MAONI YAKE YEYE ANAONAJE ??
   
 20. Modereta

  Modereta Senior Member

  #20
  Feb 23, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi si mtu wa IT, lakini mawazo ya Kiranga na Kang na wote wanaopinga tu ni kwa sababu wanapanga Mission Statement na Vision kwa kuangalia yaliyopita na IT au ICT (maana haviwezi tenganishwa)ni zaidi ya Historia ya "madudu" si kwa sababu akina fulani walipoanzisha waliboronga basi chochote kitakacho undwa au kuendelezwa kitaboronga.

  Nawaomba akina Kiranga/Kang waje na mawazo ya kuboresha sio kukataa tu. Hii sio lazima iwe "Statutory body" inaweza kuwa Association itakayokuwa sauti ya wana IT/ICT, kuna methali isemayo UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU. Inaweza ikawa ASSOCIATION na katiba yake ikalinda na kutoa msimamo wa wana IT/ICT. Mbona tuna wataalamu wengi wa IT lakini bado miradi mikubwa inaendeshwa na kumilikiwa na watu wa nje???????????????? Mko wapi wana IT, hamna chombo chochote cha kuwaongelea. Kuna mifano mingi inayoweza kuigwa kama Institution of Engineers Tanzania (IET) ni imara na inaheshimiwa sana sera yeyote inayojadiliwa kuhusu Uhandisi/Viwanda angalau huwa wanaitwa, kuna Tnzania Milk Processors Association (TAMPA) imefanya makubwa kwenye sekta hiyo, kulikuwa na Tanzania Pharmaceutical Assictaion ilifanya mengi wakati fulani ikajaharibiwa na mtu aliyeleta ukiritimba wa kusabotage waswahili, wakamfukuzia mbali, nk.

  WITO kama mnataka IT/ICT iwe moto ni kuwa na chama si STATUTORY BODY kama NBAA au ERB au Bodi ya WAFAMASIA ila vitu kama IET, TAMPA vitakavyo pigania maslahi na haki pamoja na hata nafasi za wataaluma wa IT/ICT hapa.
  Nakumbuka kulikuwa na TITA (Tanzania IT Association) walifanya mkutano pale IFM, halafu kulikuwa na TICTA (Tanzania ICT Association) halafu TISPA (Tanzania ISP Association) sijui ziko wapi.
   
Loading...