Naomba ushauri kuhusu gari aina ya Isuzu Big Horn

Aisee,usinunue hiyo,labda kama umeamua kuishiwa mapema,hutaweza kuitengeneza,ni gari mbovu sana hizo na ukitaka kuuza itakusumbua sana,parts ghari na bei mbaya.
Tafuta Toyota
 
Hii gari imetulia sana,tatizo wabongo tunafata mkumbo bila kupima wenyewe ubora wa gari kila mtu utamsikia anazungumzia Toyota.
kwa kifupi kama unataka kunuinunua hii gari nakushauri nunua tena kwa roho safiiiii hutajuta kamwe.ukiweza tafuta inayotumia diesel ya kuanzia mwaka 2002 na kuendelea.yenye engine aina ya 4jx1,hapo ni mkataba kabisa.
Angalizo ni kwamba hii engine inatumia oil number 5W30 ni nyepesi kama maji na usije ukaweka oil tofauti na hiyo kamwe! ukiweka oil tofauti ndio umeua engine.
 
Magari mabovu sana,kaka yangu aliingia kichwa kichwa akauza Tdi akalinunua alijuta kwani halikumaliza miezi 3 likasumbua engine akalitengeneza kwa gharama kubwa na baada ya mwezi engine ikafa.Paka leo ni mwaka wa pili kalipaki.
 
Hizi gari ziko poa sana hasa ukipata toleo la Uingereza ila tatizo ni moja tuu ndoa ya kikristo , wote waliokaa nayo miaka mitano au sita sio kwa kupenda
 
Mimi nimetoa mchango wangu kwa members, kutokana na uzoefu nilionao wa kuendesha na kumiliki aina zote mbili za magari. Toyota Prado. Model: kzj95 na Isuzu bighorn, model: UBS73GW.
Pia kwa kutumia knowledge yangu kama Mechanical engineer.
Isuzu bighorn ni sawa na Isuzu trooper. Isuzu bighorn ni kwa ajili ya market ya Japan na Isuzu trooper kwa market ya Europe.
Nadhani tuna tatizo na ndiyo faida ya hii mitandao, kwa lengo la kuelimishana. Watu wengi tunanunua magari kwa sababu tu tumepata pesa, na kwa sababu jamaa yangu au rafiki anayo gari aina hiyo. Hutashangaa kusikia mtu anasema nataka kununua gari kama ya fulani. Kwa kuwa tu pengine ina sura ya kuvutia. Au kwa ajili ya trade mark (chata). Hatufanyi utafiti wa kutosha kabla ya kufanya maamuzi.
Sisemi tunakurupuka ila siyo dhambi kupata ushauri wa kitaalam.
Fanya utafiti wa kutosha, utabaini kwamba Toyota Prado mayai. Model: kxj 95, suspension system yake inatumia coil springs nyuma na mbele. Mfumo ambao unafanya gari isitulie barabarani, hasa kwenye mwendo wa kasi kuanzia 120km/hr. Na ukifuatilia utagundua kuwa magari mengi ya model hii yameshapata msukosuko wa kuanguka. Ni kwa sababu ya mfumo huu wa suspension. Tatizo ambalo hata Toyota waligundua baadaye na kubadilisha mfumo kwa model iliyofuata baadaye.
Isuzu bighorn inatumia suspension system yenye coil sptings kwa nyuma na wishbone kwa mbele, mfumo unaofanya gari iwe very stable hata kwenye mwendo kasi k20km/hr na kuendelea.
 
asanteni wakuu kwa ushauri MUNAWARA kwa kweli naona niagize hii makitu maana ukishakuwa na hela ni kama vile zina majini utasikia ooh shangazi kaanguka juu ya mti tuchange tumlete MUHIMBILI. Asanteni sana.
Nimecheka sana mkuu...hahahahahahah
 
Hii gari imetulia sana,tatizo wabongo tunafata mkumbo bila kupima wenyewe ubora wa gari kila mtu utamsikia anazungumzia Toyota.
kwa kifupi kama unataka kunuinunua hii gari nakushauri nunua tena kwa roho safiiiii hutajuta kamwe.ukiweza tafuta inayotumia diesel ya kuanzia mwaka 2002 na kuendelea.yenye engine aina ya 4jx1,hapo ni mkataba kabisa.
Angalizo ni kwamba hii engine inatumia oil number 5W30 ni nyepesi kama maji na usije ukaweka oil tofauti na hiyo kamwe! ukiweka oil tofauti ndio umeua engine.
Kiufupi ni kwamba engine nyingi tofauti na Toyota oil zinataka zile super tu mambo ya Oryx za elf 30 lita 5 nooo
 
Wakuu nimechungulia Be Forward wanayo ya 2,990 cc. 4WD ya 1998 diesel Engine code: 4JX1 kwa 2700 CIF kesho naenda kutuma pesa ili nijihakikishie chombo. Swift Bye bye Sina Habarrriiii
 
Wakuu nimechungulia Be Forward wanayo ya 2,990 cc. 4WD ya 1998 diesel Engine code: 4JX1 kwa 2700 CIF kesho naenda kutuma pesa ili nijihakikishie chombo. Swift Bye bye Sina Habarrriiii
Nunua tu, hata mimi ninayo, 4jx1 turbo diesel, hiyo mashine inakimbia balaa, hiyo ni "Euro 3" engine, ni moja ya hi tech diesel engine, emission standard zimezingatiwa, ukiona gari imekubalika hata USA na UK siyo kitu ya mchezo. Pia ina Onboard Diagnostic, unaweza ukagundua baadhi ya matatizo ya engine kwa kutumia dashboard yako, kabla ya kumuita fundi, tutajuzana kwa kirefu.
1474525666460.jpg

Gari iko vizuri hiyo, hakikisha unanunua inayotumia diesel, ulaji wa mafuta uko vizuri 13km/L. Mafundi wapo wa kutosha kutokana na tatizo. Iko sensitive sana na Engine Oil, lazma uweke inayofaa. Haitaki mafundi uchwar. Inakimbia sana kama una roho nyepesi unamaliza zote 180km/h.

Mimi ninayo ya mwaka 2000, 4JX1 Turbo Engine, Manual Transmission tangu 2013.
View attachment 399074 View attachment 399075 View attachment 399077
 
Hiyo gari ni cheap kununua ila haziko maarufu kiviile so unaweza pata shida kdg kama unataka kuiuza
 
Wakuu nimeishanunua mashine BIG HORN ipo vizuri sana naokota mademu vituoni mwanzo-mwisho. Asubuhi wakati naenda job.
Hongera mkuu, enjoy the ride. Recommended Engine Oil kwa africa kutokana na joto ni 10W40 Fully Synthetic - Bora zaidi ni Atlantic au Castrol na inaenda mpaka 10,000 kms, recommended 8,000Kms
 
Hongera mkuu, enjoy the ride. Recommended Engine Oil kwa africa kutokana na joto ni 10W40 Fully Synthetic - Bora zaidi ni Atlantic au Castrol na inaenda mpaka 10,000 kms, recommended 8,000Kms

Hii castro unaweza tumia kwa gari yoyote??
 
Back
Top Bottom