IST ina tatizo la coolant kutorudi kwenye rejeta kutoka kwenye reserve tank

Duuuu hii ya leo Kali jamani!
Kwa hiyo ina maana hiyo coolant inasukumwa kutoka Kwenye radiator Hadi Kwenye engine Kwa kutumia nini?
Au coolant unapita Kwenye mfumo tofauti na maji?...
Water pump ingekua imekufa angeshajua bila kumuita fundi, kwanza maji yote ya ktk rejeta yangeisha ndani ya dk moja mara tu baada ya kuiwasha gari na pia sign ya engine kuwa overheated ingetokea kwenye dashboard.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari Wakuu!

Naomba msaada wa kiufundi kwa IST kutorejesha coolant kwenye rejeta kutoka kwenye reserve tank ambayo imekuwa ikimwagika baada ya kujaa. Nimejaribu kubadilisha kifuniko cha rejeta lakini tatizo bado linaendelea.
Sidhani kama maelezo yako yanatosheleza. Ninachojua mimi, coolant unaijaza kwenye radiator, halafu unajaza tena kwenye reserve tank mpaka kwenye minimum ili nafasi ya kupumua iwepo.

Inawezekana unajaza coolant mpaka full kwenye radiator, na kisha kuijaza mpaka juu kwenye reserve hadi coolant kumwagika baada ya kupata joto.

Ufuniko gani unatema coolant? Wa radiator au reserve?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa uelewa wangu mdogo nitakujibu, kiufupi umemaanisha gari yako inarudisha coolant fluid juu badala kuvuta ndani. Kama unamwamini fundi wako mwambie ajaribu kukagua cylinder gasket kama bado inaziba/ seal vizuri.

kuna mdau amegusia waterpump, nalo tilia maanani kidogo. Thermostat rudisha maana ndio inayopeleka taarifa kwenye control box kua engine inapandisha joto ili vitu vingine vya kupooza vifanye kazi yake.

Nijuavyo, coolant fluid haitakiwi irudishwe juu kiasi cha kufanya ipenye mfuniko na kumwagika chini. Inakolelekea ni kupasua horse pipes.
Thermostat haihusiani kabisa na kutuma any information kwenda kwenye control box and there is no any cable send information from thermostat to elsewhere, thermostat inafanya kazi kutokana na heat conductivity

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa uelewa wangu mdogo nitakujibu, kiufupi umemaanisha gari yako inarudisha coolant fluid juu badala kuvuta ndani. Kama unamwamini fundi wako mwambie ajaribu kukagua cylinder gasket kama bado inaziba/ seal vizuri.

kuna mdau amegusia waterpump, nalo tilia maanani kidogo. Thermostat rudisha maana ndio inayopeleka taarifa kwenye control box kua engine inapandisha joto ili vitu vingine vya kupooza vifanye kazi yake.

Nijuavyo, coolant fluid haitakiwi irudishwe juu kiasi cha kufanya ipenye mfuniko na kumwagika chini. Inakolelekea ni kupasua horse pipes.
Kuna sensor ya engine temperature ndio hupeleka taarifa katika control box ili control box itoe maagizo kuwa thermostat ifungue au kufunga njia..... Zinafanya kazi pamoja...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari Wakuu!

Naomba msaada wa kiufundi kwa IST kutorejesha coolant kwenye rejeta kutoka kwenye reserve tank ambayo imekuwa ikimwagika baada ya kujaa. Nimejaribu kubadilisha kifuniko cha rejeta lakini tatizo bado linaendelea.

Tatizo linaweza kuwa moja au zaidi ya yafuatayo

1. Horse pipe(s) hazija seal vizuri. A za kuangalia kale kapipe kanakounganisha rejeta ha reserve tank. Pia kuna kapipe ndani ya reserve tank kanaweza kuwa kamelegea.

2. Mfuniko wa rejeta hauseal vizuri

3. Rejeta inavujisha. Inaweza kuwa kuna matundu madogo sana. Angalia kama kuna alama za kutu kutu kati ya rejeta na kava lake

4. (Most likely problem) Head gasket imeanza kufa. Namna ya kujua kama head gasket ndio tatizo... Washa gari hali ya kuwa umefungua mfuniko wa rejeta then piga resi. Ukiona bubbles zinatoka ujue head gasket ndio mchawi wako. Nasikitika kusema kwamba ingawa gharama ya head gasket ni sh 50,000 inaweza kukugharimu engine mpya kutokana na udhaifu mkubwa wa mafundi wetu hasa kwa engine hizo za kisasa.

NB: water pump na thermostat hazihusiani na dalili hizo ulizotaja.. na ni rahisi sana kujua kama zinasumbua
 
Wadau nina ist ya 2006, juzi niliipiga sehemu radiator ikapinda ikagusa fan na kuzuia fan kuzunguka... Kulikopelekea motor kuungua.

Baada ya motor kuungua fan ikashndwa kuzunguka na mashine ikaanza kuheat.

Shida yangu ni kuwa nishaweka motor zingine kama 2 hivi na bado injini inaheat kwa kilometer chache tu hata 30 hazifiki na maji yanaisha kabisa.

Nb.
Rejeta haivuji, sasa hapa solution ipo vipi.
Je kuna aina ya moto special kwa hizi gari, au fan special,. Na ni wapi naweza nikaipata na kwa gharama gani maaana nateseka saana na nina safari. Ya kwenda bukoba week ijayo.
 
Thanks kwa ushauri Mkuu, naomba nisaidie aina ya mfuniko mzuri maana nimebadili mara mbili na kuna fundi alidai inasababishwa na thermostat akaitoa lakini tatizo likaendelea
Kwahiyo gari yako sasa hivi haina thermostat?!
 
On another observation VANGUARD huwa hazina provission ya spare tire. Kuna maujanja ambayo wabongo wameshabuni ili kusolve hilo tatizo?
fanya swap ya mlango wa nyuma funga wa rav 4 3rd generation ...zinaingiliana milango na vanguard

9131C3E5-4145-4AA7-805A-3CD57AD8466E.jpeg
 
Wadau nina ist ya 2006, juzi niliipiga sehemu radiator ikapinda ikagusa fan na kuzuia fan kuzunguka... Kulikopelekea motor kuungua.

Baada ya motor kuungua fan ikashndwa kuzunguka na mashine ikaanza kuheat.

Shida yangu ni kuwa nishaweka motor zingine kama 2 hivi na bado injini inaheat kwa kilometer chache tu hata 30 hazifiki na maji yanaisha kabisa.

Nb.
Rejeta haivuji, sasa hapa solution ipo vipi.
Je kuna aina ya moto special kwa hizi gari, au fan special,. Na ni wapi naweza nikaipata na kwa gharama gani maaana nateseka saana na nina safari. Ya kwenda bukoba week ijayo.
Aidha Temperature switch imekufa pia.. (haiwasiliani na ECU kuitaarifu wakati gani wa kufungua feni) au ulivyogonga, thermostat imeguswa haifunguki kuruhusu Maji kuzunguka ndani ya engine block.

Engine inatakiwa kufikia joto flani ili ifanye kazi vizuri... Thermostat inaangalia kuhakikisha hili joto linalotakiwa lipo, kama halipo inazuia maji kupooza engine.., Kama lipo linazidi inaruhusu maji kupooza.

Kwa mazingira yetu (Joto kubwa) Ni kweli thermostat huwa haina kazi na ndo mana wanaichomoa... sijawai kuskia mtu anaishi Dar es Salaam anawasha gari ikagoma kuwaka kwa sababu ni ya baridi mno.. au engine yake inapoa kupita kiasi.., Joto letu ukiacha soseji nje unakuta imeiva.
 
Thanx saana mkuu nilienda kwa fundi ikagundulika kuwa fan iligeuzwa ikawa inapuliza radiator... Akabadili switch..mpaka leo mambo safi tu.

Ila nataka nikafanye service naona ukanyagaji na speed haviendan...

Km nakanyaga saana afu uchanganyaji wake sio hivi... Nikachek plug na zile coil sijuh
 
Back
Top Bottom