Issue ya Takukuru na AG kutupiana mpira Faili la Chenge iliishia wapi?

Said Bagaile

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
686
256
Wenye taarifa naomba mtujuze kuhusu lile sakata la kutaka kumpeleka mahakamani Mzee wa Vijisenti, ambapo Hosea alidai kwamba faili lipo mezani kwa AG at the same time AG akadai kwamba faili halijapelekwa kwake na TAKUKURU!

Je mnaofuatilia hii movie ipo kwenye Episode ya ngapi?
 
Takukuru hawana meno!! AG anacheza na akili za Takukuru! and Vice versa its true. Ngoja mkuu tusubiri mwenye taarifa, lakini wasiwasi wangu ni kuwa Chenge keshawapiga stop mpaka pale atakapopatikana mtu mwingine wa kuhoji kama wewe hivi.
 
wewe usiwakumbushe suala hilo, mafuta yamesaidia saidia tumesahau mengi. ukitaja Chenge tu watu wanahaha, sijui hata hatma yake ya kujivua gamba imefikia wapi. File lake ni la moto ndugu yangu.
 
Wenye taarifa naomba mtujuze kuhusu lile sakata la kutaka kumpeleka mahakamani Mzee wa Vijisenti, ambapo Hosea alidai kwamba faili lipo mezani kwa AG at the same time AG akadai kwamba faili halijapelekwa kwake na TAKUKURU!

Mkuu mie nnavyokumbuka ni kuwa majibizano yalikuwa kati ya hosea na felesh na siyo werema. Au?
 
Mda wao ukifika wote watashughulikiwa kwa pamoja (yaani kwa mpigo kama kule Egypt wanavyofanya)
 
Wenye taarifa naomba mtujuze kuhusu lile sakata la kutaka kumpeleka mahakamani Mzee wa Vijisenti, ambapo Hosea alidai kwamba faili lipo mezani kwa AG at the same time AG akadai kwamba faili halijapelekwa kwake na TAKUKURU!

Je mnaofuatilia hii movie ipo kwenye Episode ya ngapi?

Ishu ilikuwa ni kati ya Hosea (Takukuru) na DPP sio AG.
 
Ishu ilikuwa ni kati ya Hosea (Takukuru) na DPP sio AG.

Sahihi kabisa!nadhani imetoka hiyo,na misururu ya matatizo mengi yanayojiri kila siku tutasahau kama kwaida yetu

Niwakumbushe kidogo,ishu ya katiba mpya ilipopamba moto ghafla ikaja ishu ya Loliondo tukasahau
Ishu ya Loliondo ilipopamba moto ikaja ya kuvuana magamba tukasahau
Baadaye ikaja ishu ya kudai chenji ya Rada nayo tumesahau
Ukaja mgawo makali wa umeme ikifuatiwa na mafuta,uuzwaji holela wa UDA tunaelekea kusahau
Hakuna kilichoshughulikiwa kikamilifu kati ya hivyo vyote!tanzania nchi nzuri sana.
 
Je! Unaikumbuka hii!

Taaanzaniiaaa! Tanzaniaa! nakupenda kwa moyo woote.
 
Back
Top Bottom