Hutqkiwi kuwa na nchi inayojisema kwamba ni Jamhuri yenye watu sawa, halafu bado ukawa na vyeo vya uchifu vya kurithimishana.

Ama ukubali kwamba watu si sawa, na kuna wengine wako juu ya wengine kwa kuzaliwa tu kwenye familia za kichifu, ama ukubali kwamba watu ni sawa na uchifu hauna maana kubwa ufutwe.

Nyerere alichagua kuunda nchi inayodhamiria kuwa na watu wote sawa.

Hili pia lilisaidia sana kuua ukabila na kujenga umoja wa kitaifa.

Kwa sasa naona tumeamua kurudisha uchifu kwa mlango wa nyuma.
Nyerere ....usawa wa binadamu! Hizi ni blah blah hakuna hiyo kitu na ona sasa politicians wetu wanavyorithiana from one generation to another!
 
Labda anazungumzia "Kaizer Chiefs Football club"😂😂 Eti Chief Mkwawa et al waliwekwa na wakoloni!!!..
What a joke !
Nimemshangaa sana mzee wetu kusema machifu wote waliwekwa na wakoloni. Amelishwa maneno au ameghafilika?

Ninachofahamu, wapo machifu waliotumika kwa maslahi ya wakoloni ili kutawala (passive colonialism). Au tulifundishwa uongo madarasani?
 
Nyerere ....usawa wa binadamu! Hizi ni blah blah hakuna hiyo kitu na ona sasa politicians wetu wanavyorithiana from one generation to another!
Sawa basi.

Tubadili katiba tuseme hii nchi ya kifalme na machifu wanaorithishana tujue moja.
 
Huyu mzee mahaba yake kwa Nyerere sijawahi kuyapatia jibu, kwa kweli sijui alikunwa wapi Nyerere. Hopeless kabisa
 
Labda anazungumzia "Kaizer Chiefs Football club"😂😂 Eti Chief Mkwawa et al waliwekwa na wakoloni!!!..
What a joke !
Hakukuwa na machifu. Viongozi wa himaya walikuwa ni watemi. Walikuwa ndio marais au wafalme wa himaya zao. Hata neno chief si la kibantu.
 
😂Hata Google Translate imekushinda!!👇👇👇

Translation results

mtemi

Noun

chief

kiongozi, mtemi
Kizazi cha Google shida sana. Wakoloni walitengeneza utawala wao na ili kuwatawala watu ilibidi kwenye ranking zao awepo mbongo chawa wao na ndiye chief

Kwenye tawala za asili kulikuwa na kiongozi au mfalme aliyewaongiza na kupigana vita aliitwa mtemi. Achana na University of Google translate
 
Mtemi kwa "kidhungu" anaitwaje😂
1........Mkwawa et al???hawa waliwekwa na wakoloni au waliwapinga wakoloni😂😂
 
Back
Top Bottom