Ninachokiona ni kwamba CCM watawatumia machifu kuhakikisha wanaingizanseranzao kupitia machifu wakati wa uchaguzi ili waendelee kutawala.

Imagine kama Rais ndio wamemfanya mkuu wa wao maana yake wako tayari kupokea maelekezo kutoka kwake hii imekaa kimtego sana.
Machief hawana nguvu kwa kizazi cha sasa
 
View attachment 2091277
Kwani uchifu ni utamaduni wetu? Makabila mengi hawakuwa na wachifu. Waliwekwa na wakoloni kwa maslahi yao (km Wazanaki). Uchifu ulipigwa marufuku na sheria mnamo 1962. Machifu waliyokuwepo (km Adam Sapi, Fundikira, Kunambi nk) waliingizwa Serikalini katika nyadhifa mbalimbali.

Ufutaji wa uchifu ulitusaidia sana kujenga umoja wa kitaifa. Nchi zingine Za Afrika (kmNigeria, Ghana nk) wamepata shida kujenga umoja wa kitaifa. Sababu mojawapo ni machifu kulinda himaya zao kwa kukuuza ukabila badala ya utaifa. Tunachotakiwa kusisitiza ni utamaduni wa kitaifa.

Issa G. Shivji ni mwanasheria nchini Tanzania na mwandishi wa Vitabu, pia ni mmoja wa wataalamu bingwa katika Afrika wa sheria na masuala ya maendeleo.

Pia amewahi kufundisha na kufanya kazi katika vyuo vikuu mbalimbali duniani kote.

Sasa hivi unatusaidia tupate Raisi wa Ma chifu sio walio wengi
 
Nigeria machief ni matajiri balaa na wako active kwenye siasa na wana nguvu. Kuanza kusajili na kuentertain machifu no kutupeleka kubaya.
 
Kama Bunge lilikaa na kutunga sheria kisha rais akaipitisha na kuondoa kabisa shughuli za machifu. Nini nyuma ya pazia Chief Hangaya awag'ag'anie. Kuna kitu juu hii kitu. Huku ni kuvunja sheria.
Screenshot_20220122-150553.png
 
Unaongelea nchi zenye makabila mawili au matatu tu.
Acha ukihiyo S.A. unajua ina makabila mangapi?Botswana?(ufinyu wako unajua ni seswana tu!)nchi zote hizo zina makabila zaidi ya unavyofikiria
 
mama kalizua tena. akili kubwa wanaangalia mbele mbali,akili za kuunga unga anaangalia mwisho wa kivuli
MaCCM ndivyo yalivyo akili zao hazina akili.
MaCCM yanapotafuta kukubalika, uwacha uharibifu mkubwa.
Samia anajua CCM ni Chama maiti,
Anachofanya ni liwalo na liwe., CCM mbele kwa mbele.
 
Hili mimi sikubaliani nalo ni siasa tu,hebu angalia hizi nchi jirani yetu,Zambia,Namibia,Botswana,SA etc etc bado zina viongozi wao wa asili na zipo na umoja na kimaendeleo wapo mbali mno kuliganisha na sisi,tuacheni maneno maneno tujenge nchi kwa misingi ya kisheria,fumua na ondoa KATIBA hii na tutengeneze KATIBA ya wananchi SIO politicians.
Hutakiwi kuwa na nchi inayojisema kwamba ni Jamhuri yenye watu sawa, halafu bado ukawa na vyeo vya uchifu vya kurithimishana.

Ama ukubali kwamba watu si sawa, na kuna wengine wako juu ya wengine kwa kuzaliwa tu kwenye familia za kichifu, ama ukubali kwamba watu ni sawa na uchifu hauna maana kubwa ufutwe.

Nyerere alichagua kuunda nchi inayodhamiria kuwa na watu wote sawa.

Hili pia lilisaidia sana kuua ukabila na kujenga umoja wa kitaifa.

Kwa sasa naona tumeamua kurudisha uchifu kwa mlango wa nyuma.
 
View attachment 2091277
Kwani uchifu ni utamaduni wetu? Makabila mengi hawakuwa na wachifu. Waliwekwa na wakoloni kwa maslahi yao (km Wazanaki). Uchifu ulipigwa marufuku na sheria mnamo 1962. Machifu waliyokuwepo (km Adam Sapi, Fundikira, Kunambi nk) waliingizwa Serikalini katika nyadhifa mbalimbali.

Ufutaji wa uchifu ulitusaidia sana kujenga umoja wa kitaifa. Nchi zingine Za Afrika (kmNigeria, Ghana nk) wamepata shida kujenga umoja wa kitaifa. Sababu mojawapo ni machifu kulinda himaya zao kwa kukuuza ukabila badala ya utaifa. Tunachotakiwa kusisitiza ni utamaduni wa kitaifa.

Issa G. Shivji ni mwanasheria nchini Tanzania na mwandishi wa Vitabu, pia ni mmoja wa wataalamu bingwa katika Afrika wa sheria na masuala ya maendeleo.

Pia amewahi kufundisha na kufanya kazi katika vyuo vikuu mbalimbali duniani kote.
View attachment 2091732

Leo hii Hangaya anaona ndiyo wa kwamza kuukwaa huo uchifu.
 
Hili mimi sikubaliani nalo ni siasa tu,hebu angalia hizi nchi jirani yetu,Zambia,Namibia,Botswana,SA etc etc bado zina viongozi wao wa asili na zipo na umoja na kimaendeleo wapo mbali mno kuliganisha na sisi,tuacheni maneno maneno tujenge nchi kwa misingi ya kisheria,fumua na ondoa KATIBA hii na tutengeneze KATIBA ya wananchi SIO politicians.
Kwa watawala waliopo ukiwaambia habari za katiba mpya wanakuona kama unataka kuwatumbukiza kwenye mto wenye mamba wenye njaa kali.
 
wengi hawaoni mbali, hata mwalimu nae baadhi ya mambo hakuona mbali mfano katiba.
Kuna mambo ambayo inatubidi tumsamehe mwl JK Nyerere maana aliichukua nchi wakati dunia bado ipo mbali mbali.

Lkn kwa wanao yafanya sasa hawa watawala wetu kipindi ambacho dunia ni sawa na kijiji lazima tuwalaumu sana.
 
Hili mimi sikubaliani nalo ni siasa tu,hebu angalia hizi nchi jirani yetu,Zambia,Namibia,Botswana,SA etc etc bado zina viongozi wao wa asili na zipo na umoja na kimaendeleo wapo mbali mno kuliganisha na sisi,tuacheni maneno maneno tujenge nchi kwa misingi ya kisheria,fumua na ondoa KATIBA hii na tutengeneze KATIBA ya wananchi SIO politicians.

Mkuu are you serious. Kwa sababu ya uchifu SA .
 
Back
Top Bottom