Nyerere ....usawa wa binadamu! Hizi ni blah blah hakuna hiyo kitu na ona sasa politicians wetu wanavyorithiana from one generation to another!Hutqkiwi kuwa na nchi inayojisema kwamba ni Jamhuri yenye watu sawa, halafu bado ukawa na vyeo vya uchifu vya kurithimishana.
Ama ukubali kwamba watu si sawa, na kuna wengine wako juu ya wengine kwa kuzaliwa tu kwenye familia za kichifu, ama ukubali kwamba watu ni sawa na uchifu hauna maana kubwa ufutwe.
Nyerere alichagua kuunda nchi inayodhamiria kuwa na watu wote sawa.
Hili pia lilisaidia sana kuua ukabila na kujenga umoja wa kitaifa.
Kwa sasa naona tumeamua kurudisha uchifu kwa mlango wa nyuma.