Israeli yasalimu amri kuhusu balozi wa Brazil

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Israel imelazimika kufutilia mbali uteuzi wa mlowezi wa kiyahudi kuwa balozi wake nchini Brazil baada ya taifa hilo kukataa kumpokea.

benjamin_netanyahu_640x360_afp_nocredit.jpg

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.


Brazil ilipinga na ikakataa katakata kumpokea balozi huyo mteule kutokana na msimamo wake mkali dhidi ya wapalestina.

Aidha Brazil ilisema kuwa Dani Dayan ambaye aliongoza unyakuzi wa mashamba ya wapalestina katika ukanda wa ukingo wa Magharibi unamnyima uwezo wa wastani kisiasa.

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, amesma kuwa Dani sasa ataihudumia taifa hilo la kiyahudia katika ubalozi wake wa New York Marekani.

160328121756_dani_dayan_640x360_reuters_nocredit.jpg

Brazil ilikatalia mbali uteuzi wake mwezi Agosti. Kauli hiyo kali ya Brazil wachanganuzi wanasema kuwa ilielezea wazi msimamo wao dhidi ya unyakuzi wa ardhi ya wapalestina.

Awali Netanyahu alikuwa ameonya kuwa angechukua msimamo mkali dhidi ya Brazil iwapo ingeendelea kumkataa balozi huyo.

Chanzo: BBC Swahili
 
Hiyo ni kawaida katika masuala ya kidiplomasia maana hata Tanzania nao tulimkataa balozi wa Germany
 
Back
Top Bottom