Israeli yafanya mashambulio mapya Gaza licha ya maombi ya kusitisha mapambano

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
13,914
2,000
Israeli imefanya mashambulizi kadhaa alfajiri ya leo katika Ukanda wa Gaza, baada ya wanamgambo wa Palestina kurusha makombora ya roketi katika miji iliyopo kusini mwa Israeli.

Mashambulizi ya alfajiri ya Jumatatu ni makubwa zaidi tangu mapambano yaanze wiki moja iliyopita.

Israeli inasema imeshambulia majengo yanayomilikiwa na wanamgambo wa Hamas pamoja na nyumba kadhaa za makamanda wa kundi hilo, hata hivyo barabara kuu kadhaa na nyaya za umeme pia zimeharibiwa.

Mashambulio hayo yanatokea wakati jumuiya ya kimataifa ikitaka pande zote mbili katika mgogoro huo kusitisha mashambulizi.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) lilifanya mkutano wa dharura jana Jumapili na Katibu Mkuu wa UN António Guterres ameonya kuwa mapambano zaidi "yanaweza kusababisha hali mbaya ya kiusalama na kibinaadamu."

Guterres pia ametaka mapambano hayo "mabaya" yasitishe haraka iwezekanavyo.

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi ameeleza leo Jumatatu kuwa nchi yake "imepiga hatua kubwa katika kutafuta kusitishwa kwa mapambano...na matumaini bado yapo."

Lakini mpaka sasa hakuna dalili za hilo kutokea huku mapambano makali yakiingia wiki ya pili

Ghasia hizo ni zao la wiki za hamaki na wasiwasi baina ya Israeli na Palestina katika eneo la Jerusalemu Mashariki ambapo hali hiyo iliishia katika mapambano katika eneo takatifu kwa Waislamu na Wayahudi.

Kundi la Hamas, ambalo linaongoza Ukanda wa Gaza, likaanza kurusha makombora ya roketi baada ya kuionya Israeli iondoke katika eneo hilo la Jerusalemu, na hapo ndipo Israeli ilipoanza kufanya mashambulizi ya anga ya kulipiza.

Jeshi la Israeli linasema zaidi ya ndege 50 za kivita zimefanya mashambulizi ya dakika 20 muda mfupi kabla ya alfajiri ya leo.

Ndege vita hizo zimepiga na kuteketeza "maeneo ya kigaidi" 35 na kuharibu zaidi ya kilomita 15 za mfumo wa mahandaki yanayomilikiwa na Hamas, linadai jeshi la Israeli.

Jeshi hilo pia linadai kuwa limezipiga nyumba tisa za makamanda "wa ngazi ya juu" wa Hamas.

Hata hivyo hakujakuwa na idadi rasmi kufikia sasa ya watu waliofariki na kueruhiwa, lakini mamlaka za Palestina katika Ukanda wa Gaza zinasema kuwa mashambulizi hayo yamesababisha umeme kukatika katika maeneo mengi na kuharibu mamia ya nyumbana majengo mengine.

"Hakujawahi kuwa na mashambulizi ya ukubwa huu,"mkaazi mmoja wa Gaza ameliambia shirika la habari la kimataifa la AFP . Mad Abed Rabbo, 39, amesema alihisi "woga mkubwa na kutishika" wakati mashambulio hayo yakiendelea.

Kabla ya mashambulizi ya alfajiri ya leo, maafisa wa Palestina walitangaza kuwa mashambulio ya jana Jumapili yaliyosababisha vifo vya watu 40 ndiyo yalikuwa mabaya zaidi.

Source: BBC​

Screenshot_20210517-134711_Facebook.jpg
 

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
21,953
2,000
Hao Hamas hutegemea Israel wanyamaze bila kujibu kila wakishambuliwa, halafu mbaya zaidi hutumia majengo ya raia kurusha makombora ili majibu yaje kupiga wananchi kisha dunia ipige makelele.

Israel tembeza kipigo, Iran akimind sana ajitose humo tuone mwisho wake.
 

jeipm

JF-Expert Member
Sep 28, 2018
378
1,000
Mbona malipo ni hapa hapa duniani

Wasubirie tu malipo yao wakati ukifika halitabakia hata chembe ya jiwe juu ya jiwe
 

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
12,252
2,000
Heading ya kipumbavu umeweka Unaisema Israel and unaandika baada ya Hamas kurusha Makombora so Heading yako ime base upande wa lamawa upande mmoja umeutupia lawama wakati msababishaji as anaonewa wakati ndie mchokozi.

Wafia Dini mnashida sana fanatic... Ungeandika Mapambano yanaendelea kati ya Magaidi wa Hamas na Nchi huru Israel. Ni ujinga sana kuwaficha Magaidi Hamas kwa kutumia jina la Wapalestina.
 

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
13,914
2,000
Heading ya kipumbavu umeweka Unaisema Israel and unaandika baada ya Hamas kurusha Makombora so Heading yako ime base upande wa lamawa upande mmoja umeutupia lawama wakati msababishaji as anaonewa wakati ndie mchokozi... Wafia Dini mnashida sana fanatic... Ungeandika Mapambano yanaendelea kati ya Magaidi wa Hamas na Nchi huru Israel. Ni ujinga sana kuwaficha Magaidi Hamas kwa kutumia jina la Wapalestina...
Hayo ni maneno ya mwandishi wa BBC sio yangu sijaweka hata nukta
 

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
12,252
2,000
Hayo ni maneno ya mwandishi wa BBC sio yangu sijaweka hata nukta
Waandishi Extremists msiwape airtime Wanamezesha watu sumu mbaya sana ambayo inaingia hadi kwenye mizizi ya damu... haitoki lakini ukiangalia na kuchunguza unaona upuuzi na uchonganishi mtupu wa kupuzwa... Gaidi popote alipo hafai
 

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
13,914
2,000
Waandishi Extremists msiwape airtime Wanamezesha watu sumu mbaya sana ambayo inaingia hadi kwenye mizizi ya damu... haitoki lakini ukiangalia na kuchunguza unaona upuuzi na uchonganishi mtupu wa kupuzwa... Gaidi popote alipo hafai
Gaidi ni nani mkuu?? Aliyefurumusha makombora bila kuchokozwa au aliyelipiza?
 

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
13,914
2,000
Ndio maana wananyooshwa kwa sababu ya ujinga wao unajua huwezi kupambana unaanzisha mapigano unaakili kweli?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom