Israel yapata hasara ya dola milioni 160 kwa mashambulio ya muqawama

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
6,210
2,000
Wazayuni wakiri kipigo, wameshapata hasara ya dola milioni 160 kwa mashambulio ya muqawama

May 13, 2021 11:53 UTC

[https://media]

Chama cha Wazalishaji Bidhaa cha utawala wa Kizayuni kimetangaza kuwa, tangu yalipoanza mashambulizi ya makombora wanamapambano wa Palestina siku chache zilizopita hadi hivi sasa, sekta ya uzalishaji bidhaa ya Israel imeshapata hasara ya dola miliioni 160.

Shirika la habari la FARS limenukuu taarifa ya chama hicho cha wazalishaji bidhaa cha Wazayuni kikiri leo Alkhamisi kuhusu hasara kubwa iliyosababishwa na mashambulio ya makombora ya wanamapambano wa Palesitna na kuongeza kuwa, sekta mbalimbali za uchumi wa Israel zimepata hasara katika mashambulizi ya tangu siku tatu zilizopita ya makombora ya wanamapambano wa Palestina.

Taarifa hiyo imesema pia kuwa, wanamuqawama wa Palestina wameshayapiga kwa makombora 540 maeneo mbalimbali ya kiuchumi ya Israel katika kipindi cha siku tatu zilizopita na kuusababishia utawala huo katili hasara ya dola milioni 160.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom