kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,991
- 17,890
Israel yalazimika kukiri nguvu kubwa za kijeshi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Sep 13, 2021 02:27 UTC
[https://media]
Waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kuwa droni yaani ndege zisizo na rubani za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zina uwezo mkubwa wa kufanya mashambulizi makini na angamizi.
Kwa mujibu wa mujibu wa tovuti ya habari ya "Arab24," waziri wa vita wa Israel, Benny Gantz alikiri jana (Jumapili) kwamba moja ya zana muhimu za kijeshi za Iran ni ndege zake zisizo na rubani ambazo ni kama makombora ya balestiki na ndege za kivita, zinaweza kuruka umbali wa maelfu ya kilomita na kufanya mashambulizi makini na angamizi.
Kabla ya hapo pia, Uzi Rubin aliyepewa lakabu ya baba wa makombora ya utawala wa Kizayuni wa Israel alikuwa naye amekiri nguvu na uwezo mkubwa wa kijeshi wa Iran akisisitiza kuwa, maenendeleo ya haraka iliyopita Iran katika miradi yake ya anga za mbali isiyo ya kijeshi na ya kijeshi, ni jambo linalotia wasiwasi mkubwa.
[https://media]Benny Gantz, waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel
Kamanda mwingine wa ngazi za juu wa jeshi la utawala wa Kizayuni naye pia amekiri kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo wa kufanya mashambulizi makali na hatari kwa Israel na kuisababishia Tel Avavi hasara kubwa.
Meja Jenerali Aharon Haliva ameendelea kusema, ishara zote zinaonesha kuwa, kutaka na kukataa, mwaka 2020 si mwaka wa mafanikio ya kiusalama kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.