Israel yaishutumu Marekani kwa kupanga kura dhidi yake

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,552
2,000
Waziri mkuu wa Israeli amefanya kikao na balozi wa Marekani nchini humo baada ya kuamuru afike mbele yake kueleza kwa nini Marekani ilipitisha mswada wa mazungumzo katika Umoja wa Mataifa wa kuikosoa Israeli.

Maelezo zaidi kuhusu mkutano huo hayajatolewa.

Hatua hiyo inajiri baada ya Israel kuwaita mabalozi wa mataifa mengine ambao waliunga mkono kura hiyo dhidi ya Israel.

Netanyahu: Israel haitaheshimu azimio la UN, Ban Ki-moon akosoa pendekezo la Netanyahu Israel yawashtumu mabalozi wa UK, Urusi, China na Uhispania.

Mkutano huo unajiri baada ya Israel kuapa kuchukua hatua za kulipiza kisasi kwa kile ilichokitaja kuwa ''hatua ya aibu'' iliochukuliwa na Marekani.
Hatua hiyo ambayo imekosoa ujenzi wa Israel katika eneo la West Bank na Jerusalem ilipitishwa baada ya Marekani kutoshiriki katika kura hiyo badala ya kutumia uwezo wake wa kuipinga.

Mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa uliokosoa mpango wa Israel kutekeleza ujenzi katika maeneo ya Palestina.

Israel imeishutumu Marekani ,ambaye ni mshirika wake wa karibu na mkosoaji wa ujenzi wa makaazi katika eneo la Palestina kwa kuanzisha kura hiyo-swala ambalo Marekani imekana.
''Kutokana na habari tulizonazo ,hatuna wasiwasi kwamba serikali ya Obama ilishinikiza kura hiyo ikashiriki pakubwa na kutaka ipitishwe'', alisema waziri mkuu Benjamin Netanyahu.

Chanzo: BBC
 

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
6,919
2,000
Baada ya Misri kuwithdraw pendekezo lake kutokana na pressure ya Israel, nahisi Obama alicoordinate na nchi nyingine kimyakimya na kuandaa resolution nyingine mbadala kimyakimya. Ukiangalia nchi zilizosponsor hiyo resolution moja ya Africa Senegal, nyingine ya Asia Malaysia, Nyingine ni ya America kusini Venezuela, na nyingine ni New Zealand , yaani composition inayoreflect World Community.
Huu mpango inaonekana ulisukwa kitaalam.sana kiasi kwamba Mossad walishindwa kuung'amua.
Mwanzo walistukia mpango wa kura kwenye baraza la Usalama dhidi yao yaani ule wa Misri, Misri alivyowithdraw wakajua wamemaliza, kumbe wanaume wapo wanadraft resolution nyingine kimyakimya!.

Resolution hii imeiweka Israel ktk hali ngumu kwa sababu inaandaa mazingira ya step ngumu zaidi kuchukuliwa dhidi yao ikiwemo vikwazo ( japo hili ni ngumu kutokana na Veto ya wamarekani lakini huwezi jua huko mbeleni maana hakuna marefu yasiyo na ncha)
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,815
2,000
Wakati mwingine mtoto ukimdekeza udhani unamwogopa, ni waafrica tu hasa watanganyika ndo wamebaki watumwa wa kifra wa Israel wazungu wameshawachoka mpaka baba mlezi US ameshaonyesha dalili ya kuwachoka na kwa Trump watapata wakati mgumu sana na muda si mrefu Israel inakwenda kuwekewa vikwazo vya uchumi na UN
 

Wickama

JF-Expert Member
Mar 8, 2009
1,466
1,500
Huu mpango inaonekana ulisukwa kitaalam.sana kiasi kwamba Mossad walishindwa kuung'amua. Mwanzo walistukia mpango wa kura kwenye baraza la Usalama dhidi yao yaani ule wa Misri, Misri alivyowithdraw wakajua wamemaliza, kumbe wanaume wapo wanadraft resolution nyingine kimyakimya!.
Ukisikia kutumia akili ndio kama scenario hii. Obama kavumilia sana vitimbi vya Israel na jeuri yao ya kudhani wanaihodhi Marekani. Majuma machache hajaondoka hatimaye kamlipa Netanyahu stahiki yake ya dharau aliyomfanyia kwenda kulihutubia bunge la congress Marekani bila hata kuishirikisha White house. Hivi Kiongozi yupi wa nje anaweza kwenda Israel ahutubie Knesset bila Netanyahu kushirikishwa? Angalia tena, kitendo cha waIsrael kumkimbilia Trump ili aokoe jahazi pia ni dharau na mwendelezo wa kudhani wanawahodhi Wamarekani japo walipaswa kujua Marekani ina rais mmoja kwa wakati mmoja. Hata Trump akiingia, mpango huu umeshapitishwa na Security Council hautakaa uondoke. Period.
 

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
6,919
2,000
Ukisikia kutumia akili ndio kama scenario hii. Obama kavumilia sana vitimbi vya Israel na jeuri yao ya kudhani wanaihodhi Marekani. Majuma machache hajaondoka hatimaye kamlipa Netanyahu stahiki yake ya dharau aliyomfanyia kwenda kulihutubia bunge la congress Marekani bila hata kuishirikisha White house. Hivi Kiongozi yupi wa nje anaweza kwenda Israel ahutubie Knesset bila Netanyahu kushirikishwa? Angalia tena, kitendo cha waIsrael kumkimbilia Trump ili aokoe jahazi pia ni dharau na mwendelezo wa kudhani wanawahodhi Wamarekani japo walipaswa kujua Marekani ina rais mmoja kwa wakati mmoja. Hata Trump akiingia, mpango huu umeshapitishwa na Security Council hautakaa uondoke. Period.
Halafu pia nimegundua kuwa Trump lina akili kichizi!. Lenyewe linaweza kusema hili au lile leo, kesho likishapata linachokitaka linaachana na slogan zake.

Lilisema linataka kumfunga Clinton, wamarekani wababe wakafurahi, sasa linasema ile ilikuwa ni kauli ya kisiasa tu.

Lilitangaza kudrain the swamp washington, sasa hivi hiyo swamp ndo kwanza limeipalilia kwa kujaza kambale wenye sharubu.

Najua na sasa hivi linatafuta uungwaji mkono wa Jewish lobby machine, ambalo lilikuwa linamuunga mkono clinton, na pia linatafuta uungwaji mkono na Jewish Media powerhouses. Likishafanikiwa litatawala kwa amani, Ila Waisrael wajue kuwa Trump ni unpredictable, anawexa akawaumiza kuliko Obama!.

Kwa sasa Waisrael wanahofia Ile Paris Conference, Israel inaogopa maazimio yaliyofikiwa yanaweza kwenda kwenye security council na kupigiwa kura kabla Obama hajaondoka madarakani tarehe 2. January!
 

Raskazoni

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
244
250
Wanaondeshwa na Israel Lobby ni wale wanaofadhiliwa nao, Trump hakufadhiliwa na maisraeli so anaweza kuamua analotaka , ana Fedha ana power kazi kwako
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom